Huu ndio uzalendo wa kweli. Unakataa rushwa ya mil 5 unapokea cheti

Watanzania siku hizi wamekua Wajinga sana kwenye Rushwa,yaani kila Mtu eti anaona Rushwa ni haki yake,na usipompaa Rushwa anakuona wwe siyo wamaana hata kidogo!!
Tumejifunza kwa viongozi wetu watukufu..
Sema wao wanakula parefuuuu hadi raha.
 
Atakuwa aikataa kwa kuhisi ni mtego yawezekana hakuwahi kupokea rushwa kubwa hivyo ..yake ilikuwa elfu hamsini au laki...
Iliwahi kunitokea askari kunipeleka polisi baada ya KUMPA elfu kumi kwa kosa la kutokufunga mkanda..

Baadae baada ya kuzoeana aliniambia kuwa kosa Hilo huwa anapewa buku mbili siyo kumi...
 
Huyu Askari kukataa hivyo vijisenti haisaidiii chochote wakati walioko juu yake wanazipiga rushwa kama hawana akili nzuri.
Hapo anaweza undiwa zengwe hata ukoplo kunyofolewa.... Matarajio ni kupokea na kupeleka %kwa wazee ... Unapewa cheti huku nyuma ukipigwa madongo kuwa ni punguani na kiherehere !!! Ingekuwa sivyo rushwa ingekuwa historia katika taifa hili kwani watumishi wengi wanauadilifu lakini.... !!!!
 
😁😁😁😁 si cheki kwa kufurahi hapana ila najiuliza siku ya pili akipewa million 5 tena ataikataa akapate cheti kingine au
 
Watanzania siku hizi wamekua Wajinga sana kwenye Rushwa,yaani kila Mtu eti anaona Rushwa ni haki yake,na usipompaa Rushwa anakuona wwe siyo wamaana hata kidogo!!
Alaf wakisikia kuna mtu kalamba bil kadhaa peke yake wanafura tena
 
Nachofahamu mimi hakuna mtu asiyependa hela hata hawa wanaoponda humu mindatandaoni wanajifanya wakemea rushwa ila hela ikikaa kihasara hasara mbele yao wanapita nayo.

On other hand huyo askari atakuja kufanikiwa mbinguni ila hapa duniani ajipange kusaga meno(kufa njaa) juzi tu tuliona mapolisi mkilialia njaa huko magazetini,leo eti unakataa hela kwakipi unachofanyiwa na hao masisiemu?

Ingekuwa mimi saivi ningepitanayo 5M.[emoji23]
 
Usawa huu unakataa ml 5 kwa issue ambayo haina madhara yoyote,pole zake.cheti akabandike ukutani kwa ajili ya ukumbusho
 
Wanasiasa wanaona? Huu ndio uzalendo, je wao wanauweza?
 
Huyu sio kavunja record huyu? Unakataa hela unakubali makaratasi
 
Amefanya Vema Aitwe Bungeni Apongezwe Chap
 
Askari wa namna hiyo wapo wengi sana.Tatizo linaanza pale kiongozi mkubwa kama waziri au mkubwa wako kazini kusikia amekula bilioni moja ya umma na kuwafanya askari kupata hasira na kuanza kupokea rushwa hadharani
 
Yaani kamanda ameacha hela amechukua cheti maajabu haya
Huyu hata polisi wenzake,sahv wanamshanga....
Na asipokuwa makini anaweza ingia kwenye mgogoro na baadhi ya askari
Huo mfumo/mtandao una wenyewe ohoooo
So mnakumbuka kile kisa,cha askari mmoja kipindi cha nyuma alikata rushwa
Akapewa cheti,lakini badaye zengwe alilokutana nayo kazini

Kwa huyu askari wangempa cheti +mln 7 angalau

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…