Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Naona umegive up hoja yako yote.

Kama ni hivyo basi hii thread nzima ni batili. Na uchawi na ushirikina utabaki kuwa imani kama imani nyingine.

Na uhalisia utabaki kuwa maisha ni mchezo wa probability tu.
Nimekubali mkuu lengo lilikuwa kuwachokonoa matajiri wafunguke ila wamegoma kufunguka
 
Wavivu ndio wa kwanza kuamini kwenye ushirikina. Wenzenu wanatengeneza connections na kupata Tender za mabilioni nyie mnakalia eti kafara na maagano 😂️😂️😂️😂️😂️😂️😂️. Hivi kuna Watu walijua kafara na maagano kuliko babu zetu wa kuabudu mizimu? Mbona hawakuwa na huo Utajiri hata wa kumiliki magari ya farasi 😂️😂️😂️😂️. Tengeneza connection, kaa karibu na wakubwa, aminika utakula mema ya nchi.
Hizo connection nyingi za tenda zinazndana na rushwa hatari. Hazina tofauti na washirikina. Tanzania hii either watu ni washirikina, wala rushwa, wakwepa kodi ndio wanatoboa. Wanaopata hela kihalali kabisa ni wachache sana.
 
Sikatai watu kuroga au kuwa washirikina kwenye maisha au biashara. Au waliotajirika kwa ushirikina nawasikia kuwa wapo.
Lakini usiongee kwamba mtu hawezi kuendesha lc300 bila kuroga au ushirikina. Hii sikubali na namshangaa mtu mwenye mawazo haya.
Wewe unaweza kuroga upate hio gari lakini wapo wengi tu wanapata bila kuroga.
Na Kuna walioroga na hawakupata chochote walichokitegemea zaidi ya kubadili waganga tu wakitegemea kwamba siku Moja watatoboa watakapompata mganga hodari kuzidi waliotangulia. Namuomba Allaah anilinde mimi na kizazi changu atuweke mbali na imani za kishirikina.!!.
Zamani miaka ya 1990 /1980 kurudi nyuma kule kwetu wilayani Ngara mkoani Kagera palikuwa na mzee /mganga mmoja aliwaaminisha watu kwamba anao uwezo wa kuzuia mvua isinyeshe.( Waganga wa mvua kwa lugha ya kihangaza na kishubi wanaitwa "abhavurati" na mmoja ni "umuvurati" ).
Basi pakitokea ukame alikuwa anawaamrisha watu wamletee sadaka kama mtama, ulezi,mahindi, kuku,mbuzi ,ndizi nk ili airuhusu mvua inyeshe.
Sasa mara nyingine wakimletea hizo sadaka zao mvua hunyesha na hapo watu huamini kuwa yeye mganga ndiye alikuwa ameizuia mvua isinyeshe. Na wakati mwingine Allaah humuangaza / kumfedhehesha sadaka keshachukua na mvua isinyeshe!!!.
Jambo la kuchekesha sana ni kwamba walikuwa wanamkamata mganga huyo na kumpeleka mtoni wakampiga fimbo nyingi sana ili aamrishe mvua inyeshe au arudishe sadaka alizopewa!!!. Mimi kwa sasa tangu miaka ya 2000 mwanzoni nipo huku mikoa ya kaskazini na Pwani sijui kama ujinga huu bado wanaufanya au waliishaachana nao.!!. Tunachojifunza ni kwamba waganga hawa ni wenye kubahatisha tu. Umeamdikiwa na Mola mtukufu kuwa utamiliki LC 300 ila muda bado haujafika, wewe ukawahi kukimbilia kwa waganga na ulivyofanikiwa ukaamini ni nguvu ya mganga wakati ukweli ni kwamba muda wa kufanikiwa ulikuwa bado kama ambavyo wale wazee wa kule Ngara waliamini mvua imenyesha kwa uwezo wa mganga ( umuvurati) kumbe muda wa mvua kunyesha ulikuwa bado!!.
Na Kuna watu wamezunguka kwa waganga sana na bado mafanikio yao ni kiduchu sana ukilinganisha na walivyokuwa wanatarajia kuwa watakuwa mamilionea. Kwahiyo tujitume, tufanye kazi, tumtegemee Mungu na tupunguze tamaa ya mafanikio ya harakaharaka na tujue Kuna walioandikiwa kupata, watapata kama walivyoandikiwa!.
Na Kuna walioandikiwa kukosa, hao hawatopata hata wakiwatoa kafara watoto wao wataishia jela kama baba yake na yule mtoto albino aliyeuawa kwa kushirikiana na kiongozi wa kanisa kule Bukoba.
 
