Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamkufanya action yoyote bado?Anasubiri kwenda form five mwezi ujao
Barehe imepiga mwereka ,hormone inachemka mpaka inafurumia lazima upate hasiraHabari wanajamvi...
Nina imani humu kuna wazazi ambao walishawahi kua na watoto wenye tabia kama hizi naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri unisaidie na mimi.
Binafsi nina mdogo wangu aliyenifuata wa kiume, ana miaka 17...huyu mdogo wangu alikua ni mpole Sanaa, akiwa nyumbani ni mtu wa kushinda ndani mda wote ni kusoma kula na kulala, mara chache sana unaweza kumkuta anaangalia movie hata marafiki zake ni mpaka waje nyumbani kutembelea ndo apige nao story bila hivyo hatoi mguu nyumbani labda aagizwe mahali..
Shida kwamba sikuizi( yani miezi hii hapa miwili) amebadilika sana hadi tunaogopa,, amekua ni mtu wa kuondoka nyumbani bila kuaga na akiondoka asubuhi harudi nyumbani msipompigia simu anaweza asionekane kabisa hadi usiku,, sometimes tukimpigia simu anaweza akapokea halafu akajibu kwa ukali kua tusimfatilie na maisha yake, hataki kula chakula nyumbani, amekua ni mtu wa kufokafoka tu mda wote hadi mama akimuuliza kitu anajibu kwa kufoka tu sio kama alivyokua zamani.
Saizi amefikia hatua kwenda kanisani pamoja na sisi hataki anasema tumuache., alikua anaumwa hakutoa taarifa mpaka anapona na hatuelewi alikua anaumwa nini yani tumefanya tu kustukia kumwona anakunywa dawa, kuna mda alivyoondoka mama akaingia chumbani kwake kukagua akakuta dawa nyingi sana, hata hatuelewi zinatibu ugonjwa gani., baada ya mama kumuuliza alikua mkali sana na ametupigia marufuku kuingia chumbani kwake hata kama ni kufanya usafi.
Ajabu ni kwamba tukimuelezea baba tabia za huyu dogo sikuizi wala hata hatilii maanani anasema tu muacheni kama alivyowaambia mumuache...hasa tatizo ni lipo kwa mama amekua na wasiwasi sana na mabadiliko ya huyu mdogo wangu yani pressure inampanda mda wote, akijaribu hata kukaa nae chini kuongea nae dogo hataki kumskiliza yeyote zaidi ni anakua mkali ukimsogelea jirani anaweza akupige makofi...
Naombeni msaada wenu wa mawazo ili niweze kumsaidia huyu mdogo wangu maana napata shida sana kumuona mama akiwa na wasiwasi mda wote [emoji1374]
Okay, sawa.Mzee kasafiri nae kwanza saiz,, nahisi atakaporudi atakua amechange
Ukute ndio anabaleheAsante,, tutajaribu kuufanyia kazi ushauri wako...ila kwenye suala la marafiki tumejaribu kuongea na marafiki zake wote nao wanasema wanashangaa mabadiliko yake yanatokana na nini
hii imeendaaLeejay49 niruhusu ni ku PM, nimejaribu kuandika ushauri kuhusu huyo mdogo wako ,nisingecoment hapa kwenye jukwaa, kwa kuwa nimehusisha maisha yangu, thus why kuna code ziko wazi sana kuhusu mimi .
Nimeshindwa kusend kwa kuwa umefunga PM yako , ila nimeusev kama hutajali nikutumie.
Watu Wana lalamika wanasema ufungue PMKapelekwa kwa wajomba zake nadhani wako wanamshughulikia saizi..hope akirudi atakua kachange[emoji4]
huu upendo ulianza linji kwa Leejay49 wangu aisee tutapigana humu ndani afungue pm ya nn😠😠😠😠😠Leejay49 niruhusu ni ku PM, nimejaribu kuandika ushauri kuhusu huyo mdogo wako ,nisingecoment hapa kwenye jukwaa, kwa kuwa nimehusisha maisha yangu, thus why kuna code ziko wazi sana kuhusu mimi .
Nimeshindwa kusend kwa kuwa umefunga PM yako , ila nimeusev kama hutajali nikutumie.
namshangaa sana jamaa sjui nimpige juju🤣Jamani wewe😃😃