1.)Ukomunisti lilikuwa wazo zuri ila lisilotekelezeka badala ya kulialia tungejifunza china mbona wao wana maendeleona sio waoga? Urusi pia?
Tupe nchi ya afrika ilofanikiwa saana kwasababu ya ubepari!!
2.)Ukomunisti ulileta uoga? Mbona china,Cuba,urusi si waoga? Kama ni uoga basi South Afrika ndowangekuwa waoga haswa. Mwalimu mmoja anawezaje kufanya nchi iogope
Tatizo nihao watu...
3.)sera ya kuweka watu pamoja lengolilikuwa zuri (ili wapate huduma kirahosi) ila ilikosewa kiutendaji kama vile binadamu tunavyokosea mambo kadhaa ktk maisha.
Hakuna kiongozi ni malaika so kukosea ni ubinadamu labda uwe muoga kujaribu mambo mapya
4.) Ni upumbafu mtupu kumlaumu rais wa kwanza kuhusu katiba. Vijana amkeni mdai katiba mpya msilaletake mletewe kitandani!!
Poor minds hulaumu kwanini hawajapewa vitu vizuri alakini best minds huvitafuta na kuvipambamia vilivyo vizuri...
You're completely wrong and out of point.
1. (a) Endapo kama Ukomunisti lilikuwa wazo zuri kama unavyodai, Je, inawezekana vipi wazo liwe zuri halafu lishindwe kutekelezeka? How comes? Uzuri wake ni upi Basi?
(b) China Wana sera mseto, hawana utawala wenye itikadi Moja tu ya siasa za ukomunisti, Bali wamechanganya itikadi mbalimbali kama vile Ukomunisti, Ubepari. China walisha-adopt sera ya Ubepari tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960 hata Urusi nao wapo hivyo hivyo, that's why ndani ya China au Urusi kuna makampuni makubwa Sana ya kutoka nchi za kibepari hususani nchi za Magharibi, e.g. Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Canada, Australia, n.k.
Aidha, hata kwenye hizo nchi za Magharibi nako pia kuna Makampuni makubwa Sana ya biashara kutoka China na Urusi. Na biashara kwenye makampuni hayo zinafanyika chini ya misingi ya siasa za kibepari, Wala siyo kwa misingi ya Ukomunisti. Sera za kibepari chini ya taasisi za kimataifa kama vile WB, IMF, WTO, n.k ndizo zinazotumika katika kuendesha biashara Kati ya mataifa hayo.
(c) Nchi za Afrika ya Kusini, Nigeria, Morocco, na Misri zilizopo barani Afrika ndizo baadhi ya nchi ambazo zinefanikiwa zaidi kutokana na Sera za Siasa za Ubepari. South Africa ni mfano mzuri zaidi kati ya hizo kwani Utawaka wa Makaburu uli-adopt Ubepari tangu mwishoni mwa miaka ya 1800's, hususani kuhusiana na suala zima la biashara ya madini ya Vito.
2. Ukomunisti huwafanya Watu kuwa dhaifu kifikra, hujenga raia waoga kwa watawala wao, husababisha raia kuwa wanafiki, wasioweza kuhoji, raia-misukule, n.k.
Aidha, South Africa siyo nchi ya kikomunisti.
3. Sera ya kuwaweka Watu pamoja aliyofanya Mwl. Nyerere chini ya Siasa za kikomunisti/ujamaa kamwe haikuwa na lengo zuri kwani iliua kabisa Real Estate Industry katika nchi hii.
Endapo kama Sera hiyo ingefanyika kwa kuzingatia misingi imara ya ubepari, basi sera hiyo ingetoa matokeo mazuri zaidi, na tena ingeing'arisha nchi kwa kuwa na Mipango-miji Bora katika bara hili.
4. Nyerere anastahili kubeba lawama nyingi zaidi kwa kuifanya nchi hii kuwa na misingi mibovu karibia kwenye kila nyanya za maisha ya Watu, ukianzia na kutunga Katiba ya nchi ambayo ni mbaya na isiyofaa.