Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Hilo chukua mwenyewe GOOGLE utakuta tu. Angalia hata USA wala hawamiliki American Airways au UK hawamiliki British Air kama majority shareholders.
Umekosa mapema swali nililokuuliza, biashara ni airways tu? Ww umesema serikali haitakiwi kufanya biashara, maswali yalilenga kujua hilo la serikali haitakiwi kufanya biashara umetoa wapi? Na wapi huko nchi zilizoendelea serikali haifanyi biashara? Umekuja na airways, Kwan biashara no airways tu?
 
Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.

Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?

1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?

2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?

3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?

Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.

Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafsi.
Ni uwekezaji kama mwingine labda ni mgeni Kwa Tanzania.

Tanzania sio Nchi ya kwanza kufanya huo uwekezaji ila nyie ni ulimbukeni wako ndio unakusumbueni.

Mwisho kwani baada ya wawekezaji kupewa uendeshaji hela Kwa Serikali imepungua au imeongezeka? Ukijibuu hapo ndio Utajua ni uwekezaji au hapana.
 
Kabla ya uwekezaji pesa ilikua inapungua au inaongezeka? kwa records za bandari toka mama aingie makusanyo yameongezeka maradufu
 
Bams tuombe uzima tu Mungu atuweke hata japo tufike 2030 then tuje turudi kwenye page hii. Naamini hutapenda kusoma maandiko yako haya.

Privatisation ndiyo engine ya growth, Serikali haziwezi kufanya biashara
Privatization na uporaji ni vitu viwili tofauti kabisa. Tanzania siyo nchi ya kwanza kufanya privatization. Tazama hata mkataba wa DP World Southampton, kama utaona ni kipuuzi kama huu wa kwetu.
 
Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.

Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?

1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?

2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?

3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?

Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.

Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafsi.
Kukataaa ule ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo yalikuwa makosa makubwa mno ya kimkakati
 
Do you think Serikali ingeweza ku transform teknolojia ya TBL ? Kwa taarifa yako TBL ilikuwa mali ya East African Breweries (Wanao manage Kenya Breweries siku hizi wanaitwa Diageo). Nyerere alipotaifisha akakiweka chini ya NDC, halafu baadaye wakabadili sheria ikawa Kampuni inayojitegemea. Toka ibinafsishwe mwaka 1967, niliona ni mwaka 1990 ndipo walibadili packaging line.

Bureaucracy ya serikali kwenye decision making, procurement regulations na compliance kwenye financial management zinacheleweaha sana mashirika au viwanda ku cope na technology
Serikali ingeweza au isingeweza hilo sifahamu. Nimekujibu uliposema mashirika mengine yaliyobinafsishwa yalikufa sababu ya kutoendana na teknolojia mpya. Hapo ndio nikahliza huyo mwekezaji kama ameshindwa kuendana na teknolojia mpya tafsiri yake uwekezaji huo haukua na maana na umefeli. Maswali yakaja kwako ni mashirika mangapi yalifanikkwa kufanya vizuri na mangapi yalianguka ili tuweze kupima kama tulifanikiwa kwenye ubinafsishaji
 
Wewe inaonekana ni zero katika masuala ya mikataba.

Mimi nimeshiriki kuandaa mikataba mingi ya kibiashara ya kimataifa. Ninaelewa ninachokiongea.

Sina shaka nabishana na layman, asiyejua chochote. IGA ile ya kishenzi iliyoiingiza DPW, siyo ya kutafuta. Iliwekwa public, na ilichambuliwa kitaalam na Tanganyika Law Society. Na mahakama ikakiri IGA ipo kinyume na sheria za nchi na za kimataifa, lakini ikasema haiwezi kutengua maamuzi ya mhimili wa Bunge. Halafu wewe usiyetambua wala kujielewa, umebakia na uchawa utakaoumiza vizazi vijavyo.
Mbwembwe humu ndani kila mtu anazo na huo ushamba wa kujitapa kwamba ni mtu wa maana kila mtu pia anap humu tunatumia ID zenye majina ya kubuni hakuna anayemjua mwenzake hivyo kila mtu anakuja na uongo wake.

Hakuna namna yoyote ile IGA ya DPW ikaingilia uwekezaji mwingine wowote unaofanyika hapo TPA, hakuna namna IGA iliyosainiwa kwa ajili ya biashara za magati namba 3-7 ikazuia biashara nyingine ya bandari katika eneo lolote iwe ni bandari ya kule Mtwara iwe ni ile ya Bagamoyo au iwe ni ya kule Tanga.

Mnachosahau ni kuwa kipengele kimoja au viwili haviwezi kusomeka kwa ujumla eti vikiwa ndio kila kitu kwenye mkataba wa biashara,. Ukisoma mkataba usome kwa ujumla usidanganye watu kwa kuegemea kwenye kifungu kimoja au viwili.

