Huu ni aina ya utapeli au ni watu wamekosa kazi ya kufanya na wanaofanya haya wanataka nini? Labda kutaka kukukomoa sijui!

Huu ni aina ya utapeli au ni watu wamekosa kazi ya kufanya na wanaofanya haya wanataka nini? Labda kutaka kukukomoa sijui!

Kuna watu wanakupigia simu eitha uwape namba ya dreva tax,bodaboda wakiomba huduma eneo fulani au Kama una namba zao uwapigie waende walipo hasa maeneo yanayotajwa ni yale wanayojua ulipo hayawezi kukosa,makanisa,shule,stendi,kiwanja cha mpira au soko

Ukimwambia bodaboda au dreva tax nenda sehemu fulani kuna mteja akifika eneo tajwa hakuna mtu na namba haipatikani,inabidi anarudi anakwambia huyo mtu hayupo na kama sehemu ni ya mbali anadai umpe nauli ya usumbufu au anampigia dreva au bodaboda njoo sehemu fulani unichukue akifika hakuti mtu au

Anakuomba umwambie bodaboda au dreva tax anunue kitu fulani aende nacho akifika atampa hela yake na nauli,ukinunua akaenda nacho hakuti mtu na simu haipatikani

Je umewahi kukutwa na kisa hiki ?

Hawa watu wamekosa kazi ya kufanya au wanataka nini?
Ndugu ninakushangaa mno kwa kiwango cha ujinga ulio nao. Inawezekanaje mtu humfahamu akuagize jambo? Pia kwa jinsi bodaboda zilivyotapaka hawezi kupata huko aliko? Dah! Inatia hasira mno uwepo wa watu wajinga kama wewe nchini.
 
Huyo
Na nani anayekufanyia hivyo? Anakujua huyo mtu au? Kwanini mtu from nowhere akupigie simu alafu akuagize kitu nawe ufanye?
Huyo alienipigia simu kumhitaji boda boda alinitaja kwa jina langu, anaomba namba y boda ninaye mfahamu, ikabidi nimpigie boda kwanza kwamba kuna mtu yupo sehemu fulani anahitaji usafiri nimpe namba yako , boda akakubali namba yake nimpe.
Nilimpa namba wakawasiliana akamuagiza mchele na mafuta, akifika atampa hela, boda ameenda kununua anafika eneo husika kupiga simu hapokei, libidi nilipe mimi mchele na mafuta na usafiri.
 
Back
Top Bottom