Huwenda hii ikawa ndio sababu ya kubadilishwa kwa noti za Tanzania

Huwenda hii ikawa ndio sababu ya kubadilishwa kwa noti za Tanzania

Inawezekana wapo wanaoficha hela na wa Tanzania walivyo sijui kama watazibadilisha.

Notisi ni fupi sana, walau wangetoa mwaka mmoja ili hela iondoke kidogo kidogo kwenye mzunguko.

Nakumbuka miaka ile mzee wangu kitu kilichokuwa kinamfanya aende mjini ni kubadili hela huku akiwa amevaa nguo nyingi nyingi na kusunda noti kibindoni.

Ukweli noti nyingine zimechoka but naamini lengo ni kuweka sura zao.
IMG-20241027-WA0015.jpg
 
U
Kwa wandewa wenyewe hii game inachezwa kimya kimya. Na sidhani kwa hali ya sasa kuna mhindi mjinga anaweka hela ndani. Mhindi ananunua dollars kisha anafungua account ya dola nje ya nchi. Nyie hata mfanyeje, mnazipata wapi hela zake?
UKiona mkuu mpaka serikali inabadili hela ghafla tu ujue kuna watu wanatargetiwa na imetoa viashiria hivyo. We ungekua mtu wa system ungrkuwa ushajua nani anaenda kulia mana mpaka muda huu huyo mtu atakuwa na jicho nyanya
 
Mwaka fulani nilipomaliza chuo kikuu nikiwa bado kupata ajira rasmi niliamua kutafuta kazi nje ya kile nilichosomea chuoni. Kwani nilipokuwa o-level shule ya ufundi nilisomea ufundi wa kupaka rangi, hivyo niliamua kutafuta kazi hiyo ili niweze kusurvive ndani ya jiji la DSM huku nikiendelea kutafuta kazi ya kile nilichosomea chuo kikuu.

Ndipo nilipopata kazi ya kupaka rangi kwenye ghorofa moja kule Kariakoo, niliifanya kazi ile vizuri na kumpendeza foreman aliyekuwa akisimamia kazi ile ndipo akanichukua mimi na mwenzangu na kunipeleka kwenye jumba moja la kifahari huko Mikocheni kwa ajili ya kufanya kazi ya sceaming na kupaka rangi.

Nilichokikuta huko ndicho kilichonifanya niandike uzi huu, kwani nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na wafanyabiashara wenye asili ya ki-asia. Hawa watu huwa targeted sana na wanasiasa hasa kwakuwa humiliki viwango vikubwa vya fedha walivyowekeza kwenye benki zetu za biashara. Kuna mbinu huitumia ili kukwepa vikwazo hivyo haswa inapokaribia kipindi cha uchaguzi mkuu.

Kipindi cha uchaguzi ni kipindi ambacho serikali moja huondoka na serikali nyingine kuingia madarakani, ni katika kipindi hicho kwamba fedha zao huwa mashakani. Fedha zao zilizopo kwenye mabenki huweza kutaifishwa ama kuzuiliwa kwa sababu kadhaa, hivyo huamua kufanya kile nilicho kishuhudia. Kuchimba mashimo mithili ya mahandaki ndani ya nyumba zao, kwenye sakafu au ukutani au hata darini hutengeneza masanduku ya siri ambayo ni vigumu sana kuyatambua.

Ndani ya mashimo hayo ndipo hutumia kuhifadhi fedha hizo, hutoa fedha zao nyingi kutoka kwenye mzunguko na kuzichimbia kwenye mahandaki ya siri yaliyoko kwenye majumba yao, lengo kuu likiwa kuhifadhi fedha hizo kwa usalama wa mitaji yao ya kibiashara, na huja kuzitoa na kuzirudisha tena kwenye mzunguko pale serikali mpya itakapo simikwa na wakijihakikishia kuwa maslahi yao yatalindwa.

Kwahivyo kitendo hicho ndicho kinachofanya uchumi wa nchi kudorora hasa inapokaribia kipindi cha uchaguzi kwani fedha nyingi zinakuwa zimeondolewa kwenye mzunguko na pia wafanyabiashara hujiepusha kufanya uwekezaji mkubwa ama kutumia pesa nyingi kwenye biashara zao kitendo kinachoweza kusababisha upungufu wa fedha kwenye mzunguko wa kiuchumi.

Kwa serikali kutangaza ulazima wa kubadilisha fedha kwa kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi mkuu, kitawalazimisha wafanyabiashara wote haswa wale walioficha fedha kwenye mahandaki kuzitoa na kuzirudisha kwenye mzunguko kwani wasipo fanya hivyo wanaweza kupoteza fedha zao moja kwa moja, lakini kwa serikali itakuwa ni faida kwa kurudisha fedha zilizofichwa kwenye mzunguko wa kawaida hivyo kuhuisha uchumi wa nchi.

Swali la kujiuliza ni kwamba tutaendelea na utaratibu huu mpaka lini wa kubadilisha noti kila tunapo amua kufanya hivyo? Vipi kwa mataifa yaliyo endelea yamewezaje kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha na kuadimika kwa fedha zao bila ya kutumia mbinu hii ya kubadilisha fedha ili kuzitoa fedha zilizofichwa kurudi tena kwenye mzunguko? Tuige kwa mataifa hayo ili kuepuka kubadilisha noti zetu mara kwa mara, tutambue kwamba noti na sarafu ni utambulisho wa kitaifa na sidhani kama ni jambo jema kubadilisha utambulisho huo kila mara.

Nawasilisha.
View attachment 3136171
Hujalielewa tangazo la BOT
 
Ni kwamba watu hawasomi tangazo vizuri na kukurupuka au mimi ndio sijaelewa!!

Hapa wanaongelea noti za zamani kabisa na ile mia tano ya noti iliyobadilishwa kua ya sarafu.

Wewe unaongelea noti mpya kitu ambacho hakijaongelewa hapo 🤔🤔

Hata hivyo ukienda unabadilishiwa hapo hapo, unawapa za zamani unachukua zinazotumika sasa. Au unahisi wanakulazimisha kuweka bank ??
Yaani watu wanakurupuka sana.
 
  • Thanks
Reactions: I M
maamuzi gani nawewe..?
hivi unajua ni biashara ngapi za magendo Africa zinaendelea..?
utakatishaji wa fedha kiasi gani unafanyika unajua..? hivi unaelewa ktk mabara yote africa ndio bara rahisi kufanya ubadhirifu,unaelewa hilo..?

unafahamu kuna biashara haramu zinafanyika nchi nyengine huko pesa wanakuja kutakatisha huku, ma bank yanatumika sana ktk kufanya hivyo!

shida hamfatilii mnabisha tu kama watu msiokuwa na akili,sidhani hata kama unaelewa dhahabu ni nini wewe!!!!!
dhahabu haiharibiki,thamani yake ipo stable na pia ni rahisi kuhifadhi kuliko fedha,hata wakitangaza wanabadili fedha nikiwa na dhahabu zangu mi sitishiki maana dhahabu hawawezi kuibadili.. badirisha fikra hizo babu!
Kwanza,Weka ushahidi wa unachokisema ukionesha kama bara la Afrika laongoza....
Weka takwimu na si porojo...
 
Hakuna mfanyabiashara mjinga anayeficha fedha ya madafu ndani kuogopa kutaifishwa kipindi hiki.
Watu wenye akili kwa sasa 'wanaficha' fedha zao kwa style hii.
1. Kununua dola ya marekani
2. Kununua dhahabu
3. Kununua dhamana za serikali na hati fungani.

Kwa hiyo style mtu anaweza kuficha hata Trilion moja, na kila siku akaongeza thamani ya faida ya zaidi ya 1milioni.
So unaenda kununua dhamana ya serikali na unadhani upo safe...?
Yani,unajiingiza kwenye register ya Benki kuu,ambapo mwanzo uliogopa kupereka pesa Benki ya Kawaida...

