Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

serikali pia inachangia kuwasema vibaya wakina baba . hawana mchango serikalini mfano utakuta siku ya kina mama mara haki za kina mama mara dawati la uonevu la kina mama mara tv na radio zoote kuna vipindi vya kina mama
Hahahaha
 
Hii dharau mkuu.....
 
Hahahaha Kama nakufahamu vile maana hii story ya kuishi kisela mtu na dingi yako niliwahi kusimuliwa na bwanamdogo mmoja hivi
Inawezekana asee. Maana mimi ukinikuta na mshua wangu kitakachokufanya ujue ni mdingi wangu ni ile kufanana tu ila matendo na maneno unaweza kudhani ni washkaji tu.
 
Nimegundua baba/mama ni muhimu nfio maana Hata kama yeye ndio alitelekeza mimba ila mtoto akikua atamtafuta hadi ampate.

Mimi wazazi wote wapo ila baba yangu wa ubatizo Sijawahi kumuona, yaani hua Natamani nikamtafute japo tu nimuone au niwaone kaka zangu wa ubatizo (I'm so crazy 😂)
Imagine baba wa ubatizo ananiuma hivi je baba mzazi itakuaje?
Tuwapende baba zetu Aisee wangalipo maana Within a second inaweza baki history kua ulikua na baba.
 
Kivyovyote hapa inaonyesha wewe, Siyo mtoto ulievuka kizingiti cha nyumba, ambayo Baba yako pia anaishi na yeye kukupeleka hiyo shule unayosoma.

Kwa watoto waliozaliwa na kukulia nje ya nyumba ambayo Baba huishi, kuna weza kutokea upunguvu wa upendo kidogo, ila siyo kwa watoto ambao amevuka kizingiti cha mlango nyumba, ambayo Baba huishi humo.
 
Thamani ya baba na mama,haijwahi kuwa sawa. Mama ana thamani kubwa yaani mara tatu zaidi ya baba. Mimi ni baba,ila sitashangaa kuja kuona watoto wangu wakimthamini sana mama yao na kumfanyia mema.

Suala la kufa yoyote ana kufa tu,ni muda tu ukifika.
Baba N mama wote wana thamani sawa kwangu kubwa
 
Mwanaume halafu "UKALIA" Sana? Hizo swaga za kulia-lia SI za kiume Kama unavyojifariji
 
Huo uhovyo unaousema kuna siku hautauona..utamkumbuka Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila sisi wengine Mola wetu ametupa mapenzi na familia zetu sana,hasa watoto,nawapenda sana watoto wangu,mpaka wake zangu wanajua.

Ila wapo baba wengine mtihani sana,mpaka unajiuliza inakuwake akawa baba...?!
Dah Mungu akubariki sana I wish ningepata upendo wa wazazi wote wawili nijue ladha yake ila ndio hivyo sijabahatika.
 
Tena wa kiume ndo hawana time na dingi, wanaona anazingua kila kitu ni kwa mother. Watoto wa kike ndo wanakuwaga na uchungu na baba...
Uko sahihi mm ninawatoto wakubwa wanne,mkubwa kabisa wa kiume ana 29 yrs huyo hana time na Mimi ila anaemfuatia wakike ana 26yrs huyo ananipenda Sana baba yake
 
Sisi alitufukuza usiku wa mbaramwezi nakumbuka kulikuwa na umande tukapitia uwanja wa michezo ulikuwa nyuma kidogo ya nyumba. Mama alikuwa anaogopa mbwa hivo hatukupitia kwa nyumba za majirani, mzee ana kacheo flani hakuna jirani angeweza tuhifadhi. Sikumbuki tulilala wapi nilikuwa mdogo bado.

Kumbukumbu yangu nyingine na mzee ni pale amekutana na mimi bila kutarajia wilaya nyingine giza linaanza ingia hivi amelewa anaongea lugha na sauti tofauti kidogo, aisee sikumtambua. Alinishikashika na kuniongelesha nilikuwa na binamu, nilipofika kwa mama nikamshtaki mzee kwamba kuna mwanaume nimekutana naye kanishikashika. Kipindi utotoni tunapigwa marufuku kuongea na strangers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…