Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Vyote unavyoviona ni vibaya ni kwa sababu unavitazama katika mtazamo wa 2024, yeye Mwalimu na wasaidizi wake waliitazama dunia ya mwaka 1980 kurudi nyuma.Baadhi ya mabaya au ubovu wa Mwl. Nyerere:-
1. Kuiga, Kuanzisha na kuendeleza Sera na Itikadi Mbaya kabisa ya Siasa za Ukomunisti/Ujamaa hapa Tanzania.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kujenga Msingi mbovu wa Taifa la hovyo kabisa lililopo hivi sasa.
Itikadi na Sera ya Ukomunisti/Ujamaa ikaja kushindwa vibaya Sana huku yeye mwenyewe akishuhudia kwa macho yake kushindwa kwa itikadi yake aliyoileta hapa Tanzania kutoka kwa marafiki zake wa China, Urusi na Cuba.
2. Kutengeneza Taifa la Watu waoga, Wanyonge, dhaifu wa fikra wasiojitambua na Wala wasioweza kuhoji. Taifa la watu 'misukule'.
3. Kutengeneza au kuunda nchi isiyokuwa na Mipango-miji, hususani kupitia kwenye Sera yake mbaya kabisa ya ujamaa/Ukomunisti. Sera au Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti ndio ilikuwa chanzo Cha Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, the Worse Operation that completely destroyed the Country and Town Planning process within the Country.
Arusha Declaration and Operation Vijiji also led to the Death of Real Estate Industry and its development.
Kupitia Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti, Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, Watu wengi sana walinyang'anywa Ardhi zao pamoja na majumba yao waliyokuwa wakimiliki. Nyumba nyingi sana za Watu zilitaifishwa, Leo hii nyumba hizo zinamilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC).
4. Kutuletea Katiba ya nchi ambayo ni mbaya kabisa, isiyofaa na ambayo imesababisha na inaendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa Raia. Katiba mbaya ambayo imewatengeneza Watawala wa nchi hii kuwa 'Miungu Watu.'
Tangu ameaga dunia ni miaka 25 robo karne, sisi tulioachwa duniani tumefanya nini kuubadili huo ubaya ili uwe ni uzuri?.