Huwezi kuwa Muislamu kama humpendi Isa (Yesu) au kumdhihaki

Huwezi kuwa Muislamu kama humpendi Isa (Yesu) au kumdhihaki

Mariam mama wa Yesu alikua na miaka 13 wakati anapat ujauzito wa Yesu Joseph alikua na miaka 93 wakati anamuoa Mariamu.....sasa watuambie huo pia ibakaji?
Leta andiko lenye umri halisi wa mariam mama wa Yesu.
 
Ni tafasiri tofauti ila mtu ni yule yule, wakuristo wengi wamepotosaha mafundisaho na ukweli kuhusu huyu Yesu au Isa kwa malengo ya kiasiasa na kiutawala.
Embu fafanua ni kwa namna gani watawala waliamua kusema Yesu alikufa akafufuka,atarudi kuhukumu wasiomfata,kuliwarahisishia wao kutawala.
 
Mkuu ni lugha jina la Yesu hubadilika kulingana na lugha husika kwa mfano:

Haya ndiyo majina ya Yesu katika lugha mbalimbali:

1. Kiarabu: عيسى (ʿĪsā)
2. Kiebrania (Hebrew): יֵשׁוּעַ (Yeshua)
3. Kigiriki (Greek): Ἰησοῦς (Iēsous)
4. Kilatini (Latin): Iesus
5. Kiingereza: Jesus
6. Kihispania: Jesús
7. Kifaransa: Jésus
8. Kijerumani: Jesus
9. Kirusi: Иисус (Iisus)
10. Kichina (Mandarin): 耶稣 (Yēsū)
11. Kihindi: यीशु (Yeshu)
12. Kiswahili: Yesu
13. Kituruki: İsa
14. Kipersia (Farsi)*: عیسی (ʿĪsā)

Jina linabadilika kulingana na fonolojia ya lugha, lakini linarejea mtu ni yuleyule –Nabii Isa au Yesu.
Aitwe Yesu aitwe Isa -- jina sio shida kama wanamlenga yule yule -- Mzungu atamuita Jesus mswahili atamuita Yesu mturuki atamuita Isa


Hoja kubwa Ni Mungu au ni mjumbe wa Mungu ?

Watu watofautiane hapo
 
Aitwe Yesu aitwe Isa -- jina sio shida kama wanamlenga yule yule -- Mzungu atamuita Jesus mswahili atamuita Yesu mturuki atamuita Isa


Hoja kubwa Ni Mungu au ni mjumbe wa Mungu ?

Watu watofautiane hapo
Ndio maana mahakamani huwa kuna maswali ya msingi ili kujua kama shahidi anamjua anayekuja kumtolea ushahidi.

wakrsto wana Yesu na wanamuita Mungu,waislam wana Issah wanamwita mtume tu.
ili tujue ni mtu mmoja huyu au lah,tujue wasifu wke pande zote.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ushahidi tafadhali mkuu, sitaki porojo hapa no evidence shut-up.
Mkuu, kama lengo lako ni kutushawishi tuingie kwenye dini yako, basi niseme wazi kwamba mimi umeishanikosa, hunipati kamwe. Maneno yako na mtindo wako wa majibizano ni ushahidi wa wazi kuwa dini unayoiwakilisha inakumbatia ukali, matusi na hasira.

Mimi siwezi kujiunga na dini inayokosa uvumilivu, staha, na busara za mazungumzo. Nimezaliwa na kulelewa katika Ukristo. Ukristo unahubiri upendo, msamaha, subira, na unyenyekevu. Yesu anatufundisha kuwapenda adui, kuwasamehe wanaotukosea hata saba mara sabini, na kuwaheshimu wanaotupinga.

Sasa hapa ndipo inapojitokeza tofauti ya kweli kati ya Yesu na Isa:

Yesu anayehubiriwa na Wakristo anaonyesha upendo wa Mungu kwa wanadamu. Ni mnyenyekevu, anayeosha mpaka miguu ya wanafunzi wake. Aliposulibiwa msalabani, aliwaombea msamaha waliomsulubisha.

