Huwa tunawacheka nyumbu wengi wakiteswa na simba mmoja. Leo nchi zote duniani zinateswa na US.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Binadamu ni wanyama tu kama wanyama wengine. Tuache kuwacheka nyumbu wengi wakifurumushwa na simba mmoja.

Historia fupi hadi tumefika hapa: US ameanza kuisumbua dunia mara tu baada ya vita kuu ya pili ya dunia. US ndiye aliibuka walau yupo salama, viwanda vyake vikifanya kazi na mashamba yake yakifanya kazi huku huko Ulaya na Asia kukiwa magofu matupu. Hilo likamfanya ndiye awe mzalishaji mkuu wa dunia. Hata pesa ya akiba duniani ikatoka Strerling ya Uingereza kuwa USD ya Marekani. Kama pound iliyotangulia, nayo USD ilikuwa backed na dola. Kwamba ukiuza kitu chochote duniani na ukapata dola, basi unaweza kuichukua hiyo dola na kuipeleka US na US wanakupa dhahabu. Bei ya dhahabu ilikuwa fixed kwa dola 35 kwa ounce(Kama gram 31).

Kwa sababu US alikuwa anazalisha kuliko anavyonunua alikuwa ana uhakika kuwa watu wenye dola watakuja kununulia tena vitu kwake badala ya kuja kudai wapewe dhahabu.

Miaka ya 60 mwishoni US akaanza kupata ushindani sokoni. Akawa ananunua zaidi kuliko anavyouza. Nchi nyingi zikaanza kujawa na dolari huku hazihitaji kununulia chochote. Hivyo zikahitaji kupeleka hizo dolari USA ili zipewe dhahabu.

US akaona hapa dhahabu zangu zitaisha. Akasema kuanzia leo sibadilishi tena dola kwa dhahabu. Ulizojikusanyia utajijua mwenyewe. Ila ukitaka unaweza kuja kuziwekeza huku kwangu kwa kununua majengo, viwanda vinavyoelekea kufa, kununua bond zangu, kuwekeza kwenye makampuni ya bima. Hapo nchi zote ambazo zilikuwa zinauza kuliko kununua, kama Japan, nchi ambazo zilikuwa na akiba kubwa ya dola ikabidi zianze kwenda kuwekeza hizo dola zao US kwa kununua makampuni na bond. Inasemekana hadi sasa Japan amewekeza US kama dolar trilioni 1.2. Ukisikia Japan anamdai USA basi ni hizo pesa alizowekeza US, hasa kwenye bond.

Kumbuka kuwa hayo yote yanawezeshwa na kitendo cha USD kuwa pesa ya dunia. Maana yake nchi kama Saudi Arabia wakituuzia mafuta inabidi tuwalipe kwa dola(Tulizopata labda kwa kuwauzia Japan Kahawa). Wakiwa na dola nyingi na hawana cha zaidi cha kununua wanazipeleka USA kuwekeza kwenye bond, majengo na vitu vingine walivyoruhusiwa. Uwekezaji kwenye bond unaifanya US izidi kuchapisha dola. So US anachapisha na kununua vitu mbalimbali duniani, hao aliowauzia nao wanazirudisha hizo dola US kwa kununua majengo na bond, kununuliwa kwa bond kunafanya US achape zaidi dola!! Ni pyramidi scheme moja matata, huku USA akiishi kwa nguvu za wengine sababu dola yake ndiyo pesa ya dunia. Na atafanya chochote kulinda hilo.

Baadaye China akakaribishwa kwenye huo ulingo. Huyu ndiyo balaa, anazalisha na kuwa na dola nyingi sana. Naye kuziwekeza ni kwenda kununua bond za Marekani, kukopesha sisi makapuku, kujenga miradi kama walivyotaka bandari ya bagamoyo nk nk. So Nchi kama China, USA na Japan zimewekeza dola nyingi USA. Hata leo dola ikianguka nao wanapata hasara kubwa sana. Hivyo haziko tayari kuona dola ikianguka, na tayari pyramidi scheme hii ya dola imewafanya wawe matajiri wakubwa(Kidogo wameanza kubadili mawazo baada ya US kufreeze dollar za Russia.)