Hizo connection nyingi za tenda zinazndana na rushwa hatari. Hazina tofauti na washirikina. Tanzania hii either watu ni washirikina, wala rushwa, wakwepa kodi ndio wanatoboa. Wanaopata hela kihalali kabisa ni wachache sana.
Hakuna mshirikina tajiri Acheni kudanganyana. Pili rushwa haiwezi kuwa sawa na ushirikina. Huwezi toa rushwa kwa usiye na connection naye, hapo ni nipe nikupe. Get connected folks.
 
Hakuna mshirikina tajiri Acheni kudanganyana. Pili rushwa haiwezi kuwa sawa na ushirikina. Huwezi toa rushwa kwa usiye na connection naye, hapo ni nipe nikupe. Get connected folks.
Ushirikina una maana pana. Hata hao wachina, wahindi, wazungu wanafanya ushirikina. Wewe unafhani ushirikina ni ulozi tu loh. Ulishaona mtu ananyongwa sababu ya ushirikina? Wenzetu rushwa wanaichulia serious sana na unaweza kunyongwa sababu hiyo. Rushwa ina athiri maisha ya watu wengi kuliko huo ushirikina.
 
Hivi mtu anaweza kufanya biashara na kuwa tajiri maeneo kama kariakoo bila uchawi?
Unaweza, Cha kwanza tambua Hilo Eneo kama Hilo biashara zinamilikiwa na mifumo ya kiimani. Biashara inafanyiwa mahesabu kiimani na hapo unakuwa na utekelezaji kimwili.

Mifumo ya nguvu za Giza ikitawala utaona watu wanaofanya huo ushirikina wanafuata masharti Yao yote kutoka kwenye huo ushirikina , hata akiambiwa sharti la kutokula Nyama maishani yake hatakula au asipate mtoto maishani yake atajitoa sadaka kwa hayo maguvu ya Giza. Maana yake hayo maguvu ya kiza yamempa nguvu ya kufuata huo utumwa na anaona ni fahari .

Kwanini tusitumie nguvu kubwa kufanya hayo katika upande wa Mungu????( Mungu atusaidie na kutupa nguvu ya kuyafuata maagizo yake). Ili uweze kufanya biashara maeneo kama hayo bila ushirikina fanya ya fuatayo:
1. Mshirikishe mungu Hilo wazo lako la kutaka uweke biashara Eneo Hilo kabla ya kwenda( ukienda tu kichwa kichwa kabla ya Kibali utapigwa tu).
A) mungu anaweza akakupa Kibali hapo hapo.. tii sauti yake na fanya hiyo biashara.
B). Mungu anaweza asikupe Kibali Cha kufungua biashara hayo maeneo kabisa badala yake akakuonyesha sehemu nyingine ambayo kwa maono yako unaweza ukaona hapana biashara kabisa ukilinganisha na unavyo ona. Usiende kufungua tu hata kama unaona Kibali hujapata kutoka kwake unaenda ukitengemea atakusaidia( mungu hatafungua hiyo biashara na wewe ,kama amakunyima hicho Kibali. Utafungua biashara bila nguvu ya mungu Wala nguvu ya Giza) kitakachotokea ni kufeli tu. Tena utayakasirisha mashetani ya hapo yatakupiga mno mno. Utakuwa sawa na kupambana majambazi wenye silaha za moto kwa ngumi.
C) anaweza kukupa Kibali lakini kinahitaji mda ,akuandae na ujiamdae kikamirifu. Subiri na kuwa mvumilifu, unaweza ukaanzia kwingine na mda ukifika utafanya tu.


2. Baada ya kupata Kibali , fanya biashara kwa mapenzi ya Mungu, kumwabudu, sadaka, Imani, kusaidia wahitaji bila kusahau Zaka.
3. Usiendekeze Uovu wewe au biashara yako.. biashara inyooke kama Rula, siwe na udanganyifu ,uongo ongo ,upigaji . Hapa ndiyo patamu na unaweza ukaona ,pamoja na kufanya mengine utaishia kupigwa tu kibiashara sababu 1: nguvu kubwa( Mungu) anayekupa hizo nguvu hataki hayo mambo hivyo utakuwa dhaifu kiroho kuliko wenye nguvu za Giza.
2: nguvu za Giza ndiyo zinapenda Sasa hayo makona Kona unayoyafanya , unafanya halafu hutaki kujiunga kuja kuya kuyasujudia .Yatahakikisha yanakunuoosha Hadi useme Yes.


