Huwenda hii ikawa ndio sababu ya kubadilishwa kwa noti za Tanzania

Pesa zilizotajwa sijui kama wewe unazo au umewahi kuzitumia toka mwaka huu uanze!
Ningekuwa mimi Post hii ningeiondoa.
 

Ni kwamba watu hawasomi tangazo vizuri na kukurupuka au mimi ndio sijaelewa!!

Hapa wanaongelea noti za zamani kabisa na ile mia tano ya noti iliyobadilishwa kua ya sarafu.

Wewe unaongelea noti mpya kitu ambacho hakijaongelewa hapo 🤔🤔

Hata hivyo ukienda unabadilishiwa hapo hapo, unawapa za zamani unachukua zinazotumika sasa. Au unahisi wanakulazimisha kuweka bank ??
 
Tactical game hii mzee, huwezi kusubmit mapesa yote hayo benki kuyabadilisha bila kushtua watu.. hili gemu linafilisi sana matajri wanaoficha hela ndani
Sasa mtu afiche fedha ya Tz ndani ili iweje? Pesa ya Tz haina thamani inayokuwa, na haiwezi kutumika kimataifa kufanya manunuzi.
Kama mimi nimeficha ndani pesa chafu zaidi ya 100bilioni, nikiamua kuzitoa sihitaji kwenda kuzibadilisha benki, nitaziingiza kwenye mzungumko ili kuzitakatisha jambo ambalo ni suala la wiki moja tu.
 
we huumwi kweli watu wananunua dhahabu wanaficha mzigo wa fedha hawataki sahivi
Tajiri yeyote lazima awe na mzigo wa fedha wa kutosha wa dola na sarafu za nchi, kikinuka dhahabu haziwezi kukusaidia katika kipindi cha muda mfupi(in short run)
 
Upo ndani ya uzi.Inawezekana.
 
Tajiri yeyote lazima awe na mzigo wa fedha wa kutosha wa dola na sarafu za nchi, kikinuka dhahabu haziwezi kukusaidia katika kipindi cha muda mfupi(in short run)
pole ndugu,dhahabu inauzika popote maana kama ni cash ukiwa na million 50 ama 100 huwezi kushindwa kwenda popote! hivi ukae na billions za kitanzania unajua ni mzigo wa kiasi gani...?
 
Kabla ya kuzichimbia mahali wanazibadili katika dola au pound. Wao sio wajinga. Au wanunue dhahabu na kuhifadhi.
 
Option hapo ni kudevelop cashless economy , suala la ukwepaji kodi ,rushwa na uhuni wa kila aina itakuwa rahisi kuucontrol ,lakini sasa nikiangalia kwa aina ya majitu yanayoongoza hii nchi na mifumo ya kishenzi iliyotengenezwa na ccm , huu mfumo wa cashless itakuwa ni fimbo ya kukandamiza watu na badala ya kutumika kama solution ya hayo matatizo yanayotukabili kama taifa
 
Na uzuri wa jambo hili (kubadilisha) linafanyika kwenye bank zote na binafsi.
 
Hujui kitu. Kilichotokea ni kuwa hizo hela hazikuwahi kuondolewa kwenye mizunguko ila as of now hazitumiki kabisa. Niambie mara ya mwisho ulitumia wapi note ya shs 20??? Au ile ya shs 500??? So kinachofanyika hakihusiano kabisa na mleta maada
 
Serikali pumbavu ya ccm ifute sifuri moja kwenye pesa
 
Huwezi kwenda kubadilisha bil moja ukarudi nayo nyumbani mkuu unaijua bank vizuri
 
Haikuwa siku ya kwanza nilifanya kwa muda fulani ila hapo nimeamua kukatisha tu maelezo yasiwe marefu, of course mwanzo iliniwia vigumu kuadopt ila nilijitahidi mpaka nikaweza, niliaminiwa kwakuwa nilikuwa na fundi mwenzangu ambaye ni competent alikuwa akinibackup na kufuta makosa yangu ya kiufundi. Kwenye kutafuta ugali lazima ujitume.
 
Huwezi kwenda kubadilisha bil moja ukarudi nayo nyumbani mkuu unaijua bank vizuri
I'm x banker najua bank banking kuliko wewe. Unaifukua unapeleka bank unaweka amana. Then unatoa kidogo kidogo tofauti yake na nilichosema ni nini?
 
Tactical game hii mzee, huwezi kusubmit mapesa yote hayo benki kuyabadilisha bila kushtua watu.. hili gemu linafilisi sana matajri wanaoficha hela ndani
Kwa wandewa wenyewe hii game inachezwa kimya kimya. Na sidhani kwa hali ya sasa kuna mhindi mjinga anaweka hela ndani. Mhindi ananunua dollars kisha anafungua account ya dola nje ya nchi. Nyie hata mfanyeje, mnazipata wapi hela zake?
 
Kuna limit huonfoki nazo zitaingia bank mazeee oooh umafikiria wajinga....nadhani kuna kiwango kulaa nacho home ingawa bado sheria kupitishwa ila kipo....nadhani 20. To 100m
Unatoa kidogo kidogo
 
Hiyo inaonekana kama vile kuna dili fulani hivi. Madili ya namna hiyo yalishawahi kutokea nchini Nigeria na nchini Liberia.

Mathalani, nchini Liberia ilitokea kwamba baadhi ya Wanasiasa Watawala wa nchi hiyo ambao ni Wahalifu (Mafisadi) walishirikiana na Watendaji wa Benki Kuu ya nchi hiyo walitoa zabuni ya kuchapisha Noti Mpya za fedha za nchi hiyo kwa Kampuni Moja huko Ulaya. Baada ya noti hizo kuchapishwa kutoka kiwandani kwa Mzabuni, zilisafirishwa kwenye ma-container kupitia baharini hadi bandari ya Mji Mkuu wa nchi hiyo Monrovia. Hao Watawala wapiga madili walifanikiwa kuiba Jumla ya Makontena manne (4) yaliyobeba Noti Mpya, makontena hayo yenye fedha (Noti mpya) yaliibiwa hapo hapo bandarini na kisha kupotelea Mahali kusikojulikana na Kamwe hayakuwahi kupatikana tena hadi leo.
Watawala wa nchi za Afrika na madili ya kifisadi ni 'damu damu' kama samaki na maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…