RRONDO labda kama umekulia ulaya utabisha,nikiwa mdogo tukicheza hizi mechi za mitaani tulikuwa tunaenda kwa mganga kuroga ili tushinde mechi,sometimes tunafungwa tunajipa moyo kuwa tulikiuka masharti.
Mwaka 2001 nikiomba visa ya kwenda USA agent wa safari yangu alinipeleka mwananyamala kwa babu mpemba kuoshwa nikakataa,akaniambia nikikosa visa nisimlaumu.nikaenda na visa nikapata.
Nilifanya kazi ofisi moja kuna jamaa kazi yake kupeleka staff wrnzetu kwa mganga ili wapande vyeo.
Kariakoo wakinga ni noma,
Kisutu,kitumbini wahindi familia zao hukosi zezeta,
Madereva wa STK ni noma kwa kupuliza.
Timu za mpira zote zina mganga wake,
Mabasi ya mikoani yanafanyiwa kafara hatari.
WAnaokwenda likizo december huko kaskazini wanaenda kufanya ushirikina ambao ni modern,mbuzi lazima achinjwe.
Mahakamani kwenye kesi kuna ushirikina hatari.
Mimi binafsi siendi kwa mganga na mtumainia Mungu ila waafrica sisi sio watu wazuri