Sasa wewe lile disco la pale mjini Rita unajua enzi hizo lilikuwa linaitwaje??Labda ni umri ndio unanitupa mkono, lakini enzi zetu DJ alikua ni 'Disc Jockey' na hakua na uhusiano wowote na mambo ya siasa za nchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa wewe lile disco la pale mjini Rita unajua enzi hizo lilikuwa linaitwaje??Labda ni umri ndio unanitupa mkono, lakini enzi zetu DJ alikua ni 'Disc Jockey' na hakua na uhusiano wowote na mambo ya siasa za nchi.
Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.
Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.
Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"
Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."
Hizi zilikuwa ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
Mr. Clean Benjamin Mkapa
Ushauri wa mwalimu ulikua valid 1995, bado ni valid 2020 na utaendelea kuwa valid miaka mingi baadae.
Unabisha?Unao ushahidi?
Sikuuliza hilo la ushauri kuwa 'valid' lini au bado uko 'valid' leo. Tafadhali nielewe.
Labda nikupe 'hint' kidogo ndipo utaelewa.
Huyo aliyepewa ushauri huo hapo 1995, na yeye leo anatoa ushauri huo huo kwa mtu wake?
Matumaini yapo, nafasi ya kurekebisha makosa ya 2015 ipo. Wahusika wanapaswa kuwa na ujasiri na kujitoa kwa maslahi ya nchi.
Ni kweli kabisa hatupangiwi, lakini mipango yetu inaweza kuvurugika.Nani kakudanganya kuwa tunapangiwa sisi?
Labda awamu hii ikimaliza muda wake!!!
Dalili sio nzuri kabisa.L
Labda awamu hii ikimaliza muda wake!!!
Ni lini mimi na wewe hatujui!!
Ulikuwa ushauri mzuri kwa kila anayetaka mema nchi hii, lakini wenye nyoyo na nyuso za viburi nyuma ya miwani ya mbao hawawezi kuona umuhimu wake.Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.
Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.
Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"
Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."
Hizi zilikuwa ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
Kabisa.Ulikuwa ushauri mzuri kwa kila anayetaka mema nchi hii, lakini wenye nyoyo na nyuso za viburi nyuma ya miwani ya mbao hawawezi kuona umuhimu wake.
Kuna wanufaika na dalili hizo Mkuu.Dalili sio nzuri kabisa.