Huwezi kuwa tajiri namba moja duniani bila kusoma shule

😄 uzi ufungwe

Ova
Diamond anaongea sana.

Pale Kariakoo kuna watu hawajulikani kama Hans Macha ila pesa yake sio mchezo maana kumiliki tu anamiliki 1.1 ya CRDB yote, bado majengo ya waliokopa na kushindwa rudisha anayo 200+

Sasa yeye kampuni ya kubeti na hisa za redio na magari ndo anajiona kawazidi watu.

Huyu tumpe yule Mama wa Vitenge ambaye alinunua ghorofa kwa Bilioni 7 sasa anazivinja
 
Kweli kabisa maneno mengi
Mimi nachojuwa wenye hela huwa hawaongei

Ova
 
Elimu hii inayotuambia binadamu wa kwanza alikua nyani zeni akawa anabadilika na kuwa binadamu 😃😃😃 nyiee
 
Ukiwa tajir unaweza ukawa msomi ndani ya dk chache lkn usomi hauwez kukufanya kuwa tajir dk chache tafakarii
 
Kusoma elimu ipi?
Elimu-binafsi ( self-education ) ndo inaweza kumfanya mtu kuwa tajiri maana hii ndo hutoa mgunduzi asilia .
Elimu ya darasani ( formal-education) inaweza kuwasaidia watu kuajiriwa na mtu mwenye elimu-binafsi .
 
Nachelea kusema wewe ndio unahitaji elimu maradufu na itachukua muda sana kwako sababu uelewa wako ni mdogo sana... Nani kasema shule hazina maana ? Pitia kwanza hilo andiko litakusaidia na utagundua Education / Elimu haianzii wala kuishia shule.... Na fikra kama zako ndio maana tumekuwa na a Lot of Uneducated people with Certificates...

Tufunge shule zote sababu mtu unaweza jifunzia mtaani na kupata elimu
 
Hicho ndicho ulichoelewa ? Kweli ni mgumu sana kuelewa..., Shule zisifungwe shule ni muhimu sana sio wote wanaweza kujifundisha wenyewe (self taught) kwahio shule pamoja na kupata elimu unapata networking na kujenga mahusiano na majadiliano..., LAKINI narudia tena na tena Shule sio Mwanzo wa kujifunza au Mwisho wa kujifunza kama wewe unategemea kwamba ukiwa shule ndio una absorb knowledge na ukiwa nje ya shule hauongezi knowledge huenda ndio maana uelewa wako seems to be lacking....
 
Kuna ukweli flani ukiona mtu ni tajiri sana na shule haipo anaishi maisha ya hovyo sana na kutokujiamini yaani inferiority complex.Hata akiwa mbunge anatumia muda mwingi kusema yeye ni wa darasa la saba .
Yuko mbunge mmoja namkubali sana shule hana ila akajiendeleza ila siku moja alisema kuwe na utaratibu wa kutoa nusu degree yaani mfano unatakiwa usome miaka 4 ukafukuzwa sababu ya kufeli basi upewe nusu degree nikajua mzee wa watu ni sababu akili yake imemtuma vile hakuwa na elimu ya kutosha.
Wote hawa wawili niliowataja wako vizuri sana kwenye siasa hata kifedha nawakubali kwa kweli wanaleta hamasa ndani ya bunge na bashasha kwa point zao.
Yuko mzee mmoja alifia kwenye guest yake na mabulungutu ya hela
yuko mwingine ana ngombe 5000 lakini analalia ngozi ya ngombe
Zuckeberg,Elon Musk,Bill Gate,Dangote,Mo Dewji wote hawa ni wasomi wazuri tu na ndio maana biashara zao ziko kimataifa.
 
Wewe ulikua unaponda elimu ya darasani nikakuambia tufunge shule umebadilsha gia tena

Watanzania mnataka nini hamjui
shule ya formal education hamuitaki basi tufunge shule ziwe sehemu za biashara watu wajifunzie mtaani hamtaki which is which

Nikusaidie wakati unawasifie wasiosoma na wanamafanikio usiiponde elimu kama ulivyofanya mwanzo sababu huo ni uzwazwa
 
Huu ni ukweli tu ulio wazi.

Dunia itabaki kutawaliwa na wasomi mpaka Yesu anarudi.

Huwezi kuwa Tajiri namba moja duniani bila kusoma shule.

Pia soma: Hili la Diamond kujihakikishia kuwa atakuwa tajiri namba moja duniani linaashiria nini katika ulimwengu wa giza?

Katika dunia ya sasa usitegemee kuwa Tajiri namba moja duniani bila kujua hesabu.

Ukijua hesabu na kuzitumia kama zinavyotaka unaweza kuwa mbali na hapo sahau.

