Huwenda hii ikawa ndio sababu ya kubadilishwa kwa noti za Tanzania

Njia rahisi ni moja tu. Kuachana na pesa za karatasi. Twende kwa pesa za kieleectronic. Hii ndo suluhu ya mambo yote. Watakao weka hela majumbani zitapotea. Watalazimika kutumia soft copy money. Ambapo serikali itaona fedha zake zote kwa kila mtu kila mahali.
 

Mtoa mada Yuko sahihi
 
Mleta uzi. Kwamba una ujuzi wa kupaka rangi uliusomea form four ni uongo, kwamba siku ya kwanza tu kwenda Kkoo ukagewa kazi na ukaaminiwa kwenda Masaki ni uongo.

Sasa tujadili hiki kingine.

Mtu aliyeficha noti zake ndani na anayeweka benki hawa wote hawana msaada katika kusaidia mzunguko wa pesa na ukuaji wa uchumi.

Katika dunia ya leo ambayo unaweza fungua akaunti ya benk online kwa nchi zingine si unafungua tu akaunt huko kwingine na kuhifadhi pesa badala ya kuchimba kama enzi za simulizi za Ben R. Mtobwa na Pesa Zako Zinanuka?

Watu wanaficha/ wanahifadhi dhahabu au dola ni ngumu kuficha/ kuhifadhi Tsh kwakua Tsh haipo steady and stable kama hivyo viwili.

Uchumi unakua stimulated na miradi mfano ya ujenzi ambayo pesa yake ikilipwa inaweza kumgusa kuanzia aliyesomea uhandisi hadi ambaye hajasoma ni anauza tu juisi za 500 kwa saidia fundi.

You can see kwamba ukiweka benki ni umeweka tu na hakuna kiasi kinakua injected kwenye mzunguko.
 
Kuna nchi ipo 100% kwenye elecronic currency?

Vulnerability to attacks ikoje? Mashambulizi mangapi yalitokea? Yaliyozuiwa successfully?
 
Ukibadilisha noti au usipobadili haibadilishi hali ya Uchumi.
Zaidi ya gharama tu.

Israeli hadi leo wanatumia Sarafu ya Shekeli pesa iliyokuwepo Enzi za Ibrahimu
Wanatakiwa waweke utaratibu wa fedha (noti) zinafikia ukomo wa matumizi (expire) muda fulani kama Dola za Marekani.
Toleo jipya zinarudi na alama, sura za viongozi vile vile kama za zamani. Kunachapishwa tarehe ya kutengenezwa tu (production date).
 
Madubwi yako mengi sana, salafu ya mia mbili iko kwenye madubwi
 
Kuna limit huonfoki nazo zitaingia bank mazeee oooh umafikiria wajinga....nadhani kuna kiwango kulaa nacho home ingawa bado sheria kupitishwa ila kipo....nadhani 20. To 100m
 
Hapo kuna vitu viwili:-

1.Noti za Tsh 20 , Tsh 200 ,Tsh 500
2.Noti za zamani Tsh 1000 , Tsh 2000 ,Tsh 5000 na Tsh 10000.

1.Noti za tsh 20 ,200 na 500,:- Hizi noti kwani zipo kwenye mzunguko? Mbona hazitumiki kitambo? Mara ya mwisho kuiona noti ya Tsh 20 au 200 ni kama 1988 au 89 na mara ya mwisho kuitumia noti ya mia 5 ni kama miaka mitatu iliyopita.

2.Noti za zamani za elfu 2 ,elfu 5 ,elfu 1 na 10:- Nakumbuka kulikuwa na version mbili za hizo noti kwenye mzunguko ,zilikuwa zinatofautiana size ,kuna kubwa na ndogo ,kubwa ndiyo za zamani na hazipo kwenye mzunguko kwa muda mrefu sana ,sikumbuki hata ni lini nimeziona hizo noti kubwa au kuzitumia.

