Huu ni ugonjwa gani unaompata ndugu yangu huyu kila akisaini mkataba mpya?

Hospital gani nzuri kwa huu ugonjwa?
 
Pole sana...mpelekeni polisi
 
Umepeleleza kama anatumia cannabis sativa?
 
Kwanza poleni
Pili inabidi muombe sana Allah awafanyie wepesi maana uchawi upo ila upaswi kuamini

Tatu muwe mnaswali sana aiseeh
Nne inabidi mumuamishe kabisa hiyo wilaya au Kijiji akakae mbali na unatakiwa akiwa anasaini mikataba Bora asimwambie mtu.

Inshallah Allah atawafanyia wepesi 😌
 
Hospital gani nzuri kwa huu ugonjwa?
kuna baba wa rafiki yangu ambae ana hali inayofanana na hiyo ila kwa namna nyingine,
wakati tukishauriana nae namna ya kumsaidia huyo rafiki yangu, alinidokezea kua tayari ameomba apointment na miongoni mwa wataalamu wa afya ya akili pale Kairuki hospita ili huyu ndugu aweze kupata usaidizi wa kisaikolojia kabala mambo hayajamuendea mrama zaidi.

hata muhimbili,
nadhani wapo madaktari bingwa wa changamoto hiyo anaweza kusaidika
 
Ipo hivi. .. Kila tatizo Lina mrango wake .

Biblia inasema au inafundisha kuwa kila muamgukapo na mkitaka kunyanyuka rudini nyuma mchunguze chanzo Cha anguko.

Usitafute tiba. Kaa Chini na muhusika mhakukishie usalama, upendo na kuendelea kumjali hata baada ya yeye kusema madudu aliwahi fanya na aseme ili mjue mnatibu vipi.

Bila kutibu chanzo basi hata Kaa sawa.....Labda atapata nafuu kidogo. ..
Ktk kubaini chanzo mnaweza deal na sphere mbili.

1. Kiroho
2. Kisaikolojia

Ikiwa ALIKOSEA sehem basi ujue anawindwa aidha
na nguvu nyingine (kiroho)
Au nguvu zake mwenyewe zinamsuta (kisaikolojia)

, muulizeni ikiwa yeye keshawahi jihusisha na Mambo ya waganga. Au uhalifu uwao wowote ule.

Anapoulizwa ahakikishiwe usalama na upendo hata baada ya kusema Mambo yake mabaya.

### In short ktk tiba za kiimani na au kisaikolojia TAFUTENI chanzo kabla ya dawa. .
Maombi, Dua, mazindiko na matambiko, vipindi vya ushauri nasaha (counselling wanapita) yote hayo bila kubaini chanzo kwanza hamta toboa ...

As unaomba unaombea Nini ???
Toka pepo .. pepo gani ???
SHINDWA ibilisi ibilisi yupi ???

(On mental health side)
Baada ya mahojiano akikataa basi mpelekeno hospitali .. yaweza kuwa aliwahi pata damage ya ubongo na hakutibiwa ipasavyo.

Muwaone madaktari wa mishipa ya fahamu na ubongo kiujumla .. wanamfanyia vipimo kucheck ikiwa ana damage yoyote kichwani au components/mishipa ya faham ya ubongo (neurons) hazipitishi umeme sawasawa.

Binti Sayuni03
Nimejarib kuwa deep spiritually na biologically. As ktk utafutaji msipo msaidia najua itakua ni burden kubwa kwa familia.
 
From a medical perspective this is a purely mental illness, inabidi aonane na Daktari bingwa wa magonjwa ya Akili -Psychiatrist,
madaktari hawa hutowapata kila hospitali, wapo hospitali kubwa mfano Muhimbili, Mlonganzila, Benjamin Mkapa, sio hizi hospitali ndogo ndogo, kutokana na maelezo yako ni aina ya ugonjwa ambao hauitaji hata vipimo, ni maongezi tu na Daktari sahihi, Chance kubwa hajarogwa ni ugonjwa wa afya ya akili akitumia dawa anakaa vizuri,.
ila pia kama mshaingiza na mambo ya Imani, Shekhe, Mwamposa napata wasiwasi kama ndugu kuwakonvice kwamba its purely science na sio uchawi.
in my opinion ntamaliza waganga, mashehe na wachungaji bila mafanikio. Fanyeni maamuzi mpelekeni hospitali yenye kitengo cha afya ya Akili.
 
mh!
 
Hali mnayoipitia naielewa vizuri sana,kwasababu tumewahi kuipitia. Kiufupi kwasasa mmevurugika na mpo tayari kufanya lolote lililo ndani ya uwezo wenu ili apone.nawaombea kwa MUNGU, awape hekima ya kumjua yeye,poleni sana. Binti Sayuni03
 
Hali mnayoipitia naielewa vizuri sana,kwasababu tumewahi kuipitia. Kiufupi kwasasa mmevurugika na mpo tayari kufanya lolote lililo ndani ya uwezo wenu ili apone.nawaombea kwa MUNGU, awape hekima ya kumjua yeye,poleni sana. Binti Sayuni03
Asante mkuu Mungu ni mwema tutazidi kumuombea akae sawa
 
Asante mkuu hakika ushauri wako ni mzuri na tutaufanyia kazi
 
Asante sana mkuu ngoja tuachane na haya maswala ya wataalamu wa asili tukamcheki hospitali
 
Awaone wazee he is a king 👑, he must be crowned already. Codes must be quered.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…