Huwezi kuwa Muislamu kama humpendi Isa (Yesu) au kumdhihaki

Huwezi kuwa Muislamu kama humpendi Isa (Yesu) au kumdhihaki

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,682
Reaction score
41,162
Kwa kweli, huwezi kuwa Muislamu ukiwa huwa umpendi na kumwaamini Malaika wote, Manabii na Mitume wote!

Qur'an (Surat Al-Baqarah 2:285):
“…Wote wanamwamini Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake. Hatubagui kati ya yeyote katika Mitume Wake…”

Uislamu ni dini ya imani kamili kwa mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu — akiwemo Yesu (Isa bin Maryam), Musa, Ibrahim, Nuhu na Muhammad (s.a.w) Waislamu Wanaamini Yesu Atarudi Kumpiga Dajjali.

Mtume Paulo ndo akaja akaharibu monotheism Gospel ya yesu akabadili muelekeo na kuunda Imani mpya ya kikuristo.

Surat Al-Ma'idah (5:116).Hii hapa tafsiri yake kwa Kiswahili:

“Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa miungu badala ya Mwenyezi Mungu?

Atasema: Subhanaka! (Utukufu ni Wako!) Hakuwa haki yangu kusema nisiyokuwa na haki nayo. Kama ningelisema, bila shaka ungalijua. Unajua yaliyo moyoni mwangu, wala mimi siyajui yaliyo moyoni Mwako. Hakika Wewe ndiwe Mjuzi wa mambo ya ghaib.

Aya hii inaonyesha wazi kuwa Yesu (Isa a.s) hakuagiza watu wamuabudu yeye wala mama yake. Badala yake, alifundisha kumwabudu Mwenyezi Mungu pekee. Aya hii ni hoja muhimu katika msimamo wa Kiislamu dhidi ya imani ya Utatu.
 
YESU NI MUNGU,HATA WEWE PIA NI MUNGU MDOGO. AU ULIWAHI KUONA WAPI MTOTO WA NYOKA AKAWA NGE? PAMBANENI NA DINI YENU MAANA INAMAPUNGUFU MENGI TU PIA.
 
Quran inachekesha sana.
Miaka yote mtu anaitwa Yeshua. Tena ni Myahudi (ushahidi uko) alaf miaka 600 mbele mseme hapana haitwi Yeshua bali anaitwa Issa.
Mkuu ni lugha jina la Yesu hubadilika kulingana na lugha husika kwa mfano:

Haya ndiyo majina ya Yesu katika lugha mbalimbali:

1. Kiarabu: عيسى (ʿĪsā)
2. Kiebrania (Hebrew): יֵשׁוּעַ (Yeshua)
3. Kigiriki (Greek): Ἰησοῦς (Iēsous)
4. Kilatini (Latin): Iesus
5. Kiingereza: Jesus
6. Kihispania: Jesús
7. Kifaransa: Jésus
8. Kijerumani: Jesus
9. Kirusi: Иисус (Iisus)
10. Kichina (Mandarin): 耶稣 (Yēsū)
11. Kihindi: यीशु (Yeshu)
12. Kiswahili: Yesu
13. Kituruki: İsa
14. Kipersia (Farsi)*: عیسی (ʿĪsā)

Jina linabadilika kulingana na fonolojia ya lugha, lakini linarejea mtu ni yuleyule –Nabii Isa au Yesu.
 
Issah wa Quran amelisurubiwa msalabani??
 
Isaya 9 : 6
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani".
Isaya 9:6 (Biblia Kiswahili):
Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wa Kiyahudi wanaitafsiri kuwa inamhusu mfalme wa wakati huo (kama Hezekia) na si masihi wa baadaye. Tafsiri inategemea imani na muktadha wa mtu anayesoma, wewe mkuristo unavutia kwako kwasbb ya malengo yako.
 
hizo sifa zote unaona zinafanana na mfalme kweli!!!hata kama umeamua kuzima kichwa???
 
YESU NI MUNGU,HATA WEWE PIA NI MUNGU MDOGO. AU ULIWAHI KUONA WAPI MTOTO WA NYOKA AKAWA NGE? PAMBANENI NA DINI YENU MAANA INAMAPUNGUFU MENGI TU PIA.
Mkuu Yesu hakuwahi kusema yeye ni Mungu Katika Yohana 17:3, Yesu anasema: “Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” Hapa Yesu anajitofautisha wazi na Mungu.

Mtoto wa nyoka sio lazima awe nyoka Kauli hiyo ni methali tu isiyotumika kama hoja ya imani. Katika Biblia, watu wote wanaitwa viumbe wa Mungu (Malaki 2:10). Kumbe mtu kuwa kiumbe wa Mungu haimaanishi kuwa yeye pia ni Mungu.

Yesu alitambua mamlaka ya Mungu juu yake Katika Yohana 5:30 anasema “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe…”Ikiwa Yesu ni Mungu, kwa nini awe hana uwezo wa kujitendea chochote?
 
Mkuu ni lugha jina la Yesu hubadilika kulingana na lugha husika kwa mfano:

Haya ndiyo majina ya Yesu katika lugha mbalimbali:

1. Kiarabu: عيسى (ʿĪsā)
2. Kiebrania (Hebrew): יֵשׁוּעַ (Yeshua)
3. Kigiriki (Greek): Ἰησοῦς (Iēsous)
4. Kilatini (Latin): Iesus
5. Kiingereza: Jesus
6. Kihispania: Jesús
7. Kifaransa: Jésus
8. Kijerumani: Jesus
9. Kirusi: Иисус (Iisus)
10. Kichina (Mandarin): 耶稣 (Yēsū)
11. Kihindi: यीशु (Yeshu)
12. Kiswahili: Yesu
13. Kituruki: İsa
14. Kipersia (Farsi)*: عیسی (ʿĪsā)

Jina linabadilika kulingana na fonolojia ya lugha, lakini linarejea mtu ni yuleyule –Nabii Isa au Yesu.
Historia ya Yeshua( Yesu) tangu sehemu alipozaliwa inatofautiana na ile ya Isa, hivyo hao ni watu wawili tofauti kwa muktadha huo.
 
kwahiyo Allah anadhani sisi wakristo tunamuita Yesu na mama yake ni Miungu!!!!
Mkuu hata sijakuelewa Allah ni Allah na Yesu ni Yesu hata kwenye biblia ya kiarabu Yesu ni Issa Allah ni Mungu.
 
Historia ya Yeshua( Yesu) tangu sehemu alipozaliwa inatofautiana na ile ya Isa, hivyo hao ni watu wawili tofauti kwa muktadha huo.
Ushahidi tafadhali mkuu, sitaki porojo hapa no evidence shut-up.
 
Mkuu hata sijakuelewa Allah ni Allah na Yesu ni Yesu hata kwenye biblia ya kiarabu Yesu ni Issa Allah ni Mungu.
rejea andiko lako kule juu,maelezo ya Allah akimuliiza Issah.
wewe umewaambiwa watu wakufanye wewe na mama yako Mungu???
 
Back
Top Bottom