Wengi hawafahamu ya kuwa uislam ni chombo au mpango wa waarabu kueneza tamaduni, mila na desturi zao. Nachelea kusema hivyo kwa sababu wenyewe waislam wanasema uislam is a total way of life.
Kwa maana nyingine ni utamaduni jumla wa maisha ya watu. Mambo yafuatayo ndiyo yanayonifanya niamini kwamba uislam ni mpango wa waarabu ku assimilate watu wengine wafuate mila za kiarabu.
1. Lugha inayotumika kufanya ibada yao ni kiarabu.
2. Muanzilishi wa dini yao alikuwa muarabu
3. Kitabu chao kimeandikwa kwa lugha ya kiarabu
4. Majina ya waumini wao ni ya kiarabu
5. MAvazi ya waumini wao ni ya tamaduni za kiarabu
6. Majengo yao ya ibada yana mtindo au architectural design ya uarabuni
7. Ala za muziki zinazotumika katika nyimbo za ibada zao ni za asili ya kiarabu
8. Vyakula au mapishi (cuisine) ni ya kiarabu
9. Namna ya kucheza muziki wa sherehe zao ni za kiarabu.
10. Mirathi, ndoa na maziko ni desturi za kiarabu
Kuna mambo mengi ambayo ukiyachunguza yanaenda zaidi ya imani. Yana taka yawe katika ujumla wote wa maisha ya Mtanzania.
Changamoto ni kwamba, kwenye secular state ni ngumu sana kutekeleza desturi hizo, kwa maana serikali yetu haifungamani na dini yoyote.
Karibuni wadau katika kujadili hili mkiwa na akili huru.
CC:
Bwana Utam kahtaan FaizaFoxy Kosugi
Mkuu inapendeza sana unapotaka kuandika chochote hasa kile ambacho huna ufahamu nacho UKAFANYA ITAFITI JAPO MDOGO.
Unless kama umekusudia kupotosha .
Ashakum si matusi -Haifai kumjibu Mjinga
lakin kwa faida ya wasomaji ipo haja ya kuweka sawa jambo hili.
Na Nitajielekeza katika point zako mbili tu
No.1 & 2 Zilizobaki umeandika nonsenses
Maana ya UISLAM si hiyo iliyoandika hapo na hapo ndipo inapoonesha uwezo wako Mdogo wa kufuatilia.
UISLAM ni Nini?
UISLAM ni Kujisalimisha kwa MUUMBA kwa Twaa(kumtii) Na kumpwekesha katika ibada (Kumuabudia yeye pekee) na Kujiepusha na Shirki (Kujitenga na mambo yote yanayohusiana na Ushirikina)
☝️ Ndio maana ya UISLAM sasa Ndugu hiyo yako umezitoa wapi?
Katika Uislam Tunaamini katika Vitabu vinne(4) walivyo letewa Manabii
1. ZABURI -Nabii DAUDI (Alayh Salaam)
2. TAURAT - Nabii MUSSA (Alayh salaam)
3. INJILI - Nabii ISSA (Alayh salaam)
4. QUR'AN -Muhammad(swala &salaam juu yake)
• Uletwaji wa hawa manabii ulielekezwa hasa kwa jamii ambazo kwa zama hizo zilikuwa zimechupa mipaka ya Uasi. za wakipelekewa UJUMBE huo kutoka kwa MUUMBA wao kwa lugha wanaielewa wao.
Na ndio maana DAUD,MUSSA na ISSA wote wakapelekwa na jamii ya MAYAHUDI na kwa lugha zao.
MWANZILISHI wa UISLAM si Nabii Muhammad (juu yake sala na salaam) Uislam upo toka Zama za Nabii NUHU ( Alayh salaam )
Na haya tumeyajua baada ya ALLAH kutupa habari za watu za Zama zilizopita kupitia huo QUR'AN , Unapomsikia NABII NUHU zivute fikra zako (kama unazo lakin) mpaka zama za mwanzo za kuanza kwa maisha ya Kiumbe Mwanadamu maana NUHU aliletwa baada ya tu ADAM.
Sasa kama Muanzilishi wa UISLAM ni MTUME WETU NUHU ,SWALEH ,IDIRISSA ,ILIYASA ,MUSSA, YAAKUBU ,SULEYMAN, DAUD, IS'HAQA
ISMAAIL, IBRAHEEM, ISSA, n.k
kama unavyodai muanzilishi ni Muhammad hao wote walikuwa DINI GANI?
na hayo majina ni majina ya dini?
wakati wote walikuja kabla ya Muhammad ( juu yake sala na salamu)
REJEA TENA ULIKOCHOTA MAKOROKORO YAKO KISHA JIFUNZE UPYA UKITANGULIZA HAMU YA KUJUA NA SI CHUKI- Kwasababu walipita watu smart & Intelligent waliokuwa na chuki sizizomithilika na wameondoka na Uislam na QUR'AN vipo vile vile , kwanini? kwasababu mwenye QUR'AN na dini yake ameahidi kuvihami na Yeye ni MKWELI WA AHADI.