cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Siyo tumbo pekee.
Hata jino tu likichachamaa huwezi kupelekea moto
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Siyo tumbo pekee.
Hata jino tu likichachamaa huwezi kupelekea moto
Ushauri umenyoooka,1. Kuanzia leo anza kutengeneza maji ya bamia yaani unachukua bamia zile unakatata unazitia ndani ya jagi lenye maji kuanzia lita mbili au tatu unaweka kwenye friji kama umeziloweka hivi.
Asubuhi ukiamka unakunywa glass moja kwenye tumbo kavu. Kunywa taratibu kidogo kidogo sana ili usipatwe kichefu chefu. Then mengine unywe mchana kabla ya kula chakula kwenye tumbo kavu lile la njaa.
Na kila muda ukisikia hayo maumivu makali kunywa hayo maji ya bamia utakayotengeza kila wakati. Hakikisha unakunywa zaidi kwenye tumbo kavu.
Bamia itakusaidia kuirepair kuta za tumbo au utumbo ambazo zimeathiriwa na acid tumboni na kusaidia kuvipa vidonda layers repair.
2. Kula matikiti maji especially kabla ya chakula. Ule kwa kadiria ya uwezo wako. Tikiti maji lina maajabu ya kuwa na maji mengi ambayo kwa components zake yatapenya hadi nandi kabisa ya tissues zako mbali mbali mwilini na kuupa mwili supply ya maji haraka kuliko ukiyanywa haya ya kawaida. Maji ya tikiti yatakusaidia ku neutralize acid na kuipunguza nguvu katika level ya damu na hivyo kuanza taratibu kuzima makali yake huku ikiitokomeza.
Kula matikiti maji na juice yake kadiri unavyoweza usikatie tamaa fululiza hata miezi ukiyala utapata nafuu yako.
3. Achana na chai ya rangi, juice au vinywaji vya kiwandani especially soda hizi kama Pepsi, coca-cola, sijui mo energy bia zote unazozijua yaani kinywaji chochote cha kiwandani achana na nacho usiguse ndio sumu. Maji haya ya kununua ya chupa si salama kwako. Tumia sana maji ya nyumbani ya kuchemsha au kata kiu na tikiti maji au tikiti lenyewe kama nilivyokuelekeza pale juu.
4. Ukipikiwa au kupika mboga yoyote itakayotiwa nyanya then hakikisha mpishi au wewe mwenyewe unaweka kitunguu swaumu kingi sana sababu kitunguu swaumu kinakata acid ya nyanya na kuifanya less effective mwilini.
5. Achana na hizo dawa za anti acid huwa ukiacha zinasababisha acid inarudi kwa kasi sana mwilini so achana nazo na zingatia chakula sana.
6. Mboga za majani kama mchicha, spinach, na mboga mboga zinginezo ziwe sehemu kubwa ya lishe yako kwa kifupi anza kuwa vegetarian kuanzia sasa.
Ukifanya hivi kwa muda wa mwaka, ukiendelea kuumwa nitafute tupigane.
Mkuu mambo vipi, una endeleaje na hali kuhusu ugonjwa wa Gastritis ?!Habari wadau, naomba mwenye kujua ugonjwa wa gastritis aniambie alipataje tiba akapona kabisa.
Nita anza tiba mbadala maana sikuwahi tumia tiba mbadala kabisaa zaidi ya dawa za ospital tuu. Nitakuja rudisha mrejesho hapa.
Naendelea poa, ni suala la Management of the disease tuu.Mkuu KUKU_UFUGAJI , tunaomba mrejesho, vipi hali yako ya tumbo? Ulipona?
Dawa zote walizokushauri hakuna iliyofanya kazi?Naendelea poa, ni suala la Management of the disease tuu.
Anza kula ugali wa mhogo badalanya dona na sembe,acha au ounguza kula wali,kula Milo miwili au mmoja kwa siku! Wanga wa kutumia uwe viazi vitamu,magimbi na mihogo ichemshwe iskaangwe. Matatizo karibu yote ya tumbo husababishwa na mtindo mbaya wa chakula.Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.
Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.
Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.
Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
View attachment 2862416
Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.
Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.
Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.
Dawa zote walizokushauri hakuna iliyofanya kazi? Disease management ndiyo kila kitu naona