PreGE2025 Huu mwaka mgumu sana kwa CHADEMA, kitatoboa kweli?

PreGE2025 Huu mwaka mgumu sana kwa CHADEMA, kitatoboa kweli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tulishaona tangia awali CDM inaenda kufa kwenye mikono ya TAL.

G55 wasikilizwe wana hoja za msingi.

Hauwezi kuzuia uchaguzi uliopo kisheria ,TAL mara nyingi kikianza kunuka anakimbia ubelgiji anawaacha wenzake magerezani wanasota ,wao washajijenga Heche ana bioashara zake ambazo zinamuingizia zaidi ya milioni 600 kwa msimu wa mavuno ,G55 wanataka nao wajaribu bahati yao maana walishawekeza senti zao kujenga chama.

WaTZ walivyo waogoa wakiona polisi tu barabarani wanaweza hata kuogopa kutoka ndani ,kwahiyo kuzuia uchaguzi haipo ,washiriki uchaguzi ila wapambane zaidi kimkakati kama walivylianzisha jimbo la Kinondoni....hao watu walifanya mapinduzi hivyo hawezi kuondolewa kwa kikaratasi lazima CDM ipambane hasa na si kwa kususa ,ukisusa wao wala si mmemsikia Nchimbi? Nchimbi ameongea ukweli mtupu hata vyama vyote vikisusa ikabakia sisiemu uchaguzi utafanyika tu ila kura itakuwa ndiyo au hapana.
Haja zao ni sawa na zile la kundi covid19 hivi sasa napendekeza jina liwe mpox55
 
Niliwahi kufikiri chadema ni chama imara kilichokomaa kumbe nilijidanganya.sikufanya utafiti wangu vizuri.Kwa macho ya juu kilionekana imara na kina watu smart kumbe kwasababu kulikua na viongozi waliokubali kubeba mapungufu ya wengine kwenye mitazamo ili chama kiwe na kauli moja.Sasa hivi kila mtu ni kambale uko mitandaoni,alafu kuna wale wenye mihemko wanasema fukuza wote watakuja wengine uku hawasemi hao wengine watakuja lini na kuongeza jambo gani kubwa nakwamuda gani.Kwasababu chama huu umaarufu wasasa ni kwasababu kuna ambao walitumia miaka kukiweka chama hapo kilipo leo.Hii agenda ya Reform kuelekea uchaguzi mimi binafsi naona ni jambo gumu kutekelezeka,kwasababu anayetakiwa aruhusu hiyo reform walianza naye maridhiano badae wakayabeza,kwahiyo walikimbia kumkaba kwenye mazungumzo ambayo ilikua ni njia rahisi yakupenyeza agenda yao kuliko hii yasasa kuelekea uchaguzi..sasa hivi ili hili hiyo agenda yao ifanyiwe kazi wanatakiwa wawe na nguvu zakila namna zitakazo mshurutisha yule yule waliyemkataa jambo ambalo naona hawawezi.Angalau pale walipogomea maridhiano wangekuja na agenda ya hakuna KATIBA MPYA hakuna uchaguzi ningewaona wana hoja ya msingi.Agenda ya kutishia uchaguzi haina maslahi mapana ya nchi kuliko agenda ya Katiba Mpya ambayo ingegusa maisha ya wananchi wote na wengi wangeielewa kirahisi.ndo maana utaona uchaguzi uliopita Magufuli alichagua viongozi aliowataka nchi nzima na nchi bado ipo na maisha yanaendelea.Kwasababu wasijidanganye kua kuna wananchi wengi serious wanayeweza kupambania mabadiliko serious zaidi mihemko na mbwembwe nakujiaminisha mitandaoni.Mimi nilidhani kwakua tumesema mbowe alilamba asali basi uongozi wasasa ungekuja na kitu tofauti chakwenda na hiyo nguvu yao kwenye uchaguzi nakuhakikisha hakuna mgombea wao anaenguliwa au kuibiwa kura ili wapate wabunge na madiwani wengi watakao wapelekea kuongeza msukumo wa mabadiiko ya tume ya uchaguzi na katiba mpya wakiwa ni sehemu ya vikao vitakavyoendelea.Lakini kumbe nawao wanategemea hisani ya reform kutoka kwa raisi wa nchi.Ndo maana naona hiyo reform nikwaajili ya maslai yao yakisiasa sio swala la wananchi wote.Sasa ninachokiona sasa hivi yote hayo hayawezekani kwasababu muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu ni mchache sana.Hadi waje wamalize kuzodoana na kufukuzana alafu waje wapate watu sahihi wakupambana na hiyo agenda yao nchi nzima watakua wamechelewa.Wakumbuke pia umaarufu wao mwingi uliongezeka kipindi kuna siasa za nginjangija sasa hivi siasa ni laini wanapaswa kua na agenda zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja.Mimi naona kuna kitu wanajichanganya kama chama ha siasa kinachofikiriwa kua mbadala.Ngoja tuone muda utatupa majibu.
 
Kwa kusudi la Mungu mwenyewe Chadema itavuka na itakuwa mshindi kwenye hii battle hutaamini!
Siasa ni mikakati sio swala la Mungu.Wenzetu wazungu wangekua wanamsubiri Mungu kwenye kila jambo lao wangechelewa sana kama ilivyo waafrika leo.Mungu alitupa akili lakini bado tunamsuubiri aje kutufanyia uku tukijipa matumaini.
 
CHADEMA kinateswa na masalia/mapando ya Mbowe na mapandikizi ya mfumo
Jeuri ya msingida na kukosa hekima ya kuua makundi ya uchaguzi ndio chanzo cha maadui kupata nguvu.Alitakiwa asikie kauli ya Mbowe kwamba waponye majeraha ya uchaguzi.Lisu anajua kuongea ila kakosa mbinu za uongozi,bora hata achote hekima kwa Heche
 
Kabisa mkuu..
Mimi sikubaliani kabisa na uchaguzi unavyoendeshwa na TAMISEMI na NEC ila pia sikubaliana na kutoshiriki uchaguzi kwa CDM ,CDM kutoshiriki ni sawa na muuza nyama kumsusia fisi bucha...sisiemu watafurahi sana CDM ikisusia uchaguzi.
 
Back
Top Bottom