Naona unapoteza muda kuongelea DPW nakukumbusha bandari bado haijamaliza katika suala zima la ubia na waendeshaji wengine na hakuna dhambi yoyote kuwa na waendeshaji kutoka kona yoyote ya dunia.

Pale Uwanja wa ndege kuna kampuni inaitwa DAHACO ipo kuanzia mwaka 1995 mpaka leo, kuna kitu gani cha ajabu kimetokea kwa wao kuwepo mahali pale?.

Utaendelea kuwapata wajinga wajinga tu.
 
Ni uwekezaji kama mwingine labda ni mgeni Kwa Tanzania.

Tanzania sio Nchi ya kwanza kufanya huo uwekezaji ila nyie ni ulimbukeni wako ndio unakusumbueni.

Mwisho kwani baada ya wawekezaji kupewa uendeshaji hela Kwa Serikali imepungua au imeongezeka? Ukijibuu hapo ndio Utajua ni uwekezaji au hapana.
Hawezi kuongelea ongezeko la pesa nia yake ni kukosoa mradi kwa hoja kwamba mali za Tanzania zinaibiwa!. Anataka tuendelee na umaskini wetu tukiwa na mali nyingi zisizotusaidia chochote.
 
Kwa nini?
10billion usd investment na ilikuwa largest maritime project in Africa second largest maritime project in the world by thata time na pia ingekuwa largest port in africa na multiplier effects kwa uchumi ingekuwa kubwa mno tungekuwa tunashindana na akina port dubai ila tukauwa mradi wa kimkakati.
 
Uzembe, wizi, ufisadi, huko bandarini, kama ilivyo kwenye Serikali nzima na taasisi zake, hakuna anayepinga wala kukataa. Lakini tusitafute suluhisho linalotupeleka kwenye matatizo makubwa zaidi kupitia ufisadi mkubwa unaofanywa na watawala wetu kupitia mikataba.

Kama dhamira ni njema, kwa nini tusiingie kwenye JV kwa kupitia mkataba mzuri bila ya kupoteza sovereignity yetu? Kama hatuna watu wenye akili na uwezo huko Serikalini kwenye masuala ya mikataba kwa nini hata tusi-copy na ku-paste e.g.mkataba wa Uingereza na DPW? Kwa nini tunaruka majivu na kukanyaga moto?

Uchafu uliopo bandarini na taasisi nyingine za Serikali ni picha halisi ya Serikali nzima ilivyo. Je, tuwape DPW waendeshe na serikali yetu kwa sababu imejaa mafisadi, majizi, wala rushwa, wazembe na walaghai? Polisi na mahakama, kupitia reports za kila mwaka, ni taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Je tuwape DPW wasimamie polisi na mahakama zetu?

Kushamiri kwa rushwa, wizi, uzembe na ufisadi ndani ya Serikali na taasisi zake, kama bandari, ndiyo ushahidi halisia kuwa Serikali imefeli kabisa, kwa sababu hizo taasisi zote, msimamizi mkuu ni Serikali. Na inafeli kwa sababu na yenyewe ni sehemu ya huo uchafu.
Pale airport DAHACO wapo miaka 30 sasa, kwanini tusiwaondoe tukaendesha sisi wenyewe?. Acheni hulka ya kipuuzi ya kuwajaza watanzania hizi akili zenye kujaa uoga.

Kwanini tusingetumia huo mfumo wa JV hapo uwanja wa ndege na pale ni eneo nyeti la kitaifa?. Acheni pia kuwajaza wasiwasi wananchi kwa hoja zenu hizi.

Bandari ilihitaji uwekezaji kwani mzigo unaopakiwa na kushushiwa ni mwingi na unazidi kuongezeka, pia inao uhitaji wa wafanyakazi kukuzwa kitaaluma.

Yaangalie hayo masuala kwa undani kabla ya kuja na hoja negative za kwamba eti tunaibiwa au tunapoteza uhuru wetu, hizo ni fikra za kijamaa hazina tena nafasi kwenye uchumi shindani wa shoroba tunaokabiliana nao hivi sasa.
 
