Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HUWEZI LAZIMISHA MWANAMKE AKUHESHIMU, MWANAMKE ANAMHESHIMU MWANAUME ANAYEMPENDA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Wanaume wengi hudhani kúmpiga Mwanamke ndio humfanya Mwanamke awe mtiifu na mwenye heshima. Wengine huwafokea na kuwatukana na kuwatolea maneno makali kwa kudhani kufanya hivyo ndio humfanya Mwanamke amheshimu.
Elewa Mwanamke sio mtoto mpaka umpige. Elewa, Mwanamke ni kiumbe pekee chenye kisasi. Elewa Mwanamke hawezi kusahau jambo baya lolote hata moja ambalo umemfanyia hasa ukimpiga àu kumfanyia ushenzi wowote.
Wazee wetu wengi wakifikisha miaka kuanzia hamsini (50+yrs) huanza kupewa kiinua mgongo chao kwa yale yote waliyofanyia Wake zao kipindi cha nyuma.
Sasa kijana anapompiga mkewe, au kumfokea kwa maneno ya kudhalilisha, alafu akaona Mwanamke wake amekaa kimya wanadhani ndio heshima imerudi. Kumbe hawa viumbe wamejiweka kiporo ambacho wanauhakika watakinywea na chai ya moto yenye tangawizi na mdalasini. Wakati huo kiporo ambaye ni wewe utakuwa wabaridi umepoa unakaribia kuchacha.
Asije akakudanganya mtu kuwa kukusanya pesa pekee kutakuondoa na kadhia ya mkeo uliyemnyanyasa. Njia pekee labda ni kupeana talaka. Vinginevyo hata uwe nani, nasema hata uwe nani. Lazima upasuke.
Wengine hufikiria heshima wataipata kwa kutoa pesa, na hiyo hupelekea kutafuta pesa kwa nguvu zote na kuwapa wake zao lakini mwisho wa siku heshima hawapewi.
Taikon Master kama mtaalamu wa saikolojia, falsafa, na mwanasosholojia ninakuambia kuwa kwenye hii dunia Mwanamke hawezi kukuheshîmu kisa unampa pesa, au kukuheshîmu kisa unampiga. Huwezi force heshima ya Mwanamke kwako.
Mwanamke anamheshimu mwanaume anayempenda bila kujali mwanaume huyo yupo katika nafasi ipi,
Hata uwe Rais, hata uwe mfalme, hata uwe mkuu majeshi, hata uwe nani. Mwanamke ambaye utamuita mkeo au ambaye utalala naye uchi mkakutana kimwili hawezi kukuheshîmu kisa hicho cheo chako au mapesa yako.
Mwanamke huogopa zaidi kumsaliti mwanaume anayempenda kuliko kitu chochote.
Kuwa mkuu wa majeshi, au Rais au jambazi hakumuogopeshi Mwanamke asiku-cheat.
Elewa Mwanamke woga wake upo katika hisia zake. Mwanamke anaogopa zaidi kupoteza kile kinachompa furaha.
Elewa, Mwanamke anaheshimu kile kinachompa furaha. Na mtu anayempenda raha ndiye anayempa raha.
Ukiona upo kwenye kundi la wale wanaume wanaodhani wanawake hawatoi pesa zao kwa wanaume jua huyo Mwanamke uliyenaye hakupendi. Na kama hakundi automatically hakuheshimu wala kukutii ila anakuigizia.
Ukiona upo na mwanamke ambaye chake ni chake lakini chako ni Chenu be aware, huyo hakupendi na automatically hakuheshimu ila anachokifanya ni unafiki.
Mtu anayesema Mwanamke hapendi lakini anapaswa awe mtiifu anashindwa kuelewa kuwa Utiifu ni matokeo ya upendo uliopitiliza.
Kumaanisha Mwanamke anatakiwa akupende sana ili awe mtiifu kwako. Huwezi mtii mtu usiyempenda. Kama unamtii mtu usiyempenda tafsiri yake ni kuwa unamwogopa.
Kuna heshima au Utiifu na kuja hofu au Woga.
Elewa kuwa hakuna pesa yoyote ya kununua upendo wa Mwanamke, asije akakudanganya mtu yeyote.
Utapigwa na kitu kizito. Upendo haununuliwi.
Elewa, Wanawake huipata pesa kipaombele baada ya ku - disappontiwa, kuumizwa na kusalitiwa na wanaume wanaowapenda.
Mwanamke yeyote aliyeumizwa na mwanaume aliyempenda sana hubadilika kwa kiwango cha juu.
Elewa huwezi fanya lolote kumpa furaha Mwanamke ambaye hana furaha. Furaha ya Mwanamke ipo kwa mwanaume anayempenda.
Usijesema sikukwambia. Hivyo ndivyo utakavyoishi ña Wanawake Mwanangu
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam