Siyo siri tena, nimebaini mchezo mchafu unaendelea kwa lengo la kumchafua Hayati Dkt Maguli.
Taratibu wanafiki wanaanza kujionesha mmmoja mmoja, wanahaha kama mtu aliyekula nyama ya binadamu. Mpaka kufikia June wanafiki wote watajulikana...
By
Malisa Godlisten
Mmesikia serikali ya wanyonge? Serikali takatifu ya shujaa wa Afrika, tuliyeambiwa amefuta ufisadi? Ngoja nikutajie machache;
Ujenzi wa SGR umesababisha hasara ya 3.5Bil kwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni wasiokua na vibali.
Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).
Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi.
Wasafi walipewa 140M, TBC 201M na Clouds 629M kutangaza tamasha la Urithi Festival. Lakini hakuna mkataba wala risiti yoyote ya kujustify malipo hayo.
18Bil zilizokusanywa ktk wilaya 135 hazikufika serikalini. Yani zilikusanywa lakini wajanja wakalala nazo mbele.
3.9Bil zilitolewa kukarabati ndege ya ATCL iliyopaki tangu mwaka 2015, lakini hela imeliwa na ndege haijakarabatibwa. Yani watu walitafuna milioni 3,900 halafu hawakupaka hata rangi.Hayo ni baadhi tu ya "madudu" ya serikali takatifu ya mwendazake. Sijaongelea HESLB, TANAPA, TANROADS, SGR, Stligler's gorge, Stand ya Magufuli. Huko kuna madudu ya kutisha.
Lakini tuliaminishwa serikali ya mwendazake haikua na doa. Watu waliokosoa waliitwa vibaraka. Serikali takatifu haikutaka kunyooshewa kidole.
Tujifunze kutofautisha mtu msafi na anayeficha uchafu. Mwendazake hakua msafi bali alijua kuficha uchafu. Ndio maana akaminya uhuru wa habari. Hatukusikia skendo kama za Escrow tukadhani serikali yake ni safi, kumbe kuna skendo kubwa zaidi ya Escrow lakini zimefichwa uvunguni.Ndio maana nasema afadhali JK aliruhusu media ziwe huru. Skendo za Richmond, EPA, Escrow aliacha wananchi wajue. Lakini mwendazake alifunika skendo zisifike kwa wananchi.
Ndio maana watu wamemtania CAG atoe pia ripoti aliyopanga kumpa mwendazake, maana angekua hai asingethubutu kusema ATCL imepata hasara ya mabilioni, au SGR imeleta hasara, au mradi wa Stigler's umejaa madudu. Angeficha kwa sababu ndivyo mwendazake alivyopenda.
Tunahitaji viongozi wasafi, sio wanaojua kuficha uchafu.!