Huwezi kuchukua nchi bila SYSTEM kuwa upande wako

Kwahiyo kwa maana nyingine unakiri Kwangu kuwa kumbe ulikuwa huna Busara ndiyo maana ukakosea vile? Waswahili bhana!
Aliyefanya busara ni mwingine siyo wewe hopeless.
 
System inakuwa upande wako ukiisha chukua nchi siyo kabla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyefanya busara ni mwingine siyo wewe hopeless.

Hili Jina la Kiislamu la Marehemu Imran Kombe ulilitoa wapi Ndugu? Siku zingine uachege kuwa na Kiherere ona ulivyoumbuka.
 
Kitu cha kwanza kuwapalilia njia wapinzani nikuhakikisha wanapata majority bungeni

Ili wawe na uwezo wa akidi kupush mambo wanayoyataka kwa votes bungeni hata serikali itakuwa na adabu kwa bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili Jina la Kiislamu la Marehemu Imran Kombe ulilitoa wapi Ndugu? Siku zingine uachege kuwa na Kiherere ona ulivyoumbuka.
Sasa kukosea jina ndo kuumbuka? Una akili ndogo Mbona?
 
Sasa kukosea jina ndo kuumbuka? Una akili ndogo Mbona?

Kama hukuwa tu na Akili ya kuweza Kujiridhisha vyema juu ya Jina la Marehemu Kombe utakuwa na Akili za Kujibizana nami?
 
Kama hukuwa na Akili ya kuweza Kujiridhisha vyema juu ya Jina la Marehemu Imran Kombe utakuwa na Akili za Kujibizana nami?
I got the last name right. Sidhani kama una akili za kukutosha. Siwezi kuwa na muda mchafu. Endelea na shughuli yako.
 
Kitu cha kwanza kuwapalilia njia wapinzani nikuhakikisha wanapata majority bungeni

Ili wawe na uwezo wa akidi kupush mambo wanayoyataka kwa votes bungeni hata serikali itakuwa na adabu kwa bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app

..Ni wazo zuri.

..kusiwepo na chama chenye kuweza kupitisha mswada bungeni bila kushirikiana na chama kingine.
 
Hii ni kwa democratic state mkuu sio hapa Tz, hata ukiwa na sifa zote hizo bado hutapewa uraisi kama hujajipanga vizuri na system. Zanzibar 2015 hayo uliyoyasema yote upinzani ulikuwa nayo lakini mwisho wa siku TISS walimteka Jecha na kumlazimisha kufuta uchaguzi jambo halijawi kutokea duniani chama tawala kudai uchaguzi haukuwa huru.
 

..hiyo inaweza kutokea kwa kaeneo kadogo kama Zanzibar.

..Tanganyika ni li nchi likubwa huwezi kulidhibiti kama Zanzibar.
 
Alibebwa na lubuva
Ndio system yenyewe sasa kama chadema wanatukana serikali,mahakana,tume ,spika unategemea nini?? Spika Wa bunge bwege,haya mahakama mabwege,vyombo vya dola mabwege,tume mabwege hivi kwa misimamo hiyo ulitarajia chadema ishinde? Na una matarajio itakuja kushinda ikiendelea na hiyo misimamo?
 
Hawawezi kua ni wananchi tu bwana,lazima ufikiri kwa kina. Jeshi likiwa upande wa uongozi na likanyanyuka kisawa sawa kudhibiti raia hakuna atakaye kohoa
JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
We ni kiazi kabisa, security services ya nchi yoyote hutii rais yeyote aliyechaguliwa na huanza kutekeleza majukumu yao kulingana na mtazamo wa huyo rais mpya na kumshauri pale wanapoona kuna shida. Angalia sakata la ESCROW lilivyokuwa handled na wana usalama wetu, japo lilikuwa bomu lakini walihakikisha linapita salama. Tumia akili na kama hunazo kaa kimya
 
..Ni wazo zuri.

..kusiwepo na chama chenye kuweza kupitisha mswada bungeni bila kushirikiana na chama kingine.
2015 CHADEMA walifanya Kosa kubwa kuelekeza nguvu kubwa kwenye urais badala ya bunge.

Walitakiwa waweke nguvu kubwa sana kwenye bunge ili wavunje hiyo majority ya ccm bungeni nafasi ya kufanya hivyo walikuwa nayo kubwa sana.

Ukiangalia majimbo waliyoyapoteza kizembe huku wakiwa wameshapata kura zaidi ya 50% yalikuwa mengi sana lakini walinyang'anywa kizembe sana.

Kama wangekuwa na nguvu ya akidi bungeni sheria mbovu zote wangeweza kubadilisha na wangeweza kupush agenda zao zikaweza kupita bungeni.

Lakini kilicho wazi zaidi ni kwamba walitoka kwenye uchaguzi mkuu wakiwa exhausted sana na walipopoteza tena wakawa hawana plan B namna gani wataendelea kunevigate the tide mapigo ya ccm na dola yakawafrustrate wakashindwa kupambana na kuanza kulia na kulalamika this was an expression of defeat which ccm received it with it's all hands.

Mwanzoni uwanja wa kuchezea ulikuwa na mbigili tu sasa ccm wameamua kuumwagia misumari kabisa ni ngumu sana CHADEMA sasa hivi kupambana kwenye uwanja huu though bado wanaback up kubwa ya wananchi kuliko aliyonayo ccm.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapinzani hawana adabu, 24/7 wanalindwa wasiuawe na watu wa nje ila wao hawana shukrani.
 
..hiyo inaweza kutokea kwa kaeneo kadogo kama Zanzibar.

..Tanganyika ni li nchi likubwa huwezi kulidhibiti kama Zanzibar.
Madam ccm ikiendelea kutawala Tanzania bara Zanzibar hakuna chama kingine kitakachoweza kupata urais hata kama kitashinda asilimia 100 ya kura zote.

ccm wanaweza kuwa tayari kutumia nguvu ya ziada (nadhani umenielewa) kuhakikisha inabaki kwenye top leadership Zanzibar no wonder 2015 walipora huo ambayo wamekuwa wakifanya hivyo kila uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaweza uovu ukizidi wakaiamsha jamii,Jamii kwa pamoja mfano ifikie 80% waikatae ccm,hata tume iwe inatoka mbinguni au kuzimu itaachia tu.Msingi ni wananchi na sio tume.Wananchi siku wakiichoka ccm hata polisi hawana uwezo wa kuisaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…