Huu utaratibu wa kuwakatia viuno wageni kwenye viwanja vya ndege nani aliuanzisha?

Huu utaratibu wa kuwakatia viuno wageni kwenye viwanja vya ndege nani aliuanzisha?

🔷 Ni vyema Mgeni anapofika kwako kwa mara ya kwanza akapokelewa na utamaduni wenu

🔷 Mimi sipingi wageni kupokelewa na burudani wanapofika kwenye malango ya nchi yetu ni jembo jema Sana na la kiungwana

🔷Lakini je! Wanaowapokea wanawawakilisha utamaduni halisi wa kabila lolote la Mtanzania?

🔷 Tanzania tuna ngoma ya asili ya matarumbeta? Tanzania tuna ngoma ambayo watu wanavaa sare kama waimba kwaya?

🔷 Ngoma ninazozijua Mimi watu wanavaa mangozi, manyoya ya wanyama, maleba, njuga , sura za vinyago na kujipaka mavumbi mazizi na makorokocho ya kutisha huku wakichezea wanyama pori kama nyoka, fisi nk huku manyu akitamba mbele kwa kujirusha au kupiga ngoma kwa tumbo makalio nk hata mtoto mdogo akiona analia au Mgeni akiona anajua amefika nchi ya kiumeni Afrika.

🔷Sasa wapo wajanja wajanja wa hapo Dar eti wsnapuliza matarumbeta au wale wa chuo Cha bagamoyo wanaocheza ngoma zilizochakachuliwa na utamaduni wa wazungu wa Scandinavia ndio eti wanatambulisha utamaduni wa bongo

🔷 Doctor Mapanaa naamini upo huku unanisoma, kama uliwaimbisha wazungu kigogo huko ulaya na wakaimba na kucheza kweli unashindwa kutafuta kikundi halisi Cha ngoma Kupokea wageni wetu ? Unashindwa kweli kwenda singida Kuna wanyaturu wanaocheza Mawindi, wagogo wapo Dodoma na mbwembwe zao, shinyanga Kuna maguno ya Jeshi, Mwanza Kuna Mwanalyaku, , bujora na Ukerewe vipo vikundi halisi vya ngoma achana na vidogoli vya wajita na wakerewe wale watachelewesha mambo maana wanaongea Sana mpaka waje wskatike sio Leo. Mara Kuna watu watatikisa vichwa yule jamaa wa Kenya wa kuandamana usiku Cha mtoto

🔷Morogoro Kuna vitu vya hatari, kusini ndio usiseme Sindimba, mganda nk .

🔷 Kaskazini Kuna wamasai wanaruka juu balaa na ni marafiki wakubwa wa watalii, Tanga Kuna ngoma zao nyingi tuu, acha zile zinazochezwa na wanawake Kuna zile za wawindaji ( naukala ndima) zima mvuto wa kipekee, Wachaga achana nao wamedanganywa na dini na kuambiwa Mila na ngoma zao ni za kizamani. Wameacha ngoma zao za kuzunguka kama mduara Sasa wamekuwa kama watumwa wakienda nje wakiambiwa waonyeshe utamaduni wao wanajifanya wamasai kama mwijaku.

🔷 Hivi doctor Mapanaa na Wizara ya utamaduni hamuoni hata ngoma za wahaya wanavochenkula?

🔷Nchi likubwa kama hili tunashindwa kufanya venting ya kikundi Cha ngoma ambacho Mgeni akiona ataendelea kuota Maisha yake yote? Shida nini? Kama NDEGE tunayo tunadondwa kusafirisha vikundi vya ngoma na makorokoro Yao yote tena wakiwa kwa wingi wao na sio watu wachache tukaitamgaza nchi yetu baadaye tukapata return ya utalii wa kitamaduni? Mama naomba uteuzi Mimi avogadro kwenye Wizara ya utamaduni , Mimi nita deal na utamaduni tuu hii michezo imeimeza na ndani ya mwaka utamaduni utaamka na tutaamza kushuhudia mafurikonya watalii
Mkuu nimecheka sana, sana mno! Kila aya yako mbavu zimenivunjika.

Naunga mkono hoja yako, upewe tu hicho kitengo cha utamaduni!
 
Sidhani kama upo sahihi nawala sidhani kama unahitaji msaada wa kueleweshwa, kwa maana hii baki na ujinga wako.
jenga hoja upangue maoni yanga, akili ya kuniona mjinga unaipata wapi ukiwa unaonekana we ni mtu mwenye akili? Wapi uliona rais wetu anachezewa ngoma huko ziara za nje ya nchi zaidi ya gwaride la heshima la jeshi, unadhani watu wa nje hawana utamaduni wao wa kukaribisha wageni? Nyie ndio wale humu mkishindwa kujenga hoja mnakimbili kutukana na kuona wengine ni wajinga huku mkijianika ujinga wenu wazi
 
M
Ukihitaji salamu njoo unikatie mauno kwanza kama Yondo, tofauti na hapo utaambulia chuya!

Huu utaratibu ulianza kama mzaha lakini kadiri siku zinavyozidi ndivyo hali inakuwa mbaya,kitu kibaya zaidi hadi wanaume watu wazima utawakuta nao wamejifunga kibwebwe wanakata mauno bila aibu wala soni!.

Viongozi wetu wakienda nchi za watu walioendelea huwezi kuona huu uwendawazimu wa kina mama na kina baba wa huko kukata mauno kama wendawazimu!.

Zamani viongozi walipokuwa wakija hapa nchini kulikuwa na vikundi vya ngoma za asili vilivyocheza kwa staha,madoido na mbwembwe bila kukata mauno ovyo!, Sijajua siku hizi hivi vikundi vimepatwa na nini maana siyo kwa miuno hiyo inayokatwa!.

Kuna mtu nilikuwa najadiliana nae akaniambia kwamba huo ndiyo utamaduni wetu na wageni wanapokuja wanapaswa wakatiwe viuno ili wafurahie utamaduni wa mtanzania!.

Kama ndivyo aisee hii ni hatari sana!.

Nimeshangaa sana kuona mijibaba yenye ndevu ikiwa inakata mauno mbele ya Rais wa Germany!,Rais kazi yake ilikuwa ni kupiga makofi tu na kushangaa!, bila shaka nadhani akirudi Germany ataenda kuwasimulia wenzie, hivyo tutegemee ugeni mzito kutoka Germany kuja kushangaa wakata miuno pale JKNIA!
Mwendo wa vibuno ,vibuno
 
ni utalii wa sanaa na utamaduni tu huoni wakija wajerumani wengine tumeingiza pesa kwenye mfuko wa chama na serikali
 
Back
Top Bottom