Mkuu pole sana,mimi huo ugonjwa kwa mwaka 2016-2020 umenitembeza sana hospital,ndanda hospital,(mtwara) baada ya kupewa referral kutoka Liwale-Lindi,ndanda walishindwa, ni kaandikiwa kwenda Mhimbili huko nilibainika kuwa na ugonjwa /tatizo kama lako,nilipewa dawa nyingi sana,zingine zilitaka kuniua.
Tatizo halikusha,ikabindi niende aghakani hospital,wapi,nikaenda hindu mandal-Mwanza wapi,nikaenda bugando hospital nikakutana na Doctor majimbe, niseme huyu ndo alikuwa chanzo cha mimi kupata nafuu,alinishauri kuhusu lishe,kula kwa wakati, sikupewa dawa nyingi sana ,pia alinikataza kunywa soda,kula maharage,maziwa,ndizi kwa namna zake,sukari nyingi kupita kiasi,pia kutoruhu hasira na huzuni ndani ya moyo wangu.
Baadae tatizo lilirudi tena,nikakutana na mtu akanishauri nitumie mlonge,ikumbukwe kwa wakati huo,nilizuiliwa kunywa soda, ndizi hapana,mboga iliyoungwa kwa viungo vingi hasa nyanya hapana,maharage, dagaa ,chakula kilicho lala nk.baada ya kutumia mlonge wa kununua kwa mwezi mzima nikianza kupata nafuu,nikaamua kuupanda huu mti nyumbani kwangu,nikaendeleza doazi kwa miezi miwili mfululizo ,hiyo ilikuwa kwaka 2021.
Baada ya hapo nikaanza kula maharage,maziwa nakunywa soda,dagaa nakula bila shida nk.
Ushauri wangu ni kuwa utashauriwa kuuziwa madawa mengi sana ya kienyeji lakini ni bure maana yanaweza kukuletea shida nyingine,hivyo mmea ambao madhara yake hayajathibitishwa kisayansi,kwani hata hao wanasansi wana usifu hadi sasa ni mlonge ,utumie huu mmea uone ,naimani utapona kabisa.
Mimi sasa nakula kila kitu ambapo hapo awali nilizuiliwa