Huu ugonjwa wa Gastritis sasa unanitesa mno

Huu ugonjwa wa Gastritis sasa unanitesa mno

Reply yako imenipa faraja sana mpaka nimehisi kupona, nime furahi sana kama kwa sasa hauna hii shida kabisa, nita tafuta huo unga muu, matumizi yake yapoje yaani kiasi gani ca kijiko, mara ngapi kwa siku ,a kwenye kikombe kiasi gani, maana kwa sasa nina tumia unga wa kokwa la parachichi asubuhi mchana na jioni kwenye kikombe kimoja cha chai ile dawa ya hospital nime acha kwa siku 5 mfululizo mpaka sasa ila sasa maumivu ndiyo balaaa kuchoka, ganzi, kichefuchefu ila nikirudi kwenye ile dawa ya hospital antacid inaitwa pantonex kidonge kimoja kwa siku ile asubuhi baada ya siku 3 au 4 napata nafuu, ila sasa ndiyo nakuwa mlemavu wa hizo dawa na siponi after miezi 2 au mwezi 1 nikianza kula vyakula vingine shida ina rudi so nakuwa najua mh hapa bado sijapona ila ni nafuu tuu nilikuwa nime pata. Sasa nauliza naweza kunywa huo mlonge huku natumia hizi dawa za antiacid maana nataka kuanzia kesho asubuhi nianze tena kumeza hizi antiacid huku nakunywa huu unga wa tangawizi maana nasikia wengi wanasema ume wasaidia pia, ila nataka kuanza kutumia huo mlonge kama wewe ume kusaidia na mimi nina imani nitapona nitoke kwenye hii shida jamani maana unateseka kuliko kawaida.
Nenda duka la dawa za kisunna nunua Habbat Soda ya unga nusu kilo, asali Lita moja. Chukua kijiko kimoja cha Unga wa Habbatsoda weka kwenye kikombe cha chai, changanya na asali vijiko vikubwa viwili vya chakula. Vuruga ichanganyike vema kabisa halafu lamba yote.

Fanya hivyo asubuhi, mchana na jioni kwa siku au miezi kadhaa Inshallah utapona!
 
Panda nyumbani kwako,huu mti ndani ya miezi mitatu unakuwa tayari kwa kuvunwa usitegemee vya Jirani,so wakti unavuna huo wa Jirani chukua mbegu upande na wewe
Jamaa anaulizia jinsi ya kuandaa huo unga zaidi ya mara 3 haumjibu we umekomaa tu panda mti nyumbani kwako, kama yupo kwenye upangaji apande wapi..

Jibu swali lake la namna ya kuuandaa ili umuepushe na gharama za kununua
 
Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.

Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.

Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.

Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
View attachment 2862416
Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.

Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.

Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.
Pole sana Mkuu Mimi pia nliwahi sumbuliwa na tatizo hilo niliponea kwenye maombi kupitia hili Andiko"Kila alitajaye jina la Bwana ataokoka" ilikua kwenye crusade nkapona mpaka Leo Niko fresh
 
Pole sana Mkuu Mimi pia nliwahi sumbuliwa na tatizo hilo niliponea kwenye maombi kupitia hili Andiko"Kila alitajaye jina la Bwana ataokoka" ilikua kwenye crusade nkapona mpaka Leo Niko fresh
uliwahi kwenda hospital kujua labda shida ilikuwa nini au ulienda moja kwa moja kwenye maombi tuu ?!
 
Nenda duka la dawa za kisunna nunua Habbat Soda ya unga nusu kilo, asali Lita moja. Chukua kijiko kimoja cha Unga wa Habbatsoda weka kwenye kikombe cha chai, changanya na asali vijiko vikubwa viwili vya chakula. Vuruga ichanganyike vema kabisa halafu lamba yote.

Fanya hivyo asubuhi, mchana na jioni kwa siku au miezi kadhaa Inshallah utapona!
Asante sana kwa mchango wako, nita ufanyia kazi mkuu
 
Nashukuru na nimefarjika sana kwa kuwa muwazi na mkweli kwa nafsi yako. Hii imekuwa ni sehemu/hatua kubwa ya tiba yako, kwani unaposema kwa mtaalamu wa afya kuwa nimetimiza ulichoniambia kwa asilimia 100, swali kwake huwa:
1: hapa shida ni nini?
2: tatizo silo
3: dawa siyo
4: matumizi siyo
5: mwenendo siyo?

A: Ninachokiona ni kutokuzingatia mwenendo wa kimaisha hasa ulaji wako kama sehemu ya maelezo yako. Naamini bado inawezekana yapo mengine unafanya bila kujua.

B: Kutokufatilia kwa daktari wako unapoona mambo hayaendi ilivyotarajiwa ili kufanya marekebisho.

C: Kutokufanya ufatiliaji kwa mtoa huduma pale ambapo unapata dalili mpya dhidi ya zile za zamani.

D: Kwa tiba yoyote utakayoamua kufuata hili ni jukumu binafsi, ila ni vyema kuzingatia tiba mwambata (mwenendo mzima wa kimaisha), ili mwili uweze kupata muda wa kurekebisha palipojeruhiwa.

E: Ni kweli kwamba matumizi ya Relcer gel na jamii yake haitakiwi kuwa ya mwendelezo kama ilivyo kwa vidonge ulivyopewa kwa sababu mbalimbali.

F: Kuna haja pia ya kuonana na mtaalamu wa afya ili kuangalia mwenendo mzima wa maisha yako(upande wa mlo, ili kujua zaidi mambo mengine unayoyanya na ni kinyume na hali uliyonayo), lengo ni uweze kusaidika zaidi bila kujali ni njia ipi ya tiba utaamua kuitumia katika tiba. Kwani bado ni muhimu kuzingatia haya ili kupata uponyaji mzuri.

Nakutakia tiba njema.
Asante sana mkuu, nitafanyia kazi muongozo uliyonipA. Ubarikiwe mnooo
 
Loweka karafu kiasi kwenye maji kwa siku mbili then kunywa hayo maji kikombe kimoja asubuhi na jioni
 
Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.

Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.

Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.

Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
View attachment 2862416
Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.

Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.

Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.
Niliugua huu ugonjwa wa takriban miaka 20,nikatumia dawa mpk nikajihisi mwili unanuka dawa,nilikuwa nachagua kipi nile na kipi nisile,lakini Yesu wangu ndiye alieniponya,vile vyote nilivyokuwa naogopa kula ninakula na sina shida kabisa,mtafute Yesu mkuu anaponya...
 
Niliugua kwa takribaban miaka 20,nikatumia dawa mpk nikajihisi mwili unanuka dawa,nilikuwa nachagua kipi nile na kipi nisile,lakini Yesu wangu ndiye alieniponya,vile vyote nikivyokuwa naogopa kula ninakula na sina shida kabisa,mtafute Yesu mkuu anaponya...
Ulienda kwenye Maombi tuu ukapona, ila ugonjwa ulipima kwanza ukajua shida hasa ilikuwa nini ?!
 
Back
Top Bottom