Huu ni ushamba, kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya

Kwani utaratibu huo umeanza leo

Ova
 
Mkuu usisahau upo Africa.
 
Wapi hawafanyi hivyo tuambie?
 
unahamisha magoli. Joe Bidden yupo ndani ya nchi huyo hakuna haja ya zulia jekundu. Hayo mengine nakuachia mwenyewe
Tusiandikie mate wino upo mwingi tu, hebu tazama hiyo clip Hangaya anapita kwenye jamvi?
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100. Na niongeze kuwa ni Ulimbukeni na kuto kupevuka Kisiasa na kimtazamo..

Huko nyuma uzi kama huu, nilisema..kuna wengine huo mpaka wanashona mashati na magauni ya vitenge na kuwaomba wananchi wajipange kwa road kuwapokea na kuwakaribisha hawa Waheshimiwa. Kwa kweli bado tuko kwa zama za Ujima.
 
Ngabu kipindi cha mwendazake ulikua unasifia kipindi cha mama unaponda kila kitu, pole sana
 
Hiyo ni mbinu ya kuongeza urefu wa kamba. na hapo bado siku atakayo rudi kamba zitakuwa ndefu zaidi. Maana utasikia Ufaransa wametoa mkopo wa milioni kadhaa, na Ubelgiji wametoa msaada wa madawati kuboresha elimu. Huku TRA wakiongeza dau la kufuli watakalo fungia vibanda vyetu.
 
Ila sisi Watanzania tumekuwa mapumbavu sana! Ina maana wakati wa mwendazake ilikuwa sawa ila kwa huyu mama ni ushamba? Tuache umazwazwa!
 
ni mawazo yako haukatazwi kutoa vile akili yako inavyofikiri,ila kaa ukijua protokali lazima izingatiwe...hata kupiga saluti nako kunaweza kuwa ni kupoteza muda,hata magwaride yanayochezwa katika ocassions mbalimbali inaweza kuwa ni kupoteza muda(kwa mujibu wa fikra zako) lakini pia hata kusalimiana nako kunaweza kuwa ni kupoteza muda kwani yanaweza kuachwa yote hayo na mambo yakaenda tu vizuri,hivyo ndivyo uzuri wa uhuru wa kufikiri na kutoa maoni ulivyo..we call it democracy,aise its enough
 
Ila sisi Watanzania tumekuwa mapumbavu sana! Ina maana wakati wa mwendazake ilikuwa sawa ila kwa huyu mama ni ushamba? Tuache umazwazwa!
Mtoa maada alikua anaimba mapambio kipindi kile, muda huu kila kitu kwake ni kibaya,
Binadamu ndivyo tulivyo
 
Infact haina tija...

Kwa sababu hapo sana sana huagwa tu kwa maneno ya kawaida "Safiri salama, ufike salama, safari njema n.k"...

Nyani Ngabu kuna wakati niliweka comment hapa kwenye uzi wako mmoja hivi, kuwa hizi tawala za Kiafrika kwa kiasi kikubwa zimerithi zile taratibu za kiuongozi za kichifu, na ndio maana nchi zetu utaona Rais hapingwi, analambwa miguu, neno lake ni sheria n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…