Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company - RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit - TECU).
Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.
Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu - Ifakara kwa kiwango cha lami, Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.
Barabara ya Kidatu - Ifakara na Daraja la Ruaha Mkuu imefunguliwa rasmi leo Agosti 04, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.