Huu ndio uzalendo wa kweli. Unakataa rushwa ya mil 5 unapokea cheti

Huu ndio uzalendo wa kweli. Unakataa rushwa ya mil 5 unapokea cheti

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Askari wa Kiteto Koplo Ismail Ally Juma amepongezwa na kupewa cheti kwa kitendo chake cha kukataa shilingi milioni 5 kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa anasafirisha wahamiaji harama 11 wakitokea Ethiopia kuelekea Afrika ya kusini.

Koplo Ismail ni miongoni mwa askari 13 waliopongezwa na Kamanda wa Polisi Manyara ACP George Katabazi kwa utendaji wao bora kwa mwaka 2021 - 2022.

1668190430026.png

 

Jeshi la polisi ni dhalimu. Hii kila mtu anafahamu. Hawa ni wapokea rushwa wakubwa.

Hatahivyo, ikitokea askari anayejielewa na akatenda haki basi mimi nampongeza.

Mwisho, kuwaita waafrika wenzako masikini wahamiaji haramu hii si sawa.

Hao ni raia wenye dhiki wanaojaribu kutafauta namna tu wapake mkate wao wakila siku.

Umesikia wewe kamanda mchovu?
 
Wewe unatetea rushwa?

Unadhani hata angechukua ingemsaidia kwa lolote?

Njaa isikutoe akili.

Ukiwa mtu mwema, baraka zipo miguuni mwako.

Vile hujui tu
Umeandika kwa urahisi utadhani ukiambiwa changia JF "alufu salasini" unazo!Muwe mnaacha unafiki.
 
Umeandika kwa urahisi utadhani ukiambiwa changia JF "alufu salasini" unazo!Muwe mnaacha unafiki.

Sasa mimi nisipokuwa na 30 thousand yakuchangia JF wewe shida yako ni nini hasa?

Unafikiria kwakutumia masaburi?

Hapa tunazungumzia hukuhu rushwa.

Huoni ni ujua kutetea rushwa?
 
Back
Top Bottom