Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Mm ukija kwangu watakuja mbwa wote kasoro mmoja huyo nisikudanganye habweki hana mwili wa kutisha ila akija mm mwenyewe najua mambo yameharibika
 
Nilishakwenda kwa rafiki yangu akanambia hanashida huyo tukazama ndani nikatoka baada ya msosi nikasema niende nikamcheki alooo akifoka sana na mm nikamletea unyang'au nikamshika domo lake nikaweka vibao viwili akili ikamkaa sawa jamaa anatoka mbwa katulia nampapasa mpka leo yule mbwa akiniona hana kelele😎
 
Nina mbwa kama wanne hivi nyumbani kwangu achilia mbali vitoto, nikikwambia usiogope usiniamini....wenzako wengi wamepitia misukosuko [emoji16]
 
View attachment 2460903
Mwanangu sana huyu anaitwa JUMBO hang’ati akiwa around na mwenyeji wake ila ukimpa respond ya kuattack ni hatari atakuweka chini ya ulinzi hadi afike mwenyeji wake..
Akhuu siruhusu kutembea na mbwa,wetu alinifuataga hadi mjini sina habari,wakati navuka barabara watu wakaniambia we dada mbwa huyo mweee,nilimtizama alijua nimekasirika,nilivyorudi nilimsema sana akanuna, hadi leo hanifuati
 
Kuna nyumba moja niliwashangaa sana, niliingia nimefika uwani mbwa akakurupuka huko akanifata huku anabweka, nikaamua kutumia ujanja wangu, nikainama chini kama naokota jiwe mbwa anashituka kidogo ila tena asogea, wao wananiangalia tu, mbwa nae alikuwa jasiri sana nikimtishia kama namponda anatulia kidogo afu anasogea, eti baadae ndio wanakuja kumshika wakati huo nimeshachoka balaa nawaza sijui akinifikia kabisa itakuwaje
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Akhuu siruhusu kutembea na mbwa,wetu alinifuataga hadi mjini sina habari,wakati navuka barabara watu wakaniambia we dada mbwa huyo mweee,nilimtizama alijua nimekasirika,nilivyorudi nilimsema sana akanuna, hadi leo hanifuati
Dah! Asa wewe nae ulipewa escorting yenye ulinzi maradufu ukamaindi ndio maana hata yeye nae alinuna kakuona hufai kuwa kiongozi kama mama sir100 hahahaa 😂🤣🤣
 
Dah! Asa wewe nae ulipewa escorting yenye ulinzi maradufu ukamaindi ndio maana hata yeye nae alinuna kakuona hufai kuwa kiongozi kama mama sir100 hahahaa [emoji23][emoji1787][emoji1787]
Yaani alinikera ujue,ingekuwaje kama angegongwa na gari,

Alikuwa anapenda kufuata balaa,kuna siku alimfuata dogo hadi shule akaingia darasani weeeeh imagine ni shule ya waarabu[emoji51]

Unaambiwa lilizuka balaa vitoto vya watu nusu vivunje miguu[emoji1787]
 
Back
Top Bottom