Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Sometimes unaweza kufikiri labda jamaa mwenye mbwa kanileta makusudi ili nije kuwa kitoweo cha mbwa wake.

Taratiib utaanza kusikia kiushuzi kinatoka chenyew huku ukipumua kwa namna isiyokuwa ya kawaida yako, na wakati huo mbwa nao wanaangalia movement yako ili ukijichanganya tu wakuoneshe kazi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbwa ambaye haumi wenyeji ulio nao hawezi kukuuma wewe,kosa la kwanza ni kuanza wenge kama unachomoka mabawa mgongoni na kukimbia hovyo ukitengana na wenyeji wako,atakuuma.

saikolojia ya mbwa hubadilika anapoona mgeni,lakini mgeni salama ni yule aliye na mwenyeji wake au aliye mtulivu hata baada ya yeye kubweka.

kuna mpuuzi nilienda naye nilipopanga kulikuwa na geti na mbwa,nikamtahadhalisha mbwa haumi,awe mtulivu heee,kufungua tu geti mbwa akamsogelea jamaa akaanza kutuka ruka kama kuku kavaa mvuko mguuni[emoji23][emoji23],mpaka ananirukia mimi,yaani nilimind sijui alikuwa na majini mjinga yule.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenyeji wengine ukizongwa na mbwa wao wanacheka tu[emoji1787],

Mie mbwa akitaka kunizongo nakuwa mkali zaidi yake,tena kama kuna mawe nampiga,

Home nachekaga tu usiku watu wanavyokimbia kuogopa mbwa,wangejua mijibwa yenyewe inabweka tu wala haing'ati[emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee mbwaa hana urafiki, staki mie mazoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mshkaji wangu nilikua naendaga kwao na wana mbwa ila wanasema ni coco yani mchana hana madhara mpaka usiku na pale kwa mshkaji naendaga mara nyingi tu na mbwa huwa ananiona ila hanaga ile kumfuata mtu miguuni kama wanavyofanya mbwa wengine wakiona tu mgeni kaingia haoo wanamkimbilia


Huyu hakua na hizo mambo yani wewe ukiingia utamkuta kalala zake hana time na wageni,sasa siku moja usiku nilienda tena kwa mshkaji wangu tukawa tunacheki movie ndani baadae muda wa kuondoka tumetoka nje mbwa yupo kibarazani na pale nje kulikua na mabox mawili jamaa akaniambia nimsaidie kuingiza ndani yeye akabeba box moja akaingia ndani sasa ile nataka kubeba box mara simu yangu ikaita hapo mbwa ananichora tu,nilivomaliza kuongea na simu ndo nikabeba box niingize ndani yani ile nakaribia mlango tu naskia mbwa ananikimbilia anabweka akapeleka mdomo wake karibu na mguu dah nilikimbilia ndani mwili unasisimka yan ilibaki kidogo tu achomoe mnofu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee sio tu ningeisoma namba bali pengine leo hii ningekuwa naitwa marehem fulani, au wangeniachia ulemavu wa kudumu, maana hakuna mbwa mkali, hatari na mwenye nguvu kama pit bull. Huyo german shepherd mwenyewe akikutana na pit bull ujue siku hiyo hata wenye mbwa wao wenyewe watashindwa kuwaamua.

