Huu ndio Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu (Mita 133) katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu lenye urefu wa mita 133 katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara sehemu ya Kidatu - Ifakara kilometa 66.9 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Morogoro.

Daraja hilo limejengwa na Mkandarasi Reynolds Construction Company - RCC ya Nigeria na Mhandisi Mshauri kutoka Kitengo cha Uhandisi (TANROADS Engineering Consulting Unit - TECU).

Usanifu na maandalizi ya nyaraka za zabuni ulifanywa na Kampuni ya kihandisi ya Crown-Tech Ltd ya Tanzania.


Ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu limejengwa sambamba na barabara ya Kidatu - Ifakara kwa kiwango cha lami, Ujenzi ulianza 02 Oktoba 2017 na kukamilika 30 Juni, 2024 kwa gharama ya Shilingi Billion 157.15, ikihusisha ujenzi wa barabara, daraja, usimamizi na fidia ya mali zilizoathiriwa na mradi.

Barabara ya Kidatu - Ifakara na Daraja la Ruaha Mkuu imefunguliwa rasmi leo Agosti 04, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 
Mama anaupiga mwingi sana
 
Hili litapewa jina la rais gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…