Huu ushaidi unaonyesha kabisa baba Diamond hakustahili haya na huenda mama ndio akawa mbaya

Kuna siku utakua na ukweli utaujua kwanini baba yako nikutupe wakati wewe ni damu yangu mwenyewe .Huu mstali Banana aliimba sana kwa sababu mara nyingi tunapoachana wakina mama hukimbilia kuondoka na watoto na hapo ndio Sumu huanza kulishwa mtoto hivyo inawezekana Sumu ya maneno aliyolishwa diamond na mama yake kwa baba bado hajakaa akatambua ukweli uko vipi mana tabia ya mama au baba hujionyesha tu ila kwa mambo ya Mama dangote kama anavyojiita nina wasiwasi tangu zamani alikuwa mapepe sana.Neno la mwisho kwa wanaume wenzangu ogopa sana ogopa sana mwanamke anayevaa pete aina ya feyluz au hakik mwogope sana mwangalie mama daimond pete anayovaa kidole kinachofata baada ya dole gumba
 
ndo mana machoko hawaishi mjini.
 
Ushahidi wako uko wapi sasa?
Mbona hakuna ushahidi wowote uliouweka zaidi ya malalamiko na matamanio yako tu!
 
Wanawake wachache uliowajua hawewezi kuwa uwakilishi halusi wa mamilioni ya wanawake katika nchi hii.
Haiwezekani mkamuhukumu mama yake Diamond mkiwa hamjui shida ya Diamond na baba yake ni ipi.
Mpaka sasa hakuna mtu anayeweza kuelezea hasa chanzo cha mgogoro wa huyo baba na familia yake.
Na pia mtoto kuhudumia wazazi wake ni hisani tu,hakuna sheria au ulazima wowote wa yeye kulea wazazi wake.Wazazi kuhudumia watoto ndio lazima na wajibu wao.Ingekuwa hoja ya maana kama Diamond angekuwa anamkashifu, anamtukana au anamuharibia maisha baba yake vingenivyo ni watu kutaka kujipa tu umuhimu katika maisha ya wengine.
 
Kwanza Uislamu halisi haukubali muziki anaoimba Diamond, ni haramu.
Diamond kama muislam halisi hakupaswa kumsikiliza mama yake pekee pia ilikuwa ni vyema pesa zake zingetumika katika kuwaunganisha tena upya baba na mama yake
 
Huyo mzee kawalea tu kina mondi baada ya tukio fulani kutokea, so akasimama kama mlezi kwa makubaliano na mama mondi ila sio baba yao halisi.
Aseee kwahiyo mama wa Queen na wa Diamond hawakuona mwanaume mwingine wa kuwalelea watoto wao wakampelekea huyu mzee abdul kwa makubaliano? TUMIA AKILI BASI
 
Swagger hazileti pesa,huenda kipaji cha muziki kimetoka kwa mama.
Alafu Diamond swagger na kipaji karithi kwa baba....

Ila upumbavu kulea kibenten Cha mama, eti anamwita Uncle Shamte
 
Sio kweli kwamba kila mwanamke anayezaa na wanaume tofauti ni mdangaji. Kuna wanaume hawawezi kuwa baba walezi, kuna wanaume wakatili, kuna wanaume wanabadilika baada ya kumzalisha mwanamke, kuna watu wanachokana kabisa baada ya kuishi pamoja kwa muda mrefu
 
Baba yake Diamond alikosa pesa au alishindwa kutoa pesa/alitelekeza familia?
Mfano kama mama yake hakupewa pesa za matunzo ndy ashindwe kumsaidia baba yake?

Wewe baba yako aliweza kukupa kila ulichohitaji utotoni?

Je huwezi kumsaidia?

Lazima ujuwe jinsi ya kutofautisha kati ya kukosa pesa,,na kukataa kutoa pesa.
 
Baba yake Diamond ndiye aliyesema hivyo?
Huyu mama anaonekana ni mzinzi,mpenda Shari,jeuri,kiburi,mwenye tabia ya kuweka kinyongo na asiyejiheshimu. Ni kweli inawezekana mzee alipiga chini kujiepusha na kero hizo
 
Masharti ya pesa za uchawi, lwanda magere amekwisha litolea ufafanuzi hili mapema haiingi akilini mama ale maisha ilihali baba kula yake ni ya kuunga unga....
 
KAMA alimtelekeza mama yake na Diamond alikuwa anaishi na mama yake basi aliwatelekeza wote wawili labda kama alikuwa amemuwekea Diamond order ya kula kwa mama ntilie peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…