Hujajibu swali langu, umeadvocate bandari kupewa mwekezaji sababu mtanzania akipewa hata stand tu ya kukusanya sh 200 anaiba. Lakini hao unaosema wanaweza na wapewe bandari like wanachokipata huko wanapeleka kwa hao hao watanzania ambao ww huwaamini, hapo unakua umefanya nini? Ndio maana nikakuuliza huwaamini watanzania kwenye bandari Ila unawaamini watanzania kwenye TRA na BOT?
Kama huko napo huwaamini basi hata huo uwekezaji unaoutaka hauna maana na hautaleta matokeo yoyote

Au lengo la kuwekeza ni nini? Kama ili tupate faida, hiyo hiyo faida inarudi kukusanywa na kupangiwa matumizi na huyo huyo mtanzania ambae bado ataiba na kufuja vilevile
Ni sawa unachosema
Kumbuka enzi za Magu walikamata mpaka watu wamechepusha mafuta mpka kwenye nyumba binafsi na malori yanabeba mafuta hapo

Kwa mfano wewe ni muwekezaji na umepewa sehemu lazima utaziba mianya yote ya wizi ingawa unawalipa TRA na kwenda BOT
Kweli ni yale yale ila utakuwa umeziba moja na hao wengine kwa sababu huwezi kubinafsisha basi watafute the finest wa kuzilinda hizo hela

Kila sehemu ni uozo, najua hata zinapokwendwa zinapigwa
Ina maana tutalalama hivi mpaka kiyama?
Hoja yako nimeielewa
 
Umekosa mapema swali nililokuuliza, biashara ni airways tu? Ww umesema serikali haitakiwi kufanya biashara, maswali yalilenga kujua hilo la serikali haitakiwi kufanya biashara umetoa wapi? Na wapi huko nchi zilizoendelea serikali haifanyi biashara? Umekuja na airways, Kwan biashara no airways tu?
Nimetoa mfano tu kuwa unaweza kutumia mfano kama huo wa mashirika haya makubwa ambayo ni national flag carriers lakini majority shareholding iko kwa kampuni binafsi
 
Wewe inaonekana ni zero katika masuala ya mikataba.

Mimi nimeshiriki kuandaa mikataba mingi ya kibiashara ya kimataifa. Ninaelewa ninachokiongea.

Sina shaka nabishana na layman, asiyejua chochote. IGA ile ya kishenzi iliyoiingiza DPW, siyo ya kutafuta. Iliwekwa public, na ilichambuliwa kitaalam na Tanganyika Law Society. Na mahakama ikakiri IGA ipo kinyume na sheria za nchi na za kimataifa, lakini ikasema haiwezi kutengua maamuzi ya mhimili wa Bunge. Halafu wewe usiyetambua wala kujielewa, umebakia na uchawa utakaoumiza vizazi vijavyo.
Tujipe muda hadi 2030 tuone kama kweli hawa DP WORLD unaowaponda ni matapeli. Namba hazitadanganya na maybe tutakuwa na serikali mpya.
 
Privatization na uporaji ni vitu viwili tofauti kabisa. Tanzania siyo nchi ya kwanza kufanya privatization. Tazama hata mkataba wa DP World Southampton, kama utaona ni kipuuzi kama huu wa kwetu.
Ni kitu gani kimeporwa? Mbona uko na negative obsession? Angalia usijepata hypertension bure kwa kukariri hoja za akina Mwabukusi
 
10billion usd investment na ilikuwa largest maritime project in Africa second largest maritime project in the world by thata time na pia ingekuwa largest port in africa na multiplier effects kwa uchumi ingekuwa kubwa mno tungekuwa tunashindana na akina port dubai ila tukauwa mradi wa kimkakati.
Invekua ni largest port in Africa? Kwa maana gani? Wingi wa mizigo? Revenues?
Ingekua second largest maritime project in the world? Hizi ni exaggeration
Narudi kwenye suala lako, uwekezaji wowote si maneno bali ni terms. Terms za huu uwekezaji ulikua na yote hayo uliyosema? Maneno ya uzuri wa uwekezaji huwa mwanzoni, huko mbeleni mambo huwa tofauti, unakumbuka kwenye uwekezaji wa gas mtwara enzi za JK? Miaka imepita zaidi ya 10, tumepata kile tulitegemea?

Magufuli alikataa terms za huu uwekezaji wa bandari bagamoyo huenda alikosea hatujui sababu hatukuziona

Alipoingia mama samia, mama samia anapenda uwekezaji serikali ikafufua mazungumzo tena lakini bado ikawa ngumu, unahisi kwa nn tena serikali ya mama samia ilishindwa kuendelea na mazungumzo ya huu mradi? Nae hakuutaka tu, au terms nae zilimshinda?
 
Mkuu wala sifurahii haya
Angalia kila leo wanaandika kufuru wanayofanya TRA baadhi yao wamekamatwa na b za kutosha

Wakichunguzwa wote na kufungwa naona hela nyingi zingepatikana
Ipo siku huenda tukajielewa na kusimamia kila kikituHutu
Huyu hapa kwenye gazeti la last week
Screenshot_20240718_143640_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom