Huwezi kutajirika kwa kutegemea mshahara, mishahara ni ya wa miaka 20s 30s na married women

Huwezi kutajirika kwa kutegemea mshahara, mishahara ni ya wa miaka 20s 30s na married women

Kama Unaishi Chini Ya Hivi Viwango Vya Kimataifa Wewe ni Masikini…

Mpendwa Mpambanaji, Habari!...

Kulingana na viwango vya vipato vinavyotumika kimataifa masikini ni mtu anayetengeneza fedha chini ya dola 30,000 za kimarekani kwa mwaka (sawa na shilingi za kitanzania milioni 48) na anayemiliki mali yenye thamani isiyozidi dola 5,000 (sawa na shilingi za kitanzania milioni 8).

Kwa kutumia viwango hivi vya kimataifa zaidi ya nusu ya wa Tanzania wanaingia kwenye kundi la watu masikini.

Ili uwe na kipato kisichopungua shilingi za kitanzania milioni 48 kwa mwaka inabidi angalau kila mwezi kipato chako kisipungue shilingi milioni 4.

Ni wafanyakazi wachache sana ambao kipato chao cha mwezi ni shilingi milioni 4 au zaidi.

Hata kwa wafanyabiashara wa kitanzania bado wengi hawatengenezi faida inayozidi million 4 kwa mwezi .

Ukigawa shilingi million 4 kwa siku thelathini ni sawa na Tshs 133,000 bado ni kiwango ambacho watu wengi waliojiajiri ama wanaofanya biashara hawawezi kuingiza kwa siku kama faida.

Kama wewe umeajiriwa je kipato chako kwa mwezi kinazidi milioni 4? …

Kama umejiajiri ama unafanya biashara je faida yako kwa siku inazidi shilingi laki moja na elfu thelathini na tatu (133,000)?...

Kama jibu lako ni hapana basi upo kwenye kundi la watu masikini.

Kama mali zako unazomiliki thamani yake haizidi shilingi milioni 8 (Tshs 8,000,000) pia upo kwenye kundi la watu masikini duniani.

Kama hauna nyumba au gari au mali nyingine yoyote amabyo thamani yake inqaweza kufikia milioni 8 tayari unaingia kwenye kundi hili la watu masikini.

Tukiachana na hivi viwango vya kimataifa ambavyo unaweza kusema ni vikubwa sana na hivyo havikutendei haki tuangalie viwango vingine ambavyo vitaamua kama wewe ni masikini au la.

Kama hauna uhakika wa kula miezi sita (6) ijayo hata usipofanya kazi upo kwenye kundi la watu masikini.

Kama kwa sababu yoyote ile kesho asubuhi vyanzo vyako vyote vya mapato vimesimamishwa kama utashindwa kuishi miezi sita (6) kwa maisha unayoishi sasa hivi basi upo kwenye kundi la watu masikini.

Kama wewe ni mfanyakazi na mishahara yako haikutani upo kwenye kundi la watu masikini.

Na kama una madeni makubwa amabyo ulitumia kwenye matumizi ya kawaida kama kula na hujui utayalipaje upo kwenye kundi la watu masikini.

Kama umejiajiri au unafanya biashara na kama biashara yako haiwezi kwenda bila ya wewe kuwepo kwenye kazi au biashara hivyo upo kwenye kundi la watu masikini.

Kama kwa sababu yoyote iwe kazi ama biashara yako imeshindwa kufanyika kwa siku kadhaa na ikawa na madhara makubwa sana kwako kiuchumi upo kwenye kundi la watu masikini.

Hii ina maana kwamba kipato unachopata kwa siku ndio unakitegemea kwa matumizi ya kila siku.

Kama unaingia kwenye mojawapo ya vigezo hivyo hapo juu wewe ni masikini.

Usiogope haupo pekee yako wa Tanzania wengi wanaingia kwenye hivyo vigezo vya umasikini.

Habari Njema Kwako…

Kama umegundua wewe ni masikini usisikitike wala kukata tamaa kwa umasikini ulionao.

Umasikini sio kilema hivyo unaweza kubadili hali hiyo kama kweli utataka kufanya hivyo.

Na ili uweze kutoka hapo ulipo unapaswa kupata maarifa sahihi kabisa ya kutengeneza UTAJIRI .
"Kama kwa sababu yoyote ile kesho asubuhi vyanzo vyako vyote vya mapato vimesimamishwa kama utashindwa kuishi miezi sita (6) kwa maisha unayoishi sasa hivi basi upo kwenye kundi la watu masikini" kwa kigezo hicho watumishi wengi wa serikali waalimu Askari afya ni masikini, kwasbb wiki moja ya kuachishwa kazi mtu anakimbia jiji........
 
"Kama kwa sababu yoyote ile kesho asubuhi vyanzo vyako vyote vya mapato vimesimamishwa kama utashindwa kuishi miezi sita (6) kwa maisha unayoishi sasa hivi basi upo kwenye kundi la watu masikini" kwa kigezo hicho watumishi wengi wa serikali waalimu Askari afya ni masikini, kwasbb wiki moja ya kuachishwa kazi mtu anakimbia jiji........
Ni kweli.. lakini ni kauzembe fulani unaweza ukatumia Mshahara kufikia uhuru wa kifedha ..

Hata hauna haja ya kufukuzwa, unaacha kazi mwenyewe ..

😀😀😀
 
Mashirika gani mkuu wengi tuko huko tunajua mishahara yao we taja nikupe salary scale zao.
Kama upo kwenye mashirika basi upo kwenye shirika lenye njaa ila niamini mimi kuna mahali watu wanakunja 9M na wachini mwishoni hawashuki 1M na point kisha vibarua hawashuki laki 3 hapo ni bila posho.
 
Nimekuelewa mkuu , uko sahihi ..

Soma tena alichoandika, halafu urudi kusoma haya maneno chini ..

Ametaja njia kuu nne za kuweza kupata utajiri na njia moja wapo amesema savings kwa kujibana!!

Yaani ufanye kazi , ujibane matumizi mpaka ile pesa uliyoisave ikufanye uwe tajiri ..

Naomba unijibu Kwamimi ambae sina chanzo cha kipato ntatumiaje mbinu namba tatu kua tajiri!?
Hapana uwezi ukasave pesa mpaka uwe tajiri isipokuwa unasave pesa Ili iweze kukutengenezea utajiri Kwa biashara utayofanya au uwekezaji
 
Kama upo kwenye mashirika basi upo kwenye shirika lenye njaa ila niamini mimi kuna mahali watu wanakunja 9M na wachini mwishoni hawashuki 1M na point kisha vibarua hawashuki laki 3 hapo ni bila posho.
Wapi mkuu acha kupa watu mwoyo, take home ya 9m sio mchezo hapa bongo
 
Unamanisha saidia fundi au civil Engineers, wengi huwezi kuwalinganisha kwa kipato na waalimu alio ajiliwa serikalini au private, mualimu hawezi kufanya muamala wa 30m bila kulopa benki au kuuza shamba.
Hapa bado hujajibu swali
 
Endelea kukaririri hivyo hivyo !! Ila nakuapia Kuna watumishi wa umma wana ukwasi wa ajabu!! Huwezi kuamini wapo kimyaaaaa!!
 
Kuna watu wapo serikalini Wana misharaha ya milioni 3,4,5,6, nk Wana ukwasi wa hatari ndugu Mimi nilikuwa sijui kama wewe ila nimewaona!?
Kuna mtu ana kopa mpaka milioni mia mbili !! Anawekeza anapiga pesa mbaya !! Watu wanatumia ajira kusaka mtaji!?
Serikalini Kuna mtu Mshahara wake ni 40M?
 
Wezi kabisa maana mshahara unapimwa tu kulingana na basics zako
Nakupa mfano mdogo Sana!! Nmb anakopesha watumishi mpaka milioni 200!! Sasa mtu aliyechukua hizo 200 m !! Akanunua
1) rice grading mashine 35milion
2) akavuta tandam Moja 40mil
3) akavuta Massey fagason Moja 30 milioni
Akawekeza kwenye kilimo Cha mpunga na kuuchakata na kuupeleka Kenya na Uganda na south Sudan na sehemu akauza Michele DSM!! Unasemaje hapo!??
 
Back
Top Bottom