Wakati huo huo wingi wa dola unasababisha mfumuko wa bei Marekani na Kufanya maisha yawe magumu sana. Sababu pesa kutoka nje zinaenda kununua majumba bei ya majumba ikawa haishikiki. Na sababu pesa hizo zinaenda kuwekeza kwenye finance sekta na si kwenye uzalishaji hasa, na mfumuko wa bei kufanya uzalishaji ndani ya USA kuwa ghali-ajira za maana USA zikaanza kufa.

Trump ameona kuwa hii pyramidi haiwezi kuendelea hivi. Inabidi turudishe uzalishaji Marekani. Inabidi tupunguze matumizi ili tupunguze uchapaji wa pesa(Ndiyo kuanzisha DOGE). Ili kurejesha uzalishaji Marekani Trump ameamua kuzipiga bidhaa kutoka nchi nyingine ushuru mkubwa. Lengo ni kuwafanya wazalishaji hao wahamie kuzalisha ndani ya USA au watu wa USA wenyewe waanze kuzalisha bidhaa hizo ambazo zitakuwa ghali kuagiza.

Tungekuwa tumechangamka hizi tarriffs ni faida kwetu tuliopigwa tarrifs kidogo. Tungeweza ibadili nchi kama Bangladesh kwenye kuuza nguo. Tuchangamke tuzalishe wenyewe. Tukileta viwanda kutoka kwa Wachina au Wahindi tutapigwa na tariffs muda si mrefu.

Usikute nyumbu mmoja akiliwa na simba wenzake hufurahi. Husema, "Afadhali majani sasa yatakuwepo ya kutosha."
 
Tulia mkuu hii ngoma bado mbichi... Wakati jitu kubwa linakata roho lazima lirusherushe miguu kitu ambacho ni hatari kwa waliokaribu nalo
Nimeandika tu hadi tulipofikia. Hatujui kesho itakuwaje. Nyumbu wanaweza sema liwalo na liwe.
 
Anachofanya Trump anataka wakubwa wenzake waweke mipango yao mezani ili Marekani ianze kujipanga kukabiliana nayo... Unakumbuka kabla hajaapishwa alitishia kwamba iwapo Urusi na China wataitumia BRICS kubuni pesa ya kimataifa mbadala wa dollars, basi yeye atapandisha ushuru kwa wanachama wote wa brics kwa 200%.
Fuatilia siasa za kimataifa kwa undani utaweza kutabiri yajayo kwa asilimia kubwa sana
 
Sasa kama uchumi wa jimbo moja tu ni kama bara zima la africa kwanini wasiwe kama nyumbu mkuu?
Ni bora huo uchumi ungekuwa unaendeshwa kwa uzalishaji. Kwamba US anatengeneza vitu anauza. Unaendeshwa kwa deni kubwa ambalo halitakaa lilipwe.
 
Ni bora huwa uchumi ungekuwa unaendeshwa kwa uzalishaji. Kwamba US anatengeneza vitu anauza. Unaendeshwa kwa deni kubwa ambalo halitakaa lilipwe.
Kwani hawatengenezi vitu,
Na kuuza?
 
Anachofanya Trump anataka wakubwa wenzake waweke mipango yao mezani ili Marekani ianze kujipanga kukabiliana nayo... Unakumbuka kabla hajaapishwa alitishia kwamba iwapo Urusi na China wataitumia BRICS kubuni pesa ya kimataifa mbadala wa dollars, basi yeye atapandisha ushuru kwa wanachama wote wa brics kwa 200%.
Fuatilia siasa za kimataifa kwa undani utaweza kutabiri yajayo kwa asilimia kubwa sana
Wachambuzi wa mambo wanasema hizi tariffs moja ya lengo lake kuwaleta watu(nyumbu)mezani kujadili. Mfano anamwambia Ujerumani akitaka asipigwe ushuru wa 25 kwenye magari basi ahamishie viwanda US. Anamwambia Japan na China hizi bond mlizonunua kwangu tunaextend muda wa kumature nk nk.

Unafikiri ni yapi yajayo?
 
