Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Kuna mshkaji wangu nilikua naendaga kwao na wana mbwa ila wanasema ni coco yani mchana hana madhara mpaka usiku na pale kwa mshkaji naendaga mara nyingi tu na mbwa huwa ananiona ila hanaga ile kumfuata mtu miguuni kama wanavyofanya mbwa wengine wakiona tu mgeni kaingia haoo wanamkimbilia


Huyu hakua na hizo mambo yani wewe ukiingia utamkuta kalala zake hana time na wageni,sasa siku moja usiku nilienda tena kwa mshkaji wangu tukawa tunacheki movie ndani baadae muda wa kuondoka tumetoka nje mbwa yupo kibarazani na pale nje kulikua na mabox mawili jamaa akaniambia nimsaidie kuingiza ndani yeye akabeba box moja akaingia ndani sasa ile nataka kubeba box mara simu yangu ikaita hapo mbwa ananichora tu,nilivomaliza kuongea na simu ndo nikabeba box niingize ndani yani ile nakaribia mlango tu naskia mbwa ananikimbilia anabweka akapeleka mdomo wake karibu na mguu dah nilikimbilia ndani mwili unasisimka yan ilibaki kidogo tu achomoe mnofu
 
Asilimia 100 Kwa maana hata mbwa awe wa wapi mimi hawezi ningata mbwa ni kiumbe rahisi sana kumtawala ukishaijua saikolojia ambayo ni simple tu kuonyesha humuogopi na kutulia hata akikutishia
 
Hahah
 
Na waking'ata na sumu ndo baas
 
Ukiambiwa hivyo usiamini kwa asilimia 100 nakumbuka niliambiwa hivyo na mwenyeji wangu baadae wakati naongea na simu nikashangaa yule dogi kanipiga jino kalioni tena kwa kuvizia ni dog anayeng'ata kimyakimya mwanzoni nilikuwa nashangaa huyu dog mbona anazungukazunguka nyuma yangu kumbe anatataka kuning'ata kalio hii leo hata nikienda kwa jamaa yule dog simpi nafasi ya kukaa nyuma yangu
 
Mradi utesek tu [emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Husimuangalie mbwa macho Kwa macho na dhibiti uoga mwili wako hisije kutema Adrenaline , atasikia harufu
 
Ungekimbia tu ungeisoma namba [emoji23][emoji23]
Aisee sio tu ningeisoma namba bali pengine leo hii ningekuwa naitwa marehem fulani, au wangeniachia ulemavu wa kudumu, maana hakuna mbwa mkali, hatari na mwenye nguvu kama pit bull. Huyo german shepherd mwenyewe akikutana na pit bull ujue siku hiyo hata wenye mbwa wao wenyewe watashindwa kuwaamua.

Na isitoshe walikuwa wakubwa last namba afu wameshiba haswa, wakitembea unasikia chini ti ti ti ti.
 

Attachments

  • images (64).jpeg
    21.5 KB · Views: 5
Kuna mbwa na Bata mzinga

Nikikutana na hivyo Vitu kwako siingii getini
Hahaha bata nao sometimes wanazingua. Hata hawa tunaowafuga ukikaa vibaya ujue anakutoa nduki kulaleki.
 
Mbwa hafai, kuna nyumba moja iko jirani na tunakoishi kuna Mzungu alikuwa anaishi hapo na anafuga mbwa wakubwa tu. Na yana sauti kubwa yakibweka, na yeye huwa anatoa kauli hiyo hiyo. Sasa kuna siku nilikatiza hapo kwake mchana, na nilikua nimejisahau kama kuna mbwa wakali, sijui nilikua nawaza nini!! Ghafla mbwa wanaunguruma pembeni yangu, kugeuka kuangalia, naona mbwa wawili wako spidi wananifuata. Sikujiuliza mara mbili, nilifyatua mbio huku napiga mayowe. Na ndala niliziacha palepale getini kwake!! Ila nilishangaa kuona watu wananicheka, halafu wala hawana mpango na mimi. Baadaye nikasimama baada ya kuona kimya, kuja kufuatilia, kumbe wako ndani ya fence, zile za waya, kwa nje kumepandwa michongoma. Kwahiyo ukicheki kwa haraka, utaona michongoma tupu. Nikazirudia ndala zangu, nikasepa.
 
Mbwa ukimjua jina hakupi shida.
Sisi kwetu ilikuwa lazima utambulishwe kwa mbwa, la siivyo hukai kwa raha.
Kwaiyo kama ni mgeni unaenda bandani kwa nje, anaitwa Max huyu ni mgeni atakuwa pamoja nasi siku zote la siovyo mgeni unacho. Sema mama alimuuzaga maana ilikuwa kero kwa wenyeji hawaji home kwa raha na mtaa mzima wanamuita mama Bibi Max, na mm dada Max.

Nyingine nilikuwa Njombe olevel sasa likizo naenda kwa Uncle, na pale kwao kuna mbwa. Sasa shida mchana hakuna wenyeji mbwa anakuwa tu around home mpaka wenyewe warudi ndy wanamfunga, kwaiyo kwao mchana hamna hata mwenyeji anaenda kuwasalimia mpaka jioni hiyooo.
Me nilikuwa nikienda nasimama barabarani naitaaa Kunjiiiiiiiiiii basi anakuja nacheza naye lakini kwa taadhari, then naingia ndani. Wenyeji wakija utasikia jaman Kunji hajakung'ata me naona jau tu watu gani niliwapa taarifa kwamba nitaenda kesho na bado wanamuacha Kunji nje.
 
Kalio alizani linadondoka nahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…