Eti kimikakati. 😄 Naona umekuwa mpole sana, baada ya kuumbuka ukijaribu kueneza udini wako kwa kutumia uongo. Kwenye hili jukwaa hoja huwa zinapangwa na kupanguliwa kwa kutumia 'facts' na takwimu. Sio hadithi ambazo huwa mnasimuliana, mkiwa kwenye vijiwe vyenu vya kahawa hapo Uwanja wa Fisi.
Census ya Kenya 2019;
Kenya: population by religious groups | Statista Wakristo nchini Kenya- 85.59%
Waislamu- 10.90%
Kama unamaanisha kwamba gatuzi za pwani, nchini Kenya, zina waislamu wengi zaidi ya wakristo umenoa. Kwenye gatuzi zote sita za pwani kwa pamoja, waislamu ni 40%, wakristo nao ni 60% ya wakazi wote.
Kenya’s Coast: Religion, Race, Ethnicity and the Elusive Nature of Political Community
Siungi mkono ukabila, uovu huo hauna faida na huwa unaendelezwa na wanasiasa, kwa faida yao. Kuna siku utakuja utokomezwe kabisa nchini Kenya na sasa hivi tunaelekea huko.