Swali mbona ikikaribia uchaguzi mkuu ndiyo mambo ya kubadilisha noti zinaanza? Kuna siri gani hapo?
 
maamuzi gani nawewe..?
hivi unajua ni biashara ngapi za magendo Africa zinaendelea..?
utakatishaji wa fedha kiasi gani unafanyika unajua..? hivi unaelewa ktk mabara yote africa ndio bara rahisi kufanya ubadhirifu,unaelewa hilo..?

unafahamu kuna biashara haramu zinafanyika nchi nyengine huko pesa wanakuja kutakatisha huku, ma bank yanatumika sana ktk kufanya hivyo!

shida hamfatilii mnabisha tu kama watu msiokuwa na akili,sidhani hata kama unaelewa dhahabu ni nini wewe!!!!!
dhahabu haiharibiki,thamani yake ipo stable na pia ni rahisi kuhifadhi kuliko fedha,hata wakitangaza wanabadili fedha nikiwa na dhahabu zangu mi sitishiki maana dhahabu hawawezi kuibadili.. badirisha fikra hizo babu!
 
Kwamba Huyo Mu Asia kaficha mamilioni ya Noti za Zamani ivo ambazo hata mtaani hazipo.
Maana noti zinazozungumziwa ni zile za zamani sio hizi tunazotumia sasa
 
Fedha nyingi nilizoshika kwa miaka ya karibuni zina sahihi ya Mpango na Ndulu au Florence. Maana yake fedha za matokeo ya Mkapa na Daudi balali ziliisha kwenye mzubguko siku nyingi mno. Labda 100, 200, 50, 20 na sh 10. Kuna kitu kingine nyuma ya hii.
 
Tactical game hii mzee, huwezi kusubmit mapesa yote hayo benki kuyabadilisha bila kushtua watu.. hili gemu linafilisi sana matajri wanaoficha hela ndani
 
Hakuna mfanyabiashara mjinga anayeficha fedha ya madafu ndani kuogopa kutaifishwa kipindi hiki.
Watu wenye akili kwa sasa 'wanaficha' fedha zao kwa style hii.
1. Kununua dola ya marekani
2. Kununua dhahabu
3. Kununua dhamana za serikali na hati fungani.

Kwa hiyo style mtu anaweza kuficha hata Trilion moja, na kila siku akaongeza thamani ya faida ya zaidi ya 1milioni.
 
Hela zinazotumika sa hivi hazihusiani hapo na Kusanyo hilo na ndo maana wametoa muda mfupi sana wa kuzikusanya... Ni ngumu sana Nchi zilizokuwa Africa eti urudishe fedha zote kwa miezi mi tatu tuu.

Hapo zinaondolewa zile noti za zamani ukiacha ambazo ziko kwenye mzunguko wa sa hivi. Na nyongeza pia hata noti za mia tano zilizotoka 2010.

Shilingi 50 na 200 na 100 na 500 za sarafu hazihusiani hapo kwani hizi zipo za mwaka 1994 au 1995 nyingi ila wameongelea noti ndo zinakusanywa..

Tangazo liko wazi kabisa ila naona watu wemefikiria mengi mara kwasababu ya uchaguzi mara kwasababu ya wanaoficha hela...

Wakati ni kama naona lina wapa nafasi walokosa matumizi wa hizo hela za zaman sa hivi zinawapa nafasi kwenda kubadilishiwa(ukute ni njia ya kuingiza fedha ambazo watu walikosa pa kuzitumia au pakupeleka)
Yaani naona wameends kuhalalisha kitu ambacho watu walishaamini hakina matumizi tena
 
Kuna Sura Tunataka tuiweke kwenye buku na Rungu la Pembe kwenye Teni,,kama hamtaki hamieni Lebanon.
 
Swali la nyongeza!!
Hivi mtu akienda Benki kubadilisha hizo fedha za zamani mfano elfu 10 ya miaka hiyo enzi ya Mzee Mwinyi anapewa elfu 10 yenye thamani ya sasa?

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
Kuna ukomo wa muda wa kubadilisha fedha za zamani. Muda ukiisha haipokelewi benki yeyote wala kule BOT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…