Sijauliza sababu ila nimeuliza US hawazalishi kuuza?
Sikukupata fresh. Kinachomatter ni trade deficits. Yaani wananunua kuliko wanavyouza. Hiyo USA wanayo toka miaka ya 70. Fikiria mwenyewe binafsi ukiwa unanunua mahitaji mengi kuliko pesa unayoingiza kwenye biashara yako!!? Utaishia kukopa. Ndiyo US anakopa kwa kuchapa pesa. Utasema uchumi mkubwa wa USA lakini unaendeshwa na madeni. Tutasema unahela kumbe unaishi kwa mikopo.
 
Japan US, na China ndio nchi zenye madeni makubwa ,kwa mtazamo wako ukiaachana na hizi nchi tajiri zisizokua na madeni ni zipi?
 
Ukitaka kufananisha madeni ya nchi inabidi uende mbali. Uangalie kiasi inachodai na kiasi inachodaiwa. Hapo Japan na China wanadai kuliko wanavyodaiwa. Hizo nchi zingine utaziangalia katika hilo.
 
Wachambuzi wa mambo wanasema hizi tariffs moja ya lengo lake kuwaleta watu(nyumbu)mezani kujadili. Mfano anamwambia Ujerumani akitaka asipigwe ushuru wa 25 kwenye magari basi ahamishie viwanda US. Anamwambia Japan na China hizi bond mlizonunua kwangu tunaextend muda wa kumature nk nk.

Unafikiri ni yapi yajayo?
Tuupe muda nafasi...
 
Ukitaka kufananisha madeni ya nchi inabidi uende mbali. Uangalie kiasi inachodai na kiasi inachodaiwa. Hapo Japan na China wanadai kuliko wanavyodaiwa. Hizo nchi zingine utaziangalia katika hilo.
Sikatai ila uchumi wa nchi una mambo mengi yanaangaliwa mpaka useme hii ni nchi tajiri yakiwemo na hayo uliyoyataja, China inakuja vizuri ila kwa Us bado mno.
 
Kabla Trump hajaapishwa kuna wafia siasa humu walisema Tanzania na Makonda wake watakoma!.
Kumbe amna bana mara hii Babu acheki na wowote anapiga spana kila kona.
 
Acha masikhara mkuu kwamba Trump anaijua Tz na umeenda mbali zaidi hadi kwa Makonda, si waona hata hizo tarrifs nchi nyingi za ulimwengu wa tatu tumefanana, labda walitugroup tu
 
Binadamu ni wanyama tu kama wanyama wengine. Tuache kuwacheka nyumbu wengi wakifurumushwa na simba mmoja.

Historia fupi hadi tumefika hapa: US ameanza kuisumbua dunia mara tu baada ya vita kuu ya pili ya dunia. US ndiye aliibuka walau yupo salama, viwanda vyake vikifanya kazi na mashamba yake yakifanya kazi huku huko Ulaya na Asia kukiwa magofu matupu. Hilo likamfanya ndiye awe mzalishaji mkuu wa dunia. Hata pesa ya akiba duniani ikatoka Strerling ya Uingereza kuwa USD ya Marekani. Kama pound iliyotangulia, nayo USD ilikuwa backed na dola. Kwamba ukiuza kitu chochote duniani na ukapata dola, basi unaweza kuichukua hiyo dola na kuipeleka US na US wanakupa dhahabu. Bei ya dhahabu ilikuwa fixed kwa dola 35 kwa ounce(Kama gram 31).

Kwa sababu US alikuwa anazalisha kuliko anavyonunua alikuwa ana uhakika kuwa watu wenye dola watakuja kununulia tena vitu kwake badala ya kuja kudai wapewe dhahabu.

Miaka ya 60 mwishoni US akaanza kupata ushindani sokoni. Akawa ananunua zaidi kuliko anavyouza. Nchi nyingi zikaanza kujawa na dolari huku hazihitaji kununulia chochote. Hivyo zikahitaji kupeleka hizo dolari USA ili zipewe dhahabu.

US akaona hapa dhahabu zangu zitaisha. Akasema kuanzia leo sibadilishi tena dola kwa dhahabu. Ulizojikusanyia utajijua mwenyewe. Ila ukitaka unaweza kuja kuziwekeza huku kwangu kwa kununua majengo, viwanda vinavyoelekea kufa, kununua bond zangu, kuwekeza kwenye makampuni ya bima. Hapo nchi zote ambazo zilikuwa zinauza kuliko kununua, kama Japan, nchi ambazo zilikuwa na akiba kubwa ya dola ikabidi zianze kwenda kuwekeza hizo dola zao US kwa kununua makampuni na bond. Inasemekana hadi sasa Japan amewekeza US kama dolar trilioni 1.2. Ukisikia Japan anamdai USA basi ni hizo pesa alizowekeza US, hasa kwenye bond.

