Huu ndio Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu (Mita 133) katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara

Huu ndio Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu (Mita 133) katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara

Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara sehemu ya Kidatu - Ifakara kilometa 66.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Morogoro.

Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company - RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit - TECU).

Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.

Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu - Ifakara kwa kiwango cha lami, Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Barabara ya Kidatu - Ifakara na Daraja la Ruaha Mkuu imefunguliwa rasmi leo Agosti 04, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hilo daraja la chuma limetutesa sana wakazi wa Ifakara. Ilikuwa ni mwendo tu wa kusubiriana. Gari za upande wa pili kuzisubiri gari nyingine zipite kwanza.

Ahueni ndugu zangu wa Ifakara, lami imewafikia.
 
Mradi ulianza 2017 wanasema, ukakamilika 2024! Umbali ni km 67 nadhani, daraja likiwa na mita 133.

Gharama ni 157bn, eti wamelipa fidia pia.

Tunajenga km 70 kwa miaka 7? Wastani wa 10km kwa miezi 12?
Tunajenga km 1 kwa 2.25bn?
#WajinGaSiSi.
 
Hilo daraja la chuma limetutesa sana wakazi wa Ifakara. Ilikuwa ni mwendo tu wa kusubiriana. Gari za upande wa pili kuzisubiri gari nyingine zipite kwanza.

Ahueni ndugu zangu wa Ifakara, lami imewafikia.
Mkuu hawa vijana wanadai ni kazi ya samia wakati ni magufuli

Japokuwa sikuwa namkubali ila hawa vijana ni wa hovyo sana
 
Kumbe mbali hivyo , almost dar shinyanga ?

Sidhani kama ni kweli
Unabishi nn?..mm nipo nasafirisha Tv yangu hisense inchi 55...nimepakata sijui kama ntafika nayo haijavunjika roho juu tu....ni masaa 12 na zaidi kufika malinyi huko mbele
 
Unabishi nn?..mm nipo nasafirisha Tv yangu hisense inchi 55...nimepakata sijui kama ntafika nayo haijavunjika roho juu tu....ni masaa 12 na zaidi kufika malinyi huko mbele
Unaenda wapi?
 
Inawezekana. Maana ya kutokea Namtumbo inaanzia Malinyi huko. Hiyo ni kuelekea Ifakara. Mbele ya Ifakara ndo kuna ya kwenda Namtumbo.

Hapo pembeni ya daraja kulikuwa na imani ya kuwepo chunusi. Enzi nipo K1 (Kilombero Sugar), daraja lilikuwa la kuvuka gari moja, mnafanya kusubiriana. Atakayewahi ndo anapita. Mbele hapo kulikuwa na stendi ya Mkamba
Hiyo Ndo njia wazee wetu zamani walikuwa wanaenda kwa mganga Binti Kalembwani!!
 
Back
Top Bottom