Mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhuru wa Tanzania, ni taa yenye kumulika nchi na miradi yake.
Ni nyota inayotukumbusha kwamba uhuru ni jambo muhimu na la kipekee kwa binadamu aliye kamili.
Hivyo basi hata hapo kwenye foleni yakupasa uwe na fikra chanya ya kutafakuri uzuri na ubora wa Mwenge na siyo kwamba unapoteza muda.
Ni muhimu kila Mtanzania akaguswa na Mbio za Mwenge, ukiwemo wewe uliyeguswa ukiwa kwenye foleni.
Usijinunishe bali furahi na tafakari huu utamaduni wetu adhimu wa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru.
Sema Mwenge oyeeeeee