Na isitoshe walikuwa wakubwa last namba afu wameshiba haswa, wakitembea unasikia chini ti ti ti ti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbwa hafai, kuna nyumba moja iko jirani na tunakoishi kuna Mzungu alikuwa anaishi hapo na anafuga mbwa wakubwa tu. Na yana sauti kubwa yakibweka, na yeye huwa anatoa kauli hiyo hiyo. Sasa kuna siku nilikatiza hapo kwake mchana, na nilikua nimejisahau kama kuna mbwa wakali, sijui nilikua nawaza nini!! Ghafla mbwa wanaunguruma pembeni yangu, kugeuka kuangalia, naona mbwa wawili wako spidi wananifuata. Sikujiuliza mara mbili, nilifyatua mbio huku napiga mayowe. Na ndala niliziacha palepale getini kwake!! Ila nilishangaa kuona watu wananicheka, halafu wala hawana mpango na mimi. Baadaye nikasimama baada ya kuona kimya, kuja kufuatilia, kumbe wako ndani ya fence, zile za waya, kwa nje kumepandwa michongoma. Kwahiyo ukicheki kwa haraka, utaona michongoma tupu. Nikazirudia ndala zangu, nikasepa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbwa ukimjua jina hakupi shida.
Sisi kwetu ilikuwa lazima utambulishwe kwa mbwa, la siivyo hukai kwa raha.
Kwaiyo kama ni mgeni unaenda bandani kwa nje, anaitwa Max huyu ni mgeni atakuwa pamoja nasi siku zote la siovyo mgeni unacho. Sema mama alimuuzaga maana ilikuwa kero kwa wenyeji hawaji home kwa raha na mtaa mzima wanamuita mama Bibi Max, na mm dada Max.

Nyingine nilikuwa Njombe olevel sasa likizo naenda kwa Uncle, na pale kwao kuna mbwa. Sasa shida mchana hakuna wenyeji mbwa anakuwa tu around home mpaka wenyewe warudi ndy wanamfunga, kwaiyo kwao mchana hamna hata mwenyeji anaenda kuwasalimia mpaka jioni hiyooo.
Me nilikuwa nikienda nasimama barabarani naitaaa Kunjiiiiiiiiiii basi anakuja nacheza naye lakini kwa taadhari, then naingia ndani. Wenyeji wakija utasikia jaman Kunji hajakung'ata me naona jau tu watu gani niliwapa taarifa kwamba nitaenda kesho na bado wanamuacha Kunji nje.
Hongeraaaaaa sanaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la bata akiwa na beef na wewe huwa anaangalia sehem ya kukufanyia ushenzi.
Unaweza kuwa umetoka zako chooni kuoga huku umejifunga kitaulo chako, ghafla anatokea nyuma yako na kukurukia. Sasa wewe kwa mshtuko itabidi utoke nduki huku taulo likiwa limeanguka na mzigo ukiwa nje unaning'inia [emoji23][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnyama hana urafiki
Kuna bull dog wa jamaa akiwa kwake mtoto wa ndugu yake wa miezi 18 akawa anacheza nae
Ghafla alimng"ata kichwa hakuachia mpaka mtoto akakata roho huku akimzunzusha kama mwanasesere

Jina ujinga na mbwa kabisa nilishawahi kuumwa utotoni na mbwa wa jirani

Nikija kwako kama una mbwa na kuambia mfungie sehemu
Hivi ni sifa kumuacha mbwa akae na wageni? Ili iweje show-off ama
Maskini lol.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua na rafiki yangu tunatembea, ghafla kuna mwanamke mmoja akapiga ukelele, tukashtuka kuna nini? "nyokaa" "nyokaa", tukasogea pale, jamaa wakaanza kumpiga yule nyoka mawe, nyoka akaingia kwenye kimti kwa chini amejificha, basi akatokea jamaa mmoja hivi mlevi na mwenzie anasema "msimpige macheni, nyoka mimi haniumi, nyoka wananijua muacheni nimkamate", basi tukaona ngoja leo tuone miujiza.

Ila tukamtahadharisha yule mlevi asifanye mchezo ile ni hatari.

Jamaa akasogea pale nyoka ameacha mkia, jamaa akamkamata mkiani kamnyanyua hakuwa mkubwa sana, yule nyoka akawa kichwa kipo chini jamaa kashika mkiani, yule nyoka akageuza kichwa kuelekea kwenye mkono wa jamaa, jamaa si akaona anang'atwa, hajamrushia huku tulipokua, acha watu wasambae , asee yule jamaa tulimfukuzaje?

Kama mwizi, jamaa pombe iliisha alikuwa anakanyaga kibati hatukumkamata yule nyoka sijui alipotelea wapi...
Hio kauli yako imenikumbusha hio moment, hizo kauli siziamini kabisa...[emoji23][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom