BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,185
- 8,715
Wanabodi,
Lazima tuwe watu wapya, watu wapya wenye maono mapya, watu wapya wenye mtazamo mpya, watu wapya walio na hamu mpya ya usawa, haki na ujumuishaji, watu wapya wanaobeba Mwenge wa Tanzania mpya, ambayo haki na uhuru kwa wananchi unaheshimiwa na kulindwa tusikubali kuogozwa na wahuni.
Huyu jamaa Chadema wamemtoa wapi sijui sasa hivi ndiyo mtaji wao wa kisiasa kuelekea kuchukuwa dola na kupata katiba mpya, wakati yupo jela nilidhani mtu mmoja makini sana mwenye ushawishi kwa jamii kumbe hali yale ndiyo hiyo.
Cha kushangaza anaongea pumba wafuasi wa Chadema wanamshangilia masikini daaah huyu jamaa Chadema wanamtegemea kuwa mrithi wa Mbowe.
Kwenye swala la katiba hata mimi naunga mkono ipitishwe, tumpe muda huyu mama kama alivyosema...ila huyu mdude na maneno yake yasiyo na hekma, tena ya kibabe haswaa, hafai kuwa kiongozi...Chadema kuweni makini sana na watu wa style hii, mtapotea aise!