View attachment 3089373Ni ngumu kunishawishi kuwa Nyerere alikuwa kiongozi bora ngumu sana.
Mtu aliyetengeneza taifa la misukule kamwe hawezi kuwa kiongozi bora.
Propaganda kubwa imefanyika kumchora Nyerere mtakatifu na genius taifa halijawahi kupata mtu wa hivyo.
Indoctrination imefanyika toka utotoni Nyerere kuonekana bora kila upande.
Jinsi watanzania tulivyo ni masikitiko akili zimeoza.
Huwezi kuwa bora kama unageuza watu wako misukule ili uwatawale vyema.
Nyerere Kama binadamu mwingine yoyote yule, alikuwa ana mazuri yake lakini pia alikuwa ana mabaya yake, ingawaje kwa kiasi kikubwa mapungufu yake mengi yalikuwa yanavumilika ukimlinganisha na wenzake wengine wote waliomfutia.
Baadhi ya mabaya au ubovu wa Mwl. Nyerere:-
1. Kuiga, Kuanzisha na kuendeleza Sera na Itikadi Mbaya kabisa ya Siasa za Ukomunisti/Ujamaa hapa Tanzania.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kujenga Msingi mbovu wa Taifa la hovyo kabisa lililopo hivi sasa.
Itikadi na Sera ya Ukomunisti/Ujamaa ikaja kushindwa vibaya Sana huku yeye mwenyewe akishuhudia kwa macho yake kushindwa kwa itikadi yake aliyoileta hapa Tanzania kutoka kwa marafiki zake wa China, Urusi na Cuba.
2. Kutengeneza Taifa la Watu waoga, Wanyonge, dhaifu wa fikra wasiojitambua na Wala wasioweza kuhoji. Taifa la watu 'misukule'.
3. Kutengeneza au kuunda nchi isiyokuwa na Mipango-miji, hususani kupitia kwenye Sera yake mbaya kabisa ya ujamaa/Ukomunisti. Sera au Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti ndio ilikuwa chanzo Cha Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, the Worse Operation that completely destroyed the Country and Town Planning process within the Country.
Arusha Declaration and Operation Vijiji also led to the Death of Real Estate Industry and its development.
Kupitia Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti, Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, Watu wengi sana walinyang'anywa Ardhi zao pamoja na majumba yao waliyokuwa wakimiliki. Nyumba nyingi sana za Watu zilitaifishwa, Leo hii nyumba hizo zinamilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC).
4. Kutuletea Katiba ya nchi ambayo ni mbaya kabisa, isiyofaa na ambayo imesababisha na inaendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa Raia. Katiba mbaya ambayo imewatengeneza Watawala wa nchi hii kuwa 'Miungu Watu.'