Kwa hiyo, kama Isa wa Qur'an ndio anakushawishi uwe na hasira na kejeli, basi hakuna shaka, Isa sio Yesu. Niache mimi nibaki na Yesu ambaye habari zake zimeandikwa kwenye Biblia.
 
Ndio maana mahakamani huwa kuna maswali ya msingi ili kujua kama shahidi anamjua anayekuja kumtolea ushahidi.

wakrsto wana Yesu na wanamuita Mungu,waislam wana Issah wanamwita mtume tu.
ili tujue ni mtu mmoja huyu au lah,tujue wasifu wke pande zote.
Hoja kubwa ya utofauti hawa wanasema ni Mungu na wengine wanasema nyie mmeposha hakuwa Mungu.

Ila kimsingi wote wanajaribu kumuongelea huyo huyo. --- nacho maanisha ni intent

And NB: kuna wakristo wachache nao wanasema sio Mungu


Huko kwenye wasifu sina comments,

Ila kwenye lugha au majina hapa ntapasimamia majina ni lugha tu na hali ya kukubaliana
 
Uongo dhambi.
Hosea 9:5

" Mtafanya nini katika siku ya mkutano wa idi, na katika siku ya karamu ya BWANA?"
hiyo siku ya idi uliyoandika, umesoma biblia aliyoandika mood au ipi? hakuna idi kwenye Biblia tunazotumia wakristo.

Hosea 9:5; "What will you do on the day of the appointed festival, and on the day of the feast of the Lord?" Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za Bwana?

KJV inasema " What will ye do in the solemn day, and in the day of the feast of the Lord? "
 
Hoja kubwa ya utofauti hawa wanasema ni Mungu na wengine wanasema nyie mmeposha hakuwa Mungu.
wala sio tofauti ya msingi kwa imani zote mbili hizi,unafikiri wangekuwa wanaamini tu hakuwa Mungu kisha wakakubali alisulubiwa na akafufuka tungekuwa na shida nao!!!issue ni kwamba tofauti ni nyingi hiyo ni moja wapo.
Ila kimsingi wote wanajaribu kumuongelea huyo huyo. --- nacho maanisha ni intent
kma ni kujaribu sawa,ila watakuwa wanabahatisha kumfanya awe wanayetamani awe.
And NB: kuna wakristo wachache nao wanasema sio Mungu
msingi wa imani ya kikristo sio kuamini Yesu ni Mungu,ni kuamini alikufa,alifufuka atakuja tena kuhukumu watu sio kuua nguruwe na kuoa.
Huko kwenye wasifu sina comments,

Ila kwenye lugha au majina hapa ntapasimamia majina ni lugha tu na hali ya kukubaliana
kabisa,na ndio maana hoja yetu pia sio jina,ni mhusika,kama wangemwita Issah awe na sifa zile zile za kwenye bible,wala kusingekuwa na shida.
 
hiyo siku ya idi uliyoandika, umesoma biblia aliyoandika mood au ipi? hakuna idi kwenye Biblia tunazotumia wakristo.

Hosea 9:5; "What will you do on the day of the appointed festival, and on the day of the feast of the Lord?" Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za Bwana?

KJV inasema " What will ye do in the solemn day, and in the day of the feast of the Lord? "
Idi maana yake sikukuu mkuu.

Hizi zingine lugha tu wakuu
 
wala sio tofauti ya msingi kwa imani zote mbili hizi,unafikiri wangekuwa wanaamini tu hakuwa Mungu kisha wakakubali alisulubiwa na akafufuka tungekuwa na shida nao!!!issue ni kwamba tofauti ni nyingi hiyo ni moja wapo.

kma ni kujaribu sawa,ila watakuwa wanabahatisha kumfanya awe wanayetamani awe.

msingi wa imani ya kikristo sio kuamini Yesu ni Mungu,ni kuamini alikufa,alifufuka atakuja tena kuhukumu watu sio kuua nguruwe na kuoa.

kabisa,na ndio maana hoja yetu pia sio jina,ni mhusika,kama wangemwita Issah awe na sifa zile zile za kwenye bible,wala kusingekuwa na shida.
Naam,

mkuu kuamini ni Mungu au sio Mungu , sio issue sana?
 