Kumbuka kuwa hayo yote yanawezeshwa na kitendo cha USD kuwa pesa ya dunia. Maana yake nchi kama Saudi Arabia wakituuzia mafuta inabidi tuwalipe kwa dola(Tulizopata labda kwa kuwauzia Japan Kahawa). Wakiwa na dola nyingi na hawana cha zaidi cha kununua wanazipeleka USA kuwekeza kwenye bond, majengo na vitu vingine walivyoruhusiwa. Uwekezaji kwenye bond unaifanya US izidi kuchapisha dola. So US anachapisha na kununua vitu mbalimbali duniani, hao aliowauzia nao wanazirudisha hizo dola US kwa kununua majengo na bond, kununuliwa kwa bond kunafanya US achape zaidi dola!! Ni pyramidi scheme moja matata, huku USA akiishi kwa nguvu za wengine sababu dola yake ndiyo pesa ya dunia. Na atafanya chochote kulinda hilo.

Baadaye China akakaribishwa kwenye huo ulingo. Huyu ndiyo balaa, anazalisha na kuwa na dola nyingi sana. Naye kuziwekeza ni kwenda kununua bond za Marekani, kukopesha sisi makapuku, kujenga miradi kama walivyotaka bandari ya bagamoyo nk nk. So Nchi kama China, USA na Japan zimewekeza dola nyingi USA. Hata leo dola ikianguka nao wanapata hasara kubwa sana. Hivyo haziko tayari kuona dola ikianguka, na tayari pyramidi scheme hii ya dola imewafanya wawe matajiri wakubwa(Kidogo wameanza kubadili mawazo baada ya US kufreeze dollar za Russia.)

Wakati huo huo wingi wa dola unasababisha mfumuko wa bei Marekani na Kufanya maisha yawe magumu sana. Sababu pesa kutoka nje zinaenda kununua majumba bei ya majumba ikawa haishikiki. Na sababu pesa hizo zinaenda kuwekeza kwenye finance sekta na si kwenye uzalishaji hasa, na mfumuko wa bei kufanya uzalishaji ndani ya USA kuwa ghali-ajira za maana USA zikaanza kufa.

Trump ameona kuwa hii pyramidi haiwezi kuendelea hivi. Inabidi turudishe uzalishaji Marekani. Inabidi tupunguze matumizi ili tupunguze uchapaji wa pesa(Ndiyo kuanzisha DOGE). Ili kurejesha uzalishaji Marekani Trump ameamua kuzipiga bidhaa kutoka nchi nyingine ushuru mkubwa. Lengo ni kuwafanya wazalishaji hao wahamie kuzalisha ndani ya USA au watu wa USA wenyewe waanze kuzalisha bidhaa hizo ambazo zitakuwa ghali kuagiza.

Tungekuwa tumechangamka hizi tarriffs ni faida kwetu tuliopigwa tarrifs kidogo. Tungeweza ibadili nchi kama Bangladesh kwenye kuuza nguo. Tuchangamke tuzalishe wenyewe. Tukileta viwanda kutoka kwa Wachina au Wahindi tutapigwa na tariffs muda si mrefu.

Usikute nyumbu mmoja akiliwa na simba wenzake hufurahi. Husema, "Afadhali majani sasa yatakuwepo ya kutosha."
Mwisho wake ndio umefika
 
Viwanda haviwezi rudi marekani kama DT anavyofikiri.

Ni wajinga tu wataona Marekani ina potential ya kupokea viwanda na kuacha kwenda Asia( future ya dunia inayokuja around the corner)

Subiri wanaozijua siasa za duniani kuliko huyo mwehu DT nao waanze kuchanga karata zao ndipo itajulikana nani mjanja.

Trump bado ana kiburi cha America supremacy anapoteza vyote mpaka washirika wale waliokuwa wa kuaminika wa marekani.
 
Back
Top Bottom