Yani,watu hizi mbinu zenu za kitoto,unafkiri ni ngumu kugundulika....🤣🤣🤣🤣
 
Kasongo yeyee..mombali nangaa,, kasongo mbona wewooh,,songali nangaa,,wo- yeyee,, kasongo mbona weweeeh,,mbona wewoooooh
 
Sio hela hizi zinazobadilishwa ni zile za zamanii mbona hamuelewi
Za zamani zilishatolewa tangazo kwamba hazitakuwa halali tena kwa kubadilishwa baada ya yarehe husika ya miaka hiyo. Hapa inaonekana kuna mtu alificha matrillion na zikabdioishwa huku yeye akishindwa kubadilisha hizo pesa haramu. Kwahiyo sasa wanazihalalisha ili kuziingiza kwenye mzunguko na kuketa inflation kwa kuwachapishia pesa mpya
 
Za zamani zilishatolewa tangazo kwamba hazitakuwa halali tena kwa kubadilishwa baada ya yarehe husika ya miaka hiyo. Hapa inaonekana kuna mtu alificha matrillion na zikabdioishwa huku yeye akishindwa kubadilisha hizo pesa haramu. Kwahiyo sasa wanazihalalisha ili kuziingiza kwenye mzunguko na kuketa inflation kwa kuwachapishia pesa mpya

Umewaza kama mimi. Hivi Kama Elfu kumi ya zamani au hata elfu tano au mbili au moja wapi imetumika au wapi watu walikuwa wanaitumia. Maana zilishaondoka mtaani kabisa.. Hata mtu ukimkuta nayo ameibakisha kama urembo . Alafu Eti Tangazo lina kuja kuzihalalisha tena hizo fedha.

Bora wangesema mia tano peks yake za noti ambazo zimetoka pamoja na hizi hizi ambazo tuko nazo katika matumizi hila zikatolewa kulipokuja sarafu..

Kuna Harufu ya utakatishaji fedha hapa
 
Inawezekana wapo wanaoficha hela na wa Tanzania walivyo sijui kama watazibadilisha.

Notisi ni fupi sana, walau wangetoa mwaka mmoja ili hela iondoke kidogo kidogo kwenye mzunguko.

Nakumbuka miaka ile mzee wangu kitu kilichokuwa kinamfanya aende mjini ni kubadili hela huku akiwa amevaa nguo nyingi nyingi na kusunda noti kibindoni.

Ukweli noti nyingine zimechoka but naamini lengo ni kuweka sura zao.
Kabisa. Nahisi kama wewe. Wanataka kufuta HISTORIA ya waasisi wa Taifa na kuweka sura zao. Ni mtazamo na malengo ya kisiasa zaidi kuliko malengo na faida za kiuchumi.
 
Mleta uzi. Kwamba una ujuzi wa kupaka rangi uliusomea form four ni uongo, kwamba siku ya kwanza tu kwenda Kkoo ukagewa kazi na ukaaminiwa kwenda Masaki ni uongo.

Sasa tujadili hiki kingine.

Mtu aliyeficha noti zake ndani na anayeweka benki hawa wote hawana msaada katika kusaidia mzunguko wa pesa na ukuaji wa uchumi.

Katika dunia ya leo ambayo unaweza fungua akaunti ya benk online kwa nchi zingine si unafungua tu akaunt huko kwingine na kuhifadhi pesa badala ya kuchimba kama enzi za simulizi za Ben R. Mtobwa na Pesa Zako Zinanuka?

Watu wanaficha/ wanahifadhi dhahabu au dola ni ngumu kuficha/ kuhifadhi Tsh kwakua Tsh haipo steady and stable kama hivyo viwili.

Uchumi unakua stimulated na miradi mfano ya ujenzi ambayo pesa yake ikilipwa inaweza kumgusa kuanzia aliyesomea uhandisi hadi ambaye hajasoma ni anauza tu juisi za 500 kwa saidia fundi.

You can see kwamba ukiweka benki ni umeweka tu na hakuna kiasi kinakua injected kwenye mzunguko.
Hujaelewa nini? O-level alikuwa technical school akajifunza kupaka rangi! Kipi cha ajabu!? Unashangaa alivyoaminiwa kwa kufanya KAZI nzuri Kariakoo?!
 
Hujaelewa nini? O-level alikuwa technical school akajifunza kupaka rangi! Kipi cha ajabu!? Unashangaa alivyoaminiwa kwa kufanya KAZI nzuri Kariakoo?!
Tafuta uone mwenye uzi alivyojibu
 
Mbna pesa BOT wanazoziongelea tayari zilishapotea mtaAni, In today's world people keep their money in things like crypto and stable fiat currencies not Tanzania shillings.
#No malice to anybody
 
Back
Top Bottom