1. Yesu na Mungu ni Mmoja

Yohana 10:30

“Mimi na Baba tu umoja.”

(Hii ni kauli ya moja kwa moja ya Yesu kuonyesha kwamba yeye na Mungu Baba ni kitu kimoja.)

2. Aliyemwona Yesu amemwona Baba

Yohana 14:9-10
Yesu akamwambia, “Mimi nimekuwa pamoja nanyi muda wote hivi, nawe hujanijua, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wasemaje, Tuonyeshe Baba? Je! huamini ya kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?”

3. Yesu ni Neno la Mungu aliyefanyika mwili

Yohana 1:1-3, 14
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu…”

(Hapa “Neno” ni Yesu – inaonyesha uungu wake.)

4. Mamlaka ya Mwana ni ya Baba

Mathayo 28:18-19

Yesu akaja akasema nao, akisema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.”

Hii ni mojawapo ya mistari wazi ya Utatu Mtakatifu — inazitaja nafsi zote tatu za Mungu kwa pamoja.

5. Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na hutumwa na Yesu

Yohana 15:26

“Lakini ajapo Msaidizi nitakayempeleka kwenu kutoka kwa Baba, yaani, Roho wa kweli atokaye kwa Baba, huyo atanishuhudia.”

6. Utatu Unaonekana Wakati Yesu Anabatizwa

Mathayo 3:16-17

Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”

Hapa tunaona Utatu:
  • Yesu anabatizwa,
  • Roho Mtakatifu anashuka,
  • Mungu Baba anazungumza kutoka mbinguni.
 
Naam,

mkuu kuamini ni Mungu au sio Mungu , sio issue sana?
wala sio issue sana,maana ni Mungu kamili na binaadam kamili.hutendi dhambi kuamini si Mungu.
na angetaka watu wote waamini yeye ni Mungu asingekuwa anaficha uwezo alio nao.
 
Huu mjadala hauna mwisho, hakuna anaejua dini ipi ni ipi lakini sote tunajua ili kwenda mbinguni ni lazima utende wema, na dini zote zimeweka wazi ni vitu gani usifanue na nini ufanye ili uende mbinguni. Tenda wema, Toa sadaka, Fanya ibada, Mengine ni rehema za mungu. Warabu walileta uislamu, wazungu walileta ukristo. Hii mada tuwaachie wao. Humu hakuma anaejua Quran iliandikwa vipi ila ukiulizwa utasema ulichoambiwa, the same na biblia. So hii mada ni waste of time
 
wala sio issue sana,maana ni Mungu kamili na binaadam kamili.hutendi dhambi kuamini si Mungu.
na angetaka watu wote waamini yeye ni Mungu asingekuwa anaficha uwezo alio nao.
wakrsto wana Yesu na wanamuita Mungu,waislam wana Issah wanamwita mtume tu.
Kwenye utofauti wa wasifu kwanini ukaitumia sasa
 
Huu mjadala hauna mwisho, hakuna anaejua dini ipi ni ipi lakini sote tunajua ili kwenda mbinguni ni lazima utende wema, na dini zote zimeweka wazi ni vitu gani usifanue na nini ufanye ili uende mbinguni. Tenda wema, Toa sadaka, Fanya ibada, Mengine ni rehema za mungu. Warabu walileta uislamu, wazungu walileta ukristo. Hii mada tuwaachie wao. Humu hakuma anaejua Quran iliandikwa vipi ila ukiulizwa utasema ulichoambiwa, the same na biblia. So hii mada ni waste of time
Hapo kwenye "Fanya ibada"
 
Kwenye utofauti wa wasifu kwanini ukaitumia sasa
hiyo nitofauti moja wapo. ila sio yenye nguvu maana hata wakristo baadhi wanaamini hivyo,ila waislam wote wanadai sio Mungu.
 
Back
Top Bottom