Huu uchawi nilikuwa siujui hadi siku ya jumapili iliyopita

Hapana Mtumishi kasome maandiko utajua kuwa sio uchawi
Mnasikitisha sana watu mnaojiita Wakristo.

Chochote walichofanya manabii na Yesu vilikuwa ni mafunuo ya Roho mtakatifu tena mara moja tu.

Unapoviamini hivyo na kurudia kuvitenda inageuka ni ibada ya sanamu.
1. Wanachofanya mitume na manabii wenu fake kuuza chumvi, ufongo, fruto, maji, sabuni nk hii ni ibada ya sanamu...regardless vinaponya au laah.

2. Tunachopaswa kufanya ni kumuomba Mungu juu ya shida, mahitaji hata majaribu...Mungu ana miujiza mipya kila siku.

3. Nabii alifanya muujiza wa kujaza mafuta kwa vyombo vya mjane mara moja

4. Nabii aliponya maji kwa chumvi mara moja tuu

5. Yesu aliponya kwa kumpaka matope kipofu mara moja tu.

Someni maandiko mnapotosha kweli ya Mungu.

Note: chumvi pekee ingezuia wachawi dunia nzima wachawo wasingeloga tena...je watu hawajawahi sikia hili?
 
Hii kitu nahisi naifahamu na ulifanya kitu bora zaidi kukaa kimya na kutokujibizana unajua katika ulimwengu wa kiroho sana sana kwenye maswala ya kichawi ili mchawi akuroge au dawa zake zifanye kazi lazma kwanza akubadilishe Aura yako au kwa lugha nyepezi Energy zako..

Na ndo maana hata kwa wale wasioamini uchawi ili waweze kurogwa kwanza lazma wapigwe matukio ya mauza uza ili akiona hivyo aanze kupata hofu ile hofu ndo negative energy ambayo itatumika kama mtaji kwa wachawi..ila kama akipata mauza uza na hakupata hofu basi wachawi watamuogopa

Kingine ni hasira hasira huchochea Negative energy kuliko chochote na huvuta nguvu za giza kuliko Energy yoyote ile yoyote mwenye kucontrol hasira bhasi huyo kapona katika ulimwengu wa kiroho...

Ukiwa na hasira Energy za nuru huondoka na Huja negative energy kubwa sana hii huwa nyepesi saja kupenyezewa nguvu zozote za kichwi au za uovu na ndo maana unaweza ukaua ukiwa na hasira au kufanya lolote halafu baadaye ukashangaa umewezaje kufanya hivyo ni wakati ambapo mwili wako wanaweza kufanya watakavyo wabaya wako...

Hongera sana Endelea kuamini unachoamini maana kinakupa ushauri mwema kuhusu Kubalance Nguvu na energy ulimwengu wa kiroho ili usikuletee madhara
 
Ulitumia sura ya Al Jinn kuomba dua?
 
Napokea sadaka kwa watakaovutiwa na tangazo hili

Namba ya kutuma ni ya Lucas mwashambwa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Wewe sio mshauri wa kiroho ni mjasiliamali wa kiroho maana unapewa na sadaka.
 
Basi ndo huu uchawi niliopigwa , nateseka mpaka leo kiaina. Yaani ikitokea ugomvi na mimi nikakasirika.
Mbaya sana hio,, siku hizi mjini usi react ovyo hasa kuruhusu hasira zako waziwazi watu wanapenyesha mambo humo,,,,, mimi ilinitokeaga kitu kila nikisikia azana hasira zinapanda nakua kama mmasai anapandisha mori
 
Mkuu haya ndio tunataka.
Kuna watu wanafukiri sifa kupigana kila vita. Kumbe vingine ni mitego ili ujae watu wapitishe hujuma zao kwako.
 
Mbaya sana hio,, siku hizi mjini usi react ovyo hasa kuruhusu hasira zako waziwazi watu wanapenyesha mambo humo,,,,, mimi ilinitokeaga kitu kila nikisikia azana hasira zinapanda nakua kama mmasai anapandisha mori
Pole sana. Mimi azana zote huwa zinanikuta nimeshaomba. Hasa ile ya asubuhi. Huwa siruhusu initangulie kwa mujibu wa mafunuo yangu ya rohoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…