Huu ndio Muonekano wa Daraja la Ruaha Mkuu (Mita 133) katika barabara ya Mikumi- Kidatu - Ifakara

Daraja hili halina hata taa za barabarani Wala deflectors kwa pembeni?? Designing process ilikuwaje Hadi wamesahau kuweka vitu hivi muhimu???
 
Daraja hili halina hata taa za barabarani Wala deflectors kwa pembeni?? Designing process ilikuwaje Hadi wamesahau kuweka vitu hivi muhimu???
Mradi ulianza 2017 wanasema, ukakamilika 2024! Umbali ni km 67 nadhani, daraja likiwa na mita 133.

Gharama ni 157bn, eti wamelipa fidia pia.

Tunajenga km 70 kwa miaka 7? Wastani wa 10km kwa miezi 12?
Tunajenga km 1 kwa 2.25bn?
 
Zinafika Km ngapi kutoka hapo Moro Hadi pale Lumecha pachani?
Nimefanya utafiti wangu nimebaini umbali wake ni kama hivi ifuatavyo:-
1. Umbali wa kutoka Morogoro Mjini Hadi Mikumi ni 120 km.
2. Mikumi Hadi Kidatu ni 35 km.
3. Kidatu-Ifakara-Lupiro-Malinyi - Lumecha Namtumbo ni 486 km

Hivyo basi, JUMLA ya Umbali wa kutoka Morogoro Mjini-Mikumi-Ifalara-Malinyi hadi Lumecha Namtumbo ni Kilomita 641.

Aidha, umbali wa kutoka Dsm hadi Morogoro ni 196 km.

Hivyo, umbali wa kutoka Dsm- Morogoro-Mikumi-Ifakara-Malinyi-Lumecha Namtumbo ni Kilomita 837.
 
Hapo sawa so Ni kama masaa 11 hivi kwa basi .
Unatoka zako Songea kabla jua halijazama upo DSM au unashuka Moro unaingia kwenye SGR
 
Kweli kasimamia, maana pesa ya ujenzi walitoa israel toka mwaka 2017 ndio barabara imekamilika leo
Huo mradi wa jiwe kwani umesahau lijualikali alipiga mpaka magoti akiomba hiyo rami ijengwe jiwe akapiga simu ujenzi ukaanza hapo hapo
 
Hii road ndo itakuja Hadi huku Namtumbo??
Inawezekana. Maana ya kutokea Namtumbo inaanzia Malinyi huko. Hiyo ni kuelekea Ifakara. Mbele ya Ifakara ndo kuna ya kwenda Namtumbo.

Hapo pembeni ya daraja kulikuwa na imani ya kuwepo chunusi. Enzi nipo K1 (Kilombero Sugar), daraja lilikuwa la kuvuka gari moja, mnafanya kusubiriana. Atakayewahi ndo anapita. Mbele hapo kulikuwa na stendi ya Mkamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…