Huu ni ugonjwa gani unaompata ndugu yangu huyu kila akisaini mkataba mpya?

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
Ndugu zangu hili jambo linanitatiza sijui niseme ni ugonjwa au ni nini.

Iko hivi, nina kaka yangu anaendesha bodaboda hizi za mikataba, sasa mara ya kwanza mwaka jana alikabidhiwa pikipiki mpya na boss wake akafanya kazi kama wiki hivi mara ghafla akaanza kuwehuka, yaani ni kama ukichaa hivi unampata hataki kula, hataki kukaa chini hadi alazimishwe, kuna siku alivua na nguo kabisa akaanza kwenda barabarani uchi, alimjeruhi baba

walivyopishana mlangoni bahati nzuri alichokuwa ameshika ilikuwa ni kijiko la sivyo tungesema mengine.

Sasa tulihangaika naye kwenye maombi huko anatulia akirudi nyumbani hali ni mbaya na kuna muda anasema asamehewe mara wamuache wasimuue, sasa anaowasema kuwa wanamfanyia hivyo eti baba na mama( mama huyu anayeishi na baba ni yule mama yangu wa kambo) nina uhakika baba yangu na mama huyu anayekaa naye hawana haya mambo ya uchawi kwanza wamroge ili iweje, ni kitu hakiwezekani.

Kuna Sheikh alikuja kumsomea dua na dawa za mitishamba kama wiki mbili ndiyo alitulia akaja akapona kabisa, akaendelea na shughuli zake, sasa hii juzi amepewa mkataba mpya na pikipiki mpya, hii hali imemuanza tena ninajiuliza ni nini kipo katikati ya hili jambo je, ni mikono ya watu au ni nini maana akienda hospitali hamna tatizo.

Naombeni wenye ujuzi kuhusu hili swala au msaada tumpeleke wapi ili hii hali isije kumrudia tena. Maana tunachanganyikiwa kabisa usipokuwa makini anaweza kumdhuru mtu au akakudhuru wewe mwenyewe hata majirani wakija kumuona hawakai kabisa wanamuogopa.
 
Akiwa sawa muulizeni kama alishirikiana na wenzake wakaiba boda ya mwenzao.
Japo ni ngumu kukubali..
Kama waliiba jamaa naseti kila akipata boda anakutana na kichapo..
Hii kweli ngumu, sasa sijui tumpeke wapi maana hata hajitambui anavyoviongea hata havieleweki
 
Ndugu zangu hili jambo linanitatiza sijui niseme ni ugonjwa au ni nini.

Iko hivi, nina kaka yangu anaendesha bodaboda hizi za mikataba, sasa mara ya kwanza mwaka jana alikabidhiwa pikipiki mpya na boss wake akafanya kazi kama wiki hivi mara ghafla akaanza kuwehuka, yaani ni kama ukichaa hivi unampata hataki kula, hataki kukaa chini hadi alazimishwe, kuna siku alivua na nguo kabisa akaanza kwenda barabarani uchi, alimjeruhi baba

walivyopishana mlangoni bahati nzuri alichokuwa ameshika ilikuwa ni kijiko la sivyo tungesema mengine.

Sasa tulihangaika naye kwenye maombi huko anatulia akirudi nyumbani hali ni mbaya na kuna muda anasema asamehewe mara wamuache wasimuue, sasa anaowasema kuwa wanamfanyia hivyo eti baba na mama( mama huyu anayeishi na baba ni yule mama yangu wa kambo) nina uhakika baba yangu na mama huyu anayekaa naye hawana haya mambo ya uchawi kwanza wamroge ili iweje, ni kitu hakiwezekani.

Kuna Sheikh alikuja kumsomea dua na dawa za mitishamba kama wiki mbili ndiyo alitulia akaja akapona kabisa, akaendelea na shughuli zake, sasa hii juzi amepewa mkataba mpya na pikipiki mpya, hii hali imemuanza tena ninajiuliza ni nini kipo katikati ya hili jambo je, ni mikono ya watu au ni nini maana akienda hospitali hamna tatizo.

Naombeni wenye ujuzi kuhusu hili swala au msaada tumpeleke wapi ili hii hali isije kumrudia tena. Maana tunachanganyikiwa kabisa usipokuwa makini anaweza kumdhuru mtu au akakudhuru wewe mwenyewe hata majirani wakija kumuona hawakai kabisa wanamuogopa.
Huo ni ugonjwa wa Akili kwa 100%. Baadhi ya wataalamu wanaita kichaa mlipuko (Schizophrenia attack episode?!)
Hakuna kulogwa wala ushirikina hapo, ni pure science.
Kwanini akipewa mkataba wa pikipiki hiyo hali inalipuka?
Jibu rahisi huenda likawa ni msongo wa mawazo (stress) katika kupambana na rejesho la pesa za tajiri. Magonjwa mengi ya akili yakiwa yametulia yanaweza kulipuka upya kwa msongo wa mawazo.

Atapata wapi msaaada?
Msaada kamili uko hospitali, aonane na madaktari wa Afya ya Akili. Huyo akizingatia dawa na jamii ikawa karibu naye anatulia fresh na mtasahau kabisa kama aliwahi kupitia hizo mbanga.
 
Asante mkuu itabidi tumpeleke kwenye maombi na huko pia
 
Back
Top Bottom