Biashara ya kumtegemea mungu ni nzuri sana lakini inahitaji kujitoa kumtumikia , Tena sio kitoto kitoto lakini inalipa.
Swari: kwanini kwenye hayo makafara na ushirikina mtu anambiwa asipate hata mtoto anakubali, alale hata na mzazi wake anakubali , au anaambiwa pesa yake sio ya kutumia kwenye pombe, kula vizuri au kutoa msaada na anaacha hata pombe????? Kwanini kufuata ya mungu ni ngumu? ??
 
Yuko sahihi anachokisema.

Nimepita kwenye field ya madereva nimejionea sana how witchcraft is applied in their daily activities.

Mkuu, wanasema no research no right to speak...
Translation: wanatapeliwa na waganga
 
Nilichogundua ni kwamba ulikua unataka tu kutuonesha kwamba wewe unajua sana aina za magari...sasa LC300 ndo kitu gani?!...watanzania wangap wanafatilia mambo ya model za magari?!..unapoandika bango lako tumia lugha nyepesi kila mtu akuelewa acha kuwapa kazi ya watu kwenda kugoogle...ungeandika LandCruiser bango lako lingekua rahisi sna kueleweka
 
Sad kusoma posts kama hizi ya kuwa kuna watu wanaweza kuwa defeated mentally kama hivi.

Ubongo unakubali chochote unachokiamisha. Mawazo yako ndio yenye uwezo wa kuuaminisha ubongo ya kuwa jambo fulani liinawezekana au la; hiyo ndio register yake.

Uwezi kupewa gari la kifahari kama manna kutoka mbinguni, lakini unaweza kulipata kwa kupanga mikakati (of course with the right mission plan).

Utakiwi kuwa na defeated notion kwenye mtazamo wa maisha kama hivi hasa kwenye simple goals.

Hivi wangapi humu wangeweza baki salama kwa changamoto zetu za maisha tulizopitia wengine na kubaki Salama na akili timamu.

Mission ya gari tu bila ya changamoto za mamia ya binadamu wanaotaka uumie; kuna watu kwao ngumu. Sasa ungeuweza mziki wetu, watu wako wote wa karibu wanakuombea ukwame na unasonga mbele.

Mnacheza na maisha.
 
Nyingi mnaotukuza magari na simu ndio kipindi kile mlikuwa mmeinamia sanamu la Ng'ombe wa dhahabu
 
Sad kusoma posts kama hizi ya kuwa kuna watu wanaweza kuwa defeated mentally kama hivi.

Ubongo unakubali chochote unachokiamisha. Mawazo yako ndio yenye uwezo wa kuuaminisha ubongo ya kuwa jambo fulani liinawezekana au la; hiyo ndio register yake.

Uwezi kupewa gari la kifahari kama manna kutoka mbinguni, lakini unaweza kulipata kwa kupanga mikakati (of course with the right mission plan).

Utakiwi kuwa na defeated notion kwenye mtazamo wa maisha kama hivi hasa kwenye simple goals.

Hivi wangapi humu wangeweza baki salama kwa changamoto zetu za maisha tulizopitia wengine na kubaki Salama na akili timamu.

Mission ya gari tu bila ya changamoto za mamia ya binadamu wanaotaka uumie; kuna watu kwao ngumu. Sasa ungeuweza mziki wetu, watu wako wote wa karibu wanakuombea ukwame na unasonga mbele.

Mnacheza na maisha.
Eti lc 300 hio si pesa ya mstaafu mmoja wa umma aliyefanya kazi miaka 40.
Kwa wengine ni pesa ya kununulia pumba za kulishia nguruwe.
Fikra za black zimejengwa kwenye uchawi.
You is what you think na brain inajengwa na vitu viwili unavyoviona na kuvisikia
 
Eti lc 300 hio si pesa ya mstaafu mmoja wa umma aliyefanya kazi miaka 40.
Kwa wengine ni pesa ya kununulia pumba za kulishia nguruwe.
Fikra za black zimejengwa kwenye uchawi.
You is what you think na brain inajengwa na vitu viwili unavyoviona na kuvisikia
Kabisa, it’s sad; kuna watu wana fikra kama hizi.
 
Back
Top Bottom