NIMEFUNGA UZI

Meneja Wa Makampuni
Wewe ni Mungu?wengi waliomilki Dunia walisoma?
Mansa Mussa alisoma wapi?
Bill Gates ni college dropout
Mark Zuckerberg nk.
Mwenyezi Mungu ndiyo mwenye maamuzi..Kama kijana ameona anamaono hayo ni sawa.
Ni Bora kufikiria kujenga ghorofa ya kufika mawinguni hata ukishindwa basi ukomee ghorofa hata 100...
Anaweza akaishia kuwa tajiri wa kwanza Africa ambayao pia inamuweka meza moja na matajiri wa Dunia kama alivyo Dangote hadi kwenye harusi za nyumbani kwake huwakosi wenzake kina bill Gates
 
Kuna ukweli flani ukiona mtu ni tajiri sana na shule haipo anaishi maisha ya hovyo sana na kutokujiamini yaani inferiority complex.Hata akiwa mbunge anatumia muda mwingi kusema yeye ni wa darasa la saba .
Yuko mbunge mmoja namkubali sana shule hana ila akajiendeleza ila siku moja alisema kuwe na utaratibu wa kutoa nusu degree yaani mfano unatakiwa usome miaka 4 ukafukuzwa sababu ya kufeli basi upewe nusu degree nikajua mzee wa watu ni sababu akili yake imemtuma vile hakuwa na elimu ya kutosha.
Wote hawa wawili niliowataja wako vizuri sana kwenye siasa hata kifedha nawakubali kwa kweli wanaleta hamasa ndani ya bunge na bashasha kwa point zao.
Yuko mzee mmoja alifia kwenye guest yake na mabulungutu ya hela
yuko mwingine ana ngombe 5000 lakini analalia ngozi ya ngombe
Zuckeberg,Elon Musk,Bill Gate,Dangote,Mo Dewji wote hawa ni wasomi wazuri tu na ndio maana biashara zao ziko kimataifa.

Naomba nikuulize

Gsm ana inferiority complex?

Niambie professor gani anamzidi Gsm kwa chochote ?

Je Kishimba inferiority complex ?

Niambie professor gani anamzidi kishimba kwa chochote ?

Je Abood ana inferiority complex?

Je Shabiby ana inferiority complex?

Niambie professor gani anawazidi mali hao watu ?
 
Wewe ulikua unaponda elimu ya darasani nikakuambia tufunge shule umebadilsha gia tena
Narudia tena una shida kubwa ya uelewa chukua majibu yote ambayo nimejibu humu onyesha wapi nimeponda elimu Iwe ya Darasani au kwenye Kichuguu
Watanzania mnataka nini hamjui
shule ya formal education hamuitaki basi tufunge shule ziwe sehemu za biashara watu wajifunzie mtaani hamtaki which is which
Aliyesema hatutaki shule au shule zifungwe ni nani ? Kitu ambacho hujui Elimu ni muhimu na elimu sio kama maji unakwenda shule unachota na kuondoka elimu ni muendelezo wa kujifunza mpaka siku unaingia kaburini
Nikusaidie wakati unawasifie wasiosoma na wanamafanikio usiiponde elimu kama ulivyofanya mwanzo sababu huo ni uzwazwa
Kwahio unadhani ambao hawana vyeti certificates hawasomi ? Huo ndio uzwazwa sasa ninaokwambia na niliokua nakwambia tangia mwanzo.....

'The man who does not read has no advantage over the man who cannot read.'

Sasa wewe kama unajiona superior sababu una cheti kinasema wewe ni doctor wa kitu fulani na kudharau watu ambao wanafanya kitu katika industry yao kwamba unawazidi wakati wao wana experience na elimu ya hicho kitu kukuzidi wewe..., its being hubrus to say the least
 
Naomba nikuulize

Gsm ana inferiority complex?

Niambie professor gani anamzidi Gsm kwa chochote ?

Je Kishimba inferiority complex ?

Niambie professor gani anamzidi kishimba kwa chochote ?

Je Abood ana inferiority complex?

Je Shabiby ana inferiority complex?

Niambie professor gani anawazidi mali hao watu ?
hatuangaliii kuzidiana hapa MUNGU sio mchoyo hata siku moja hata Canal Sander wa Marekani mwenye KFC hakuwa na elimu kubwa lakini alikuwa tajiri sana.
Kwanza kwa taarifa yako ma prof asilimia kubwa ni watu hatuwezi sema ni masikini ila maisha yao ni ya kawaida sana na wengine ni masikini kabisa unakuta hata hana nyumba wala gari.
Ninachomaanisha hapa ni ile hali ya kujiamini.
Kubali kataa ukweli ni ule ule utajiri wa msomi aliyebobea na ambaye shule ni kidogo kuna tofauti kubwa mno.
Hatushindani kwa pesa hapa hata mimi naandika hapa ni msomi mzuri tu lakini mawe sina nina ya mboga tu kubadili
 
Narudia tena una shida kubwa ya uelewa chukua majibu yote ambayo nimejibu humu onyesha wapi nimeponda elimu Iwe ya Darasani au kwenye Kichuguu

Aliyesema hatutaki shule au shule zifungwe ni nani ? Kitu ambacho hujui Elimu ni muhimu na elimu sio kama maji unakwenda shule unachota na kuondoka elimu ni muendelezo wa kujifunza mpaka siku unaingia kaburini

Kwahio unadhani ambao hawana vyeti certificates hawasomi ? Huo ndio uzwazwa sasa ninaokwambia na niliokua nakwambia tangia mwanzo.....

'The man who does not read has no advantage over the man who cannot read.'

Sasa wewe kama unajiona superior sababu una cheti kinasema wewe ni doctor wa kitu fulani na kudharau watu ambao wanafanya kitu katika industry yao kwamba unawazidi wakati wao wana experience na elimu ya hicho kitu kukuzidi wewe..., its being hubrus to say the least
Kuna sehemu yeyote kwenye uzi ambayo nimekuambia nina cheti au nimekuambia kiwango cha elimu yangu ebu nionyeshe nasubiria
 
Back
Top Bottom