Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Bila shaka ni last born ndio maana mpk usafi mnamfanyia. Hapo ni stiki tu akili itamrudi.
 
baba ake ndo atamuweza inawezekana ana mental illness!! plus kuna kitu hakiko sawa kisaikologia na kiakili huyo mtoto hana msiri hapo nyumbani ndo maana hataki hata mjue afya yake
 
Huyo ameshaingia kwenue uvutaji wa bangi, ana makundi. Kijana wangu alibadilika hivo hivo.

Namshukuru Mungu nilitumia njia rafiki sana kumrejesha. Baba atumie njia ya kukaa nae, azungumze nae kwa utaratibu, awe rafiki hasa, asitumie ukali na vitisho.

Wa kwangu nilifanya hivo, alikuwa genius sana maana form two alipata A zote, baada ya hapo alidrop sana ( ndicho kipindi alianza bangi)

Mwaka huu amemaliza form six ila ametulia, zipo tu kasoro za ucheckbob hivi na mawazo ya kimaisha yasio ya kiuhalisia
 
Kijana wa umri kama huo hajichanganyi na wenzake, hachezi mpira , itakuwa sigara au mabangi tu.
 
Waliondoka na mzee walienda kwa baba zake wakubwa huko alimwacha kama wiki hivi wakamrudisha akiwa mtulivu hadi leo hajasumbua tena,. Ila tu hawataki kutuambia walimfanya nini😃😃
😀😀😀 hata yeye mwenyewe mkimuuliza anasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…