Huu ni mwaka wa kusafiri sana kuifaidi dunia

Maswali mazuri, tutajitahidi kuyafafanua kama ifuatavyo:

1. Ukisoma maelezo ya package utaona kuna siku 4 hadi 5 za kuwepo huko. Siku zinaanza kuhesabika pale utakapopokelewa kwenda hotelini...
Ahsante kwa majibu mazuri ila nina bado sijaridhika.

1.Kushindwa kujibu namba 5 kunafanya mtu ashindwe kujiandaa hasa kwa bajeti yake angalau ungeweka makadirio ya jumla kwamba angalau ukila chakula cha kawaida kwa siku utatumia kiasi kadhaa hasa ukizingatia nyinyi ni wazoefu na mmeshapeleka watu mara nyingi,hamuwezi kushindwa hili.Hotel ni biashara kwanini wasiwape Menu zao?

2.Pia kusema Masuala ya dharura yapo kwenye sera za hoteli na camps utakazofikia bado halimsaidii mteja,ukishafika huko kwenye camps ukiwa hujajiandaa,maana yake haupo salama,kwanini usiziweke hapa hizo sera maana ninyi si mnawasiliana nao,uwazi ni muhimu sana.

Asante
 
2. ZANZIBAR PACKAGE

Hii ya nyumbani kabisa.



Gharama ya Package ni Dola 898 sawa na takribani Milioni 2 tu.

Yaliyomo:
1. Utafikia Hoteli ya Melia yenye hadhi ya nyota 5 na utalala hapo kwa siku 3 mfululizo.
2. Chakula ni bure asubuhi, mchana na usiku.
3. Siku nzima utatembezwa katika Mji wa Kale wa Stone Town pamoja na Kisiwa cha Prison Island.
4. Siku nyingine (nusu siku) utaenda kufanya utalii wa kutazama jua linavyozama kwa view nzuri.
5. Usafiri bure kurudi Airport au Bandarini

NB: Hii imeanza Januari 7 na mwisho wake ni Februari 28, 2022.

Gharama za usafiri kutoka ulipo kufika Zanzibar ni juu yako. Hii kwa watu wa maeneo jirani kama Dar na Tanga wataichangamkia sana. Au wote waliopo maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki hawatatumia gharama kubwa ya nauli.

Mawasiliano: 0757 212 122 / 0737 555 522
Karibuni.
 
Ahsante kwa majibu mazuri ila nina bado sijaridhika.

1.Kushindwa kujibu namba 5 kunafanya mtu ashindwe kujiandaa hasa kwa bajeti yake angalau ungeweka makadirio ya jumla kwamba angalau ukila chakula cha kawaida kwa siku utatumia...
1. Mdau, swali hili uliuliza directly tukakosa jibu la moja kwa moja kwa sababu machaguo ya vyakula yanatofautiana mtu na mtu. Hakuna bei moja ndio sababu tukasema vyakula na bei zake vipo kwenye menu ya hoteli husika.

2. Tulimaanisha sera zipo kuhusu dharura na kumhudumia mteja anapopata dharura ya kiafya. Hivyo sio suala la kuwa na mashaka nalo.

Unaweza kutupigia simu kwa ufafanuzi zaidi: 0757 212 122 / 0737 555 522
 
Hii itakufanya ulale chumba single??
 
Nipo Congo Brazaville nabarizi, ni short holiday ya mwanzo wa mwaka na tutafanya nyengine kabla ya July in shaa Allah.

Maisha ndio haya haya bestyyyy
 
Kumbe kwenda Turkey n cheap sana... kuliko kwenda China.. kama mna tour kwa ajili ya wafanyabiashara utustuee.. twende tukajifunze kuanzisha viwandaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…