Huwezi kutajirika kwa kutegemea mshahara, mishahara ni ya wa miaka 20s 30s na married women

"Kama kwa sababu yoyote ile kesho asubuhi vyanzo vyako vyote vya mapato vimesimamishwa kama utashindwa kuishi miezi sita (6) kwa maisha unayoishi sasa hivi basi upo kwenye kundi la watu masikini" kwa kigezo hicho watumishi wengi wa serikali waalimu Askari afya ni masikini, kwasbb wiki moja ya kuachishwa kazi mtu anakimbia jiji........
 
Ni kweli.. lakini ni kauzembe fulani unaweza ukatumia Mshahara kufikia uhuru wa kifedha ..

Hata hauna haja ya kufukuzwa, unaacha kazi mwenyewe ..

😀😀😀
 
Mashirika gani mkuu wengi tuko huko tunajua mishahara yao we taja nikupe salary scale zao.
Kama upo kwenye mashirika basi upo kwenye shirika lenye njaa ila niamini mimi kuna mahali watu wanakunja 9M na wachini mwishoni hawashuki 1M na point kisha vibarua hawashuki laki 3 hapo ni bila posho.
 
Hapana uwezi ukasave pesa mpaka uwe tajiri isipokuwa unasave pesa Ili iweze kukutengenezea utajiri Kwa biashara utayofanya au uwekezaji
 
Kama upo kwenye mashirika basi upo kwenye shirika lenye njaa ila niamini mimi kuna mahali watu wanakunja 9M na wachini mwishoni hawashuki 1M na point kisha vibarua hawashuki laki 3 hapo ni bila posho.
Wapi mkuu acha kupa watu mwoyo, take home ya 9m sio mchezo hapa bongo
 
Unamanisha saidia fundi au civil Engineers, wengi huwezi kuwalinganisha kwa kipato na waalimu alio ajiliwa serikalini au private, mualimu hawezi kufanya muamala wa 30m bila kulopa benki au kuuza shamba.
Hapa bado hujajibu swali
 
Endelea kukaririri hivyo hivyo !! Ila nakuapia Kuna watumishi wa umma wana ukwasi wa ajabu!! Huwezi kuamini wapo kimyaaaaa!!
 
Kuna watu wapo serikalini Wana misharaha ya milioni 3,4,5,6, nk Wana ukwasi wa hatari ndugu Mimi nilikuwa sijui kama wewe ila nimewaona!?
Kuna mtu ana kopa mpaka milioni mia mbili !! Anawekeza anapiga pesa mbaya !! Watu wanatumia ajira kusaka mtaji!?
Serikalini Kuna mtu Mshahara wake ni 40M?
 
Wezi kabisa maana mshahara unapimwa tu kulingana na basics zako
Nakupa mfano mdogo Sana!! Nmb anakopesha watumishi mpaka milioni 200!! Sasa mtu aliyechukua hizo 200 m !! Akanunua
1) rice grading mashine 35milion
2) akavuta tandam Moja 40mil
3) akavuta Massey fagason Moja 30 milioni
Akawekeza kwenye kilimo Cha mpunga na kuuchakata na kuupeleka Kenya na Uganda na south Sudan na sehemu akauza Michele DSM!! Unasemaje hapo!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…