Hivi mtu anaweza kufanya biashara na kuwa tajiri maeneo kama kariakoo bila uchawi?
Unaweza, Cha kwanza tambua Hilo Eneo kama Hilo biashara zinamilikiwa na mifumo ya kiimani. Biashara inafanyiwa mahesabu kiimani na hapo unakuwa na utekelezaji kimwili.
Mifumo ya nguvu za Giza ikitawala utaona watu wanaofanya huo ushirikina wanafuata masharti Yao yote kutoka kwenye huo ushirikina , hata akiambiwa sharti la kutokula Nyama maishani yake hatakula au asipate mtoto maishani yake atajitoa sadaka kwa hayo maguvu ya Giza. Maana yake hayo maguvu ya kiza yamempa nguvu ya kufuata huo utumwa na anaona ni fahari .
Kwanini tusitumie nguvu kubwa kufanya hayo katika upande wa Mungu????( Mungu atusaidie na kutupa nguvu ya kuyafuata maagizo yake). Ili uweze kufanya biashara maeneo kama hayo bila ushirikina fanya ya fuatayo:
1. Mshirikishe mungu Hilo wazo lako la kutaka uweke biashara Eneo Hilo kabla ya kwenda( ukienda tu kichwa kichwa kabla ya Kibali utapigwa tu).
A) mungu anaweza akakupa Kibali hapo hapo.. tii sauti yake na fanya hiyo biashara.
B). Mungu anaweza asikupe Kibali Cha kufungua biashara hayo maeneo kabisa badala yake akakuonyesha sehemu nyingine ambayo kwa maono yako unaweza ukaona hapana biashara kabisa ukilinganisha na unavyo ona. Usiende kufungua tu hata kama unaona Kibali hujapata kutoka kwake unaenda ukitengemea atakusaidia( mungu hatafungua hiyo biashara na wewe ,kama amakunyima hicho Kibali. Utafungua biashara bila nguvu ya mungu Wala nguvu ya Giza) kitakachotokea ni kufeli tu. Tena utayakasirisha mashetani ya hapo yatakupiga mno mno. Utakuwa sawa na kupambana majambazi wenye silaha za moto kwa ngumi.
C) anaweza kukupa Kibali lakini kinahitaji mda ,akuandae na ujiamdae kikamirifu. Subiri na kuwa mvumilifu, unaweza ukaanzia kwingine na mda ukifika utafanya tu.
2. Baada ya kupata Kibali , fanya biashara kwa mapenzi ya Mungu, kumwabudu, sadaka, Imani, kusaidia wahitaji bila kusahau Zaka.
3. Usiendekeze Uovu wewe au biashara yako.. biashara inyooke kama Rula, siwe na udanganyifu ,uongo ongo ,upigaji . Hapa ndiyo patamu na unaweza ukaona ,pamoja na kufanya mengine utaishia kupigwa tu kibiashara sababu 1: nguvu kubwa( Mungu) anayekupa hizo nguvu hataki hayo mambo hivyo utakuwa dhaifu kiroho kuliko wenye nguvu za Giza.
2: nguvu za Giza ndiyo zinapenda Sasa hayo makona Kona unayoyafanya , unafanya halafu hutaki kujiunga kuja kuya kuyasujudia .Yatahakikisha yanakunuoosha Hadi useme Yes.
Biashara ya kumtegemea mungu ni nzuri sana lakini inahitaji kujitoa kumtumikia , Tena sio kitoto kitoto lakini inalipa.
Swari: kwanini kwenye hayo makafara na ushirikina mtu anambiwa asipate hata mtoto anakubali, alale hata na mzazi wake anakubali , au anaambiwa pesa yake sio ya kutumia kwenye pombe, kula vizuri au kutoa msaada na anaacha hata pombe????? Kwanini kufuata ya mungu ni ngumu? ??