Huu ndio ushauri pekee aliopewa Mkapa na Mwalimu Nyerere alipokuwa akiunda serikali yake 1995

Ujumbe umefika pahali pake
Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.

Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.

Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"

Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."

Hizi zilikuwa ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
 
Kwa sasa hatupangiwi
Sikuuliza hilo la ushauri kuwa 'valid' lini au bado uko 'valid' leo. Tafadhali nielewe.

Labda nikupe 'hint' kidogo ndipo utaelewa.

Huyo aliyepewa ushauri huo hapo 1995, na yeye leo anatoa ushauri huo huo kwa mtu wake?
 
Rest in eternal peace my present. You were a true patriot who dared to reform our beloved Tanzania.

Your legacy will forever live on.
 
Nimeshindwa kuamini baada ya kuliona baraza la JPM la muhula wake wa pili, sijui ni nani wanaomshauri kwenye mambo haya.

Lakini hiki alichokifanya kina weka 'precedent', kwamba pindi tukapopata rais kutoka upande wa pili basi watu wasije kulalamika akiteua wengi wa upande huo.
 
Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.

Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.

Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"

Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."

Hizi zilikuwa ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
Ulikuwa ushauri mzuri kwa kila anayetaka mema nchi hii, lakini wenye nyoyo na nyuso za viburi nyuma ya miwani ya mbao hawawezi kuona umuhimu wake.
 
Back
Top Bottom