Huu ni utoto au utaahira?

Huu ni utoto au utaahira?

Ni hivi yalimtokea shost, boyfriend anakwenda kwake, lakini hamfahamishi nyumbani. Mpaka wamepata mtoto, mama mkwe amekuja kumwona mtoto, ubatizo wa mtoto umefanyika kwa shost mama amekuja kama mgeni. Sasa siku moja shost anakwenda Kariakoo shopping, anakutana na jamaa yuko na mother, khe, baada ya salamu aliuliza mnakwenda wapi, mama alijibu kupanda basi twende nyumbani, mama alikuwa na mzigo, shost aliofer lift, jamaa alitaka kutoa nje, mama aliona unafuu ule alikubali.

Wamefika home, masikini mama anaishi kwenye nyumba ya nyuma mbele ameweka msingi tu na ni wa muda mrefu. shost aligundua kwanini jamaa alikuwa hataki afike home. Sasa kama mtu umesha zaa nae, haya si ni mambo ya kawaida tu. Hakuna aliyeumbiwa umasikini.
Hujakoma tu kuleta habari za ma shosti zako humu??? Si ulisema ulisutwa??

We naona mpaka wakukate viganja
 
Umepata mapenzi kwa kuwa umejiwekea ka status mjini unaona aibu kumpeleka kwenu kutokana na hali halisi . Hii ni kukosa confidence ya maisha, utoto au ni utaahira?


Kosa la Kwanza Lipo kwa Kumpa Mapenzi kisa tu ana status Mjini.. Kwa hiyo Dhamira mliyojijengea ndio ilimpa hofu kukupeleka kwao. Yeye ni Fake na kwa Ufake wake ukakubali kumvulia Nguo Mpaka kumzalia Mtoto sasa kuja kukwambia ukweli kuwa yeye kwao ni choka mbaya tayari ungemtosa hasa ukizingatia mazingira aliyokupatia.

Muache kuachagua Pia Pole yako lakini
 
Hujakoma tu kuleta habari za ma shosti zako humu??? Si ulisema ulisutwa??

We naona mpaka wakukate viganja


Siyo tu kuleta story za Mashost hizi ni Story zake ila anazivika uhusika wa Mtu Mwingine- Impersonation- Ukiangalia katika ya kila hiyo story ya Shost huwa anajiweka uhusika ila anadhani watu hawajui huwa wanapotezea tu ili maisha yasonge Mbele hakuna kitu wa Dada hawapendi kama kuwa challenged au kuonekana wamekuwa offended.

Na Kuna siku alikuja kuaga kuwa hatakuwa tena Mwanachama wa JF lakini anaonekana bado yupo tu.. in Makongoro Voice.

Yaani JF kuna Fake Nyingi san Duuu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hata girls mna matatizo, unakua na mtu hadi mimba na mtoto umezaa hufahamu hata kwa mzazi mwenzako! Labda km unaiba ume wa mtu
